SHINYANGA HOI AGIZO LA RAIS MAGUFULI
![]() |
| Wanafunzi wakiendelea na Masomo huku migongo ikiwa hoi baada ya shule yao kutokuwa na madawati |
SOMA HABARI KWA KINA
Serikali ya mkoa
wa Shinyanga imeshindwa kukamilisha agizo la Rais John Magufuli la kutatua
tatizo la uhaba wa Madawati kwa shule za msingi na sekondari ambapo bado
inakabiliwa na upungufu wa madawati 9,545
Rais Magufuli
alitoa agizo hilo la kukamilisha uhaba wa madawati kwa shule zote nchini ambapo
mwisho wa kukabidhi madawati hayo ilipangwa kuwa june 30 huku mkoa wa Shinyanga ukishindwa kutekeleza
agizo hilo.
Akitoa takwimu
hizo jana Ofisa Elimu taaluma mkoa James Malima amesema katika shule za msingi kuna upungufu wa
madawati 7,310, sekondari 2,235 na kufanya jumla kuu kuwa ni 9,545 huku
utengenezaji wa madawati hayo kwenye halimashauri bado ukiendelea ambapo badhi
yao zimeshavuka lengo.
Aidha Malima
ametaja halmashauri ambazo zimetekeleza agizo hilo la Rais Magufuli la kumaliza
tatizo la uhaba wa madawati kuwa ni halmashauri ya mji wa kahama, na
msalala,ambazo zImemaliza tatizo hilo kwa shule zote za msingi na sekondari.
Pia Malima
amezitaja halmashauri za Ushetu ambayo imekamilisha tatizo la madawati kwa shule
za sekondari pekee, huku shule za msingi ikiwa na upungufu wa madawati 387,
shinyanga manispaa nayo ikabiliwa na uhaba wa madawati 2,033 kwa shule za
msingi ambapo sekondari imeshatekeleza agizo hilo.
Hata hivyo
amezitaja halmashauri mbili ambazo hazijatekeleza agizo hilo kwa shule zote
kuwa ni kishapu ambapo shule za msingi inakabiliwa na uhaba wa madawati
2,112,sekondari 1,965, Shinyanga vijijini msingi 2,778,sekondari 270 na hivyo
kufanya mkoa kuwa na upungufu wa madawati 9,545.
Na Marco Maduhu -Msukuma Blog

