ALBINO WAPEWA MFUNZO YA KUTENGENEZA DAWA YA MALARIA
Watu wenye ualbino mjini Shinyanga wamepewa mafunzo ya ujasiriamali ya kutengeneza bidhaa mbalimbali, ikiwamo dawa asili ya kutibu ugonjwa wa Malaria, ambazo watakuwa wakiziuza na kujipatia kipato ambacho kitaendesha maisha yao na kukuza uchumi katika familia zao.
Mafunzo hayo yametolewa na Shirika la dawa za asili Anamed kutoka Jijini Mwanza ambayo yalitolewa kwa awamu mbili kuanzia Julai mwaka jana na kuhitimishwa Leo Mei 29 mwaka huu, ambayo yana mlengo wa kuwawezesha kuwa inua kiuchumi kupitia bidhaa hizo.
Akizungumza kwenye kuhitimisha mafunzo hayo Katibu wa Chama cha watu wenye Ualbino mjini Shinyanga (TAS) Lazaro Aniel, alisema baada ya kuona Albino wanakabiliwa na hali duni ya kimaisha, ndipo wakaona ni vyema kutafuta wafadhiri ili waweze kupewa mafunzo hayo ya ujasiriamali ambayo yatawakwamua kiuchumi.
“Mafunzo haya ni Muhimu sana kwetu ambapo yataweza kutuinua kiuchumi na kuondokana na hali duni ya kimaisha, ikiwa na sisi tutakuwa na shughuli za uzalishaji mali ambazo zitatuingizia kipato, na tunaiomba jamii ituunge mkono pale tutakapo kuwa tunauza bidhaa zetu,”alisema Anaeli
Aidha alita mafunzo ambayo yametolewa kuwa ni utengenezaji wa Sabuni dawa za kuogea, Meno,Jiwe la nyoka, Batiki, Lotion, Lipsstick, mafuta ya kutibu magonjwa ya ngozi, pamoja na dawa asili za kutibu ugonjwa wa malaria.
Naye mkufunzi wa mafunzo hayo ya ujasiriamali kutoka Shirika hilo la Anamed Dk Peter Feleshi, alisema bidhaa hizo ambazo wanazitengeneza pia zina faida kwao ambazo zinauwezo wa kuwatibu magonjwa ya Ngozi, na Malaria, na kutoa wito kwao elimu hiyo waitumie vyema kuwakomboa kimaisha.
Nao baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo Barnaba Mhoja na Rehema Samweli, kwa nyakati tofauti walisema wamefarijika kupatiwa ujuzi huo, ambao utawafanya kubadilisha mfumo wa maisha yao na kuondokana na umaskini.
TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA
Mkufunzi wa mafunzo hayo ya ujasiriamali DK Peter Feleshi wa kwanza mkono wa kushoto, akiwa na watu hao wenye Ualbino akitoa somo la utengenezaji bidhaa mbalimbali iliwapate ujuzi na kuweza kuviuza na hatimaye kuwaingizia kipato.
Mkufunzi wa mafunzo hayo ya ujasiriamali Peter Feleshi akiendelea na utoaji wa somo hilo la ujasiriamali kwa watu hao wenye Ualbino katika ukumbi wa Bwalo la Polisi mjini Shinyanga.
Mkufunzi wa mafunzo ya ujasiriamali DK Peter Felesh akiendelea na mfunzo kwa vitendo ambapo hapo wanatengeneza Lipstick ,akiwa na Mwanafunzi Elias Manumbu.
DK Peter Feleshi akionyesha mimie ambayo wanatumia kutengeneza bidhaa hizo za ujasiriamali ikiwamo na dawa asili ya kutibu ugonjwa wa Malaria.
Mafunzo ya ujasiriamali yakiendelea.
Mafunzo ya ujasiriamali yakiendelea hapo wakikata Lebo kwa ajili ya kuweka kwenye bidhaa walizozitengeneza.
Mkufunzi wa mafunzo hayo ya ujasiriamali Dk Peter Feleshi akiendelea na mafunzo kwa vitendo akiwa na Mwanafunzi Leah Wiliamu.
Mafunzo ya ujasiriamali yakiendelea
Baadhi ya bidhaa zikiwa zimekwisha tengenezwa kwenye mafunzo hayo ya Ujasiriamali kwa vitendo.
Na Marco Maduhu,ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga