MBUNGE MASELE APEWA MTIHANI UWEKEZAJI VIWANDA SHINYANGA


Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele, amepewa mtihani wa uwekezaji viwanda mkoani hapa, kutokana na nafasi kubwa aliyoipata ya kuchaguliwa kuwa makamu wa Rais wa Bunge la Afrika, ambapo atakuwa na fursa ya kuzungumza na marais wanchi mbalimbali,wafanyabiashara wakubwa na kuja kuwekeza viwanda.


Hayo yalizungumzwa Mei 26,2018 mjini Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara na Mbunge wa Jimbo la Msalala wilayani Kahama Ezekiel Maige, wakati akitambulisha wabunge walioambatana na mbunge Masele kuja jimboni kwake kuwa shukuru wananchi kwa kumchangua kuwa mbunge, na hatimaye kupata nafasi hiyo Muhimu kwa watanzania wote.


Maige alisema mkoa wa Shinyanga ni mkoa ambao una fursa nyingi ya uwekezaji pamoja na kuwa na Rasilimali za kutosha, lakini hauna viwanda ambavyo vitatumia Rasilimali hizo na hatimaye kuupatia maendeleo, sambamba na kunyanyua uchumi wa wananchi, ikiwa na vijana kupata ajira kwenye viwanda hivyo.


“Mbunge Masele kwa nafasi hiyo kubwa uliyoipata ya umakamu wa Rais wa Bunge la Afrika, hivyo tunatarajia mkoa wa Shinyanga utapata sasa Kiwanda cha Nyama, Ngozi, Maziwa, chuo cha madini, hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga, pamoja na kutuletea mfumo wa kilimo cha umwagiliaji,”alisema Maige.


"Naomba viongozi wa serikali mkoani Shinyanga muandike maandiko mbalimbali ya kuomba miradi zikiwamo fursa za uwekezaji ikiwa kwa sasa tuna mtu ambaye atatusaidia kupata miradi hiyo kwa urahisi,"aliongeza.


Naye Mbunge Masele alimtoa wasiwasi Maige pamoja na wananchi wa mkoa wa Shinyanga, kuwa kutokana na nafasi hiyo kubwa aliyoipata, atahakikisha unatumia mbinu zote kuwa shawishi wawekezaji kuja kuwekeza mkoani humo pamoja na Tanzania kwa ujumla, ili nchi ipate kupiga hatua kimaendeleo kupitia uchumi wa viwanda.


Pia aliwaomba radhi wananchi wa jimbo la Shinyanga mjini kwa kutokuwepo jimboni humo kwa kipindi kirefu, kwa madai alikuwa akiitafuta nafasi hiyo muhimu ya umakamu wa Rais wa Bunge la Afrika, ambayo itakuwa chachu ya maendeleo kwa jimbo hilo na taifa kwa ujumla.


Nao baadhi ya wananchi wa jimbo hilo la Shinyanga mjini akiwamo Joyce Malieta, walimtaka Mbunge huyo Masele kuacha tabia ya kutelekeza Jimbo kwa kipindi Kirefu, ikiwa walimchangua kutatua kero zao, na nafasi hiyo kubwa aliyoipata isiwe ndiyo kisingizio cha kutoonekana kabisa jimboni na kutotekeleza ahadi zake hadi kwenye kipindi cha Uchaguzi.


Aidha wabunge wengine waliomsindikiza Mbunge Stephen Masele kuja kushukuru wapiga kura wake kwa kumchangua kuwa mbunge wa Jimbo hilo la Shinyanga mjini, ni Seif Gulamali wa Jimbo la Manoga, Jitu Son, Babati, pamoja na Jackline Msongozi mbuge wa Vitimaalumu mkoani Ruvuma.

TAZAMA HABARI PICHA HAPA CHINI


Mbunge wa jimbo la Msalala wilayani Kahama Ezekieli Maige akisalimia na wakazi wa jimbo la Shinyanga mjini kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge Stephen Masele, na kuwataka wananchi wa endelee kumwamini mbunge wao.

Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele ambaye pia ni Makamu wa Rais Bunge la Afrika akizungumza na wakazi wa jimbo la Shinyanga mjini, na kuwataka wamvumulie ikiwa kwa sasa atakuwa na majukumu mengi na kutokuwepo jimboni muda wote.


Wananchi wa jimbo la Shinyanga mjini wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge wao Stephen Masele.

Wananchi wa Jimbo la Shinyanga mjini wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge wao Stephen Masele ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika .

Baadhi ya madiwani wa CCM halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge Stephen Masele wa kushukuru wananchi kumchangua kuwa mbunge na hatimaye kupata nafasi ya kuwa Makamu wa Bunge la Afrika.

Mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele mkono wa kushoto akitetea jambo na Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Charles Sangula kabla ya kwenda kuzungumza na wapiga kura wake na kuwashukuru kwa kumchangua kuwa mbunge wao.

Mbunge wa jimbo la Babati Jitu Soni akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara amewataka wakazi wa jimbo hilo la Shinyanga mjini kuendelea kumwamini mbunge wao kwa atawaletea maendeleo makubwa.

Mbunge wa jimbo la Msalala Ezekiel Maige mkono wa kushoto akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele kabla ya kwenda kuzungumza na wapiga kura wake.

Burudani ikitolewa kwenye mkutano huo wa hadhara wa mbunge Stephen Masele wa kuwashukuru wapiga kura wake na kujitambulisha kwao kupata nafasi hiyo ya umakamu wa Rais wa Bunge la Afrika.

Mbunge wa jimbo la Manonga Seif Gulamali akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara alimpongeza mbunge Stephen Masele kwa nafasi hiyo aliyoipata na kuwataka wananchi wa jimbo la Shinyanga wajivunie kuwa na mbunge makini ambaye atawatatulia kero zao.

Burudani ikitolewa kwenye mkutano huo wa hadhara yenye maudhui ya kumpongeza Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele kwa kupata nafasi ya kuwa Makamu wa Rais Bunge la Afrika.

Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele mkono wa kushoto akishikana mkono na mbunge wa jimbo la Babati Jitu Soni wakati akienda kuzungumza na wapiga kura wake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Zimamoto mjini Shinyanga.
Mbunge wa Vitimaalumu kutoka mkoa wa Ruvuma Jackline Msongozi akiwataka wananchi wa jimbo la Shinyanga mjini kuwa puuza watu ambao wamekuwa wakidai mbunge ametelekeza jimbo ikiwa Mwanaume ni yule ambaye anatafuta na siyo wa kukaa nyumbani, ambapo Mbunge Masele ni mtafutaji na hatimaye amepata nafasi nzuri ya umakamu wa Rais wa Bunge la Afrika ambayo ni Sifa kwa watanzania wote na wananchi wa Shinyanga na kutarajia kupata maendeleo.

Wananchi wa Jimbo la Shinyanga mjini wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge Stephen Masele.

Mbunge wa jimbo la Msalala Ezekiel Maige mkono wa Kushoto akimpongeza Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele mara baada ya kumaliza kuzungumza na wapiga kura wake na kuwa ahidi kupata Neema kubwa ikiwa kwa sasa ana nafasi kubwa ya Umakamu wa Rais wa Bunge la Afrika.

Awali mbunge Stephen Masele akiingia kwenye uwanja wa Zimamoto mjini humo akipungua wapiga kura wake mkono, akiwa karibu na katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangula.

Wananchi wa Jimbo la Shinyanga mjini wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge wao Stephen Masele.


Waandishi wa habari nao wakiwa kwenye mkutano huo wa Mbunge Masele, wakwanza kulia ni Frola Masalu wa Radio Faraja, akiwa na Sam Bahari ambaye ana angalia Camera wa Gazeti la Mtanzania.

Wananchi wa Jimbo la Shinyanga mjini wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge wao Stephen Masele.

Wananchi wa Jimbo la Shinyanga mjini wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge wao Stephen Masele.

Wananchi wa Jimbo la Shinyanga mjini wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge wao Stephen Masele.

Wananchi wa Jimbo la Shinyanga mjini wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge wao Stephen Masele.

Wananchi wa Jimbo la Shinyanga mjini wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge wao Stephen Masele.

Baadhi ya Madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kutoka CCM Wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge Stephen Masele.

Wana CCM wakiwa kwenye barabara ya Buhanghija Kona wakisubili kumpokea mbunge wao Stephen Masele.

Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele akiwa amewasili mjini Shinyanga tayari kwenda kuzungumza na wapiga kura wake kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja vyta Zimamoto mjini humo.


Na Marco Maduhu ,ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.





Powered by Blogger.