MBUZI 47 WAMEDAIWA KUFA KWA KULA MAJANI YENYE SUMU KUTOKA MACHUNGANI ENEO LA JESHI



Mbuzi 47 wenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni mbili mali ya bwana Sleyo Rashidi mkazi wa mjini Shinyanga, wamedaiwa kufa kwa kula majani yenye sumu katika eneo la marisho Jeshini Kata ya Kizumbi mjini hapa, sehemu ambayo mbuzi hao walikuwa wakichunga.

Imedaiwa mbuzi hao waliaanza kufa usiku wa kuamkia leo Mei 25,2018 katika kitongoji cha Busongo Kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi majira ya saa 10 usiku, ambapo sumu hiyo waliokula kutoka machungoni eneo hilo la Jeshi, ilianza kuwazidi na kuanza kufa mmoja baada ya mwingine.


Akisimulia tukio hilo mchungaji wa mifugo hiyo Daudi Dotto, alisema ilipofika majira ya saa 10 usiku alianza kusikia mbuzi wakilia, na alipo kwenda kwenye banda lao alikutana na mbwa huku mbuzi 47 wakiwa wameshakufa na matumbo yao kuvimba.


“Mbuzi hawa hua na wachunga mara zote katika eneo la Jeshini Kizumbi ambapo hua tunakatazwa, lakini kutokana na uhaba wa maeneo ya marisho hua tunachunga hivyo hivyo kwa kuiba , na majira ya jioni ni kazirudisha nyumbani  ndipo majira hayo ya usiku wakafa mbuzi 47,” alisema Dotto.


Naye Daktari wa mifugo wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Velani Mwaluko ambaye alifika kwenye eneo hilo, alisema katika uchunguzi wa awali amebaini mbuzi hao wamekufa  kwa kula majani yaliyopuliziwa Sumu, ambapo amechukua baadhi ya Nyama kwenda maabara Jijini Mwanza, ili kubaini aina hiyo ya Sumu.


Pia aliangiza Nyama hivyo isitumiwa kwa matumizi yoyote ya binadamu, ambapo kuna baadhi ya Mbuzi zilikuwa tayari zimeshaanza kuchinjwa na kuchunywa kama kitoweo, na kupiga marufuku zimwagiwe mafuta ya taa na kisha kuchimbiwa shimo kubwa na kufukuwa.

Kwa upande wake mtoto wa mmiliki wa mifugo hiyo Mudafu Hilali, alisema wana jumla ya mbuzi 91, ambapo Mbuzi 47 ndio wamekufa wenye thamani ya Shilingi Milioni 2,3 na kubaki 40, huku wanne wakiwa wamejeruhiwa na mbwa kwa kung’atwa sehemu za Shingoni na Miguuni.


Aidha Kaimu Ofisa Mifugo wa Kijiji cha Bugayambelele Kata ya Kizumbi Rashida Masawe ambaye ni mtendaji wa kijiji hicho, alitoa wito kwa wachungaji kuacha tabia ya kuchunga mifugo kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi wala kwenye mashamba ya wakulima, ili kujiepusha na adha hizo za vifo vya mbuzi kufa kwa sumu.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI



Daktari wa mifugo wa manispaa ya Shinyanga Velani Mwaluko akiangalia mbuzi 47 zilizokufa kwa madai ya kula majani yenye Sumu kutoka kwenye machungo ,mkono wa kulia ni mtoto wa mmiliki wa mbuzi hao Mudafu Hilali.

Mbuzi 47 wa bwana Sleyo Rashid wakiwa wamekufa kwa madai ya kula majani yenye sumu, wakiwa kwenye banda lao eneo la Kitongoji cha Busonga katika kijiji cha Bugayambelele manispaa ya Shinyanga.

Mbuzi aliyekufa kwa madai ya kula sumu akiwa amechinjwa tayari kwa wanazengo kugawana nyama.

Daktari wa mifugo wa manispaa ya Shinyanga Velan Mwaluko akiangalia mbuzi 47 zilizokufa kwa madai ya kula majani yenye Sumu.

Mbuzi aliyekufa kwa madai ya kula majani yenye sumu akiwa anafanyiwa uchunguzi wa awali na kubainika mbuzi hao 47 walikuwa majani yaliyokuwa na Sumu.

Daktari wa mifugo manispaa ya Shinyanga Velani Mwaluko mkono wa kulia akichunguza mbuzi hao nini kilicho wauwa na kubainika walikula majani yenye Sumu.

Mbuzi aliyekufa kwa madai ya kula majani yenye Sumu, akiwa amechunwa tayari kwa kitoweo.

Uchunaji Mbuzi ukiendelea.

Daktari wa mifugo manispaa ya Shinyanga Velani Mwaluko mkono wa kushoto akiwa na Mtoto wa mmiliki wa mbuzi hao Mudafu Hilali.

Mudafu Hilali ambaye ni mtoto wa mmiliki wa mifugo hiyo akiangalia mbuzi hao 47 wakiwa wamekufa kwa madai ya kula majani yenye sumu, wenye thamani ya Shinyanga Milioni 2.3.

Mbuzi 47 wa bwana Sleyo Rashidi mkazi wa manispaa ya Shinyanga wakiwa wamekufa kwenye banda lao, baada ya kudai kula majani yenye Sumu.

Mchungaji wa mbuzi hao Daudi Dotto akitoa maelezo kuwa mbuzi hao jana alikuwa amewachunga kwenye eneo la Jeshi lililipo Kizumbi manispaa ya Shinyanga.

Mchungaji wa mbuzi hao Daudi Dotto akiwa amebeba mbuzi kwenda kufanyiwa uchunguzi wa awali ilikubaini tatizo lililosababisha kifo chao.

Daktari wa mifugo manispaa ya Shinyanga Velan Mwaluko wa kwanza mkono wa Kushoto akiwa na baadhi ya viongozi wa Kijiji cha Bugayambelele kitongoji cha Busonga eneo ambalo mbuzi hao wamekufa kwa madai ya kula majani yenye Sumu.

Daktari wa mifugo manispaa ya Shinyanga Velan Mwaluko akiendelea na zoezi la uchunguzi kubaini kitu gani kilicho wauawa mbuzi hao 47, ambapo awali ilidaiwa kung'atwa na mbwa lakini hawakuwa na makovu na kubanika wamekula majani yaliyopuliziwa Sumu.

Uchunaji mbuzi ukiendelea.

Wananchi wa Kitongoji cha Busonga wakishuhudia vifo vya mbuzi hao 47.

uchunguzi wa awali ukiendelea.

Mbuzi 40 waliosalia kudhurika na Sumu , huku wengine Wanne wakiwa wameshambuliwa na mbwa wakati alipokwenda kufatua kitoweo pindi mbuzi hao walipokuwa wakifa mmoja baada ya Mwingine, mara baada ya kudaiwa kula majani yenye Sumu.

Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.

Powered by Blogger.