ACT- WAZALENDO WADAI UPINZANI UKIFA WANANCHI WATATESEKA



Naibu Katibu mkuu wa ACT Wazalendo Taifa Msafiri Mtemelwa akizungumza na viongozi wa chama hicho mkoani Shinyanga na kuwataka wasiteteleke na siasa zinazoendelea hapa nchini kwa kuhama hama viongozi ndani ya chama hicho bali waendelee kuwa ngangari kukijenga chama.


Soma habari kamili

Chama cha ACT-Wazalendo kimewataka viongozi wake kutotishika na namna siasa za sasa hivi nchini Tanzania jinsi zina vyoendeshwa, bali waendelee kukijenga chama na kuonyesha upinzani wa kweli, ikiwa wakiruhusu upinzani kufa wananchi watateseka kama enzi za mfumo wa chama kimoja ulivyokuwa.

Wamesema kuondoka kwa viongozi wakuu ndani ya chama hicho, isewe ndio sababu ya kuhofia chama kufa ikiwa viongozi kuhama ndani ya vyama hakukuanza kipindi hiki, bali ulianza tangu zamani lakini vyama havikufa na ndio vileendelea kuimalika, na hivyo kuwataka viongozi ndani ya chama hicho kujenga mapenduzi ya kweli.

Akizungumza leo Februari 18 mwaka huu mjini Shinyanga na viongozi wa chama hicho kabla ya kuanza mkutano wa ndani, Naibu Katibu mkuu wa ACT Wazalendo Taifa Msafiri Mtemelwa, alisema sifa ya kuwa kiongozi ndani ya chama ni kukijenga chama kuwa imara, na siyo kuwaza kununuliwa ili kuuwa upinzani ambao utawarudisha watanzania kwenye matatizo.

“Mimi nimeishi kwenye mfumo wa chama kimoja enzi za hayati Rais Mwalimu Julias Nyerere, watu walikuwa wanateseka sana pamoja na kukimbia makazi yao hasa kwenye kodi za vichwa, lakini baada ya mfumo wa vyama vingi kuingia wapinzani walipigania mambo mengi na wananchi kuishi kwa raha,”alisema Mtemelwa

Aliongeza”upinzani ndio chachu ya maendeleo hapa nchini tukisimama kwenye majukwaa na kupigania jambo Serikali inalisikiliza na kutekeleza, hivyo tukiruhusu upinzani kufa nani atawapigania wananchi, si wataishi maisha ya shinda sana na kurudi zama zile za ujima, naomba ndugu zangu tusiuwe upinzani tujenge chama.”

Naye mjumbe wa kamati kuu taifa wa chama hicho Nyangaki Shilungushela, aliwataka viongozi hao kujituma kufanya kazi za chama na kujiamini, na kubainisha chama chenye upinzani wa kweli kimebaki ACT, ambapo vyama vingine vimeshindwa kazi ya mapinduzi na kubaki kufanya siasa za maji taka.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya kampeni na uchaguzi wa chama hicho taifa Mohamed Babu, aliwataka viongozi hao pindi wanapokuwa wakifanya uchaguzi wa ndani, wachague viongozi wazuri wenye uwezo wa utendaji kazi, pamoja na kuchagua wagombea wenye sifa za uongozi katika chaguzi zijazo mwaka (2019-2020)



TAZAMA PIA HABARI PICHA HAPA CHINI


Naibu Katibu mkuu wa ACT Wazalendo Taifa Msafiri Mtemelwa, akizungumza na viongozi wa chama hicho mkoani Shinyanga na kuwatoa hofu kuwa kuhama kwa viongozi wakubwa ndani ya chama hicho hakiwezi kufa na wala upinzani kufa, ndiyo wanazidi kuimalika zaidi na kuwataka viongozi hao waache kuishi ndani ya chama kwa mkumbo wa mtu fulani, bali waishi kwa miongozo na kanuni ya chama hicho.

Mwenyekiti wa kamati ya kampeni na uchaguzi wa chama cha ACT Wazalendo Taifa  Mohamed Babu, akizungumza na viongozi wa chama hicho mkoani Shinyanga na kuwataka kutoa pia kipaumbele kwa wanawake ndani ya chama hicho kushika nyazifa mbalimbali za uongozi.

Mwenyekiti wa kamati ya kampeni na uchaguzi wa chama cha ACT Wazalendo Taifa  Mohamed Babu, akizungumza na viongozi wa chama hicho mkoani Shinyanga na kuwataka mwezi Agost wafanye uchaguzi wa ngazi zote na kuchagua viongozi wenye sifa pamoja na kutoa nasafi za viti maalumu kwa wanachama wanaokipigania chama, na siyo kuweka watu wengine wa kuja.

Mjumbe wa kamati kuu taifa wa chama cha ACT Wazalendo Nyangaki Shilungushela, akizungumza kwenye kikao cha  viongozi wa chama hicho mkoani shinyanga, na kuwataka kujituma kufanya kazi za chama na kujiamini, na kubainisha chama chenye upinzani wa kweli kimebaki ACT, ambapo vyama vingine vimeshindwa kazi ya mapinduzi na kubaki kufanya siasa za maji taka.
Baadhi ya viongozi wa chama cha ACT Wazalendo mkoani Shinyanga wakisikiliza Nasaha kutoka kwa viongozi wao wa kitaifa, kuwa wakijenge chama na kutokubali kununuliwa ili kuuwa upinzani, ikiwa upinzani hauwezi kufa ambapo kuhama kwa viongozi ndani ya vyama haukuanza kipindi hiki.

Baadhi ya viongozi wa chama cha ACT Wazalendo mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha viongozi wao wa kitaifa.

Na Marco Maduhu ambaye pia ni Mwandishi wa gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.

Powered by Blogger.