SERIKALI KULIPA FIDIA KINGA BIMA YA MAZAO


Ofisa mwandamizi wa shirika la Bima ya Taifa kutoka Makao Makuu jijini dare s salaamu Catherine Nangali kitengo cha Madai ya fidia ya Magari na Kilimo akitoa elimu kwa wakulima hao juu ya  umuhimu wa kujiunga na Bima hiyo ya Kinga ya mazao.


SOMA HABARI KAMILI

Serikali kupitia Shirika la Bima la Taifa linatarajia kuzindua Bima ya Kinga ya Mazao kutoka kwa mkulima yakiwa Shambani, ambapo pale atakapo kosa kuvuna mavuno ya uhakika tofauti na misimu mingine iliyopita, Shirika hilo litamlipa fidia mapungufu hayo na kuendelea kumyanyua kiuchumi.

Hayo yalibainishwa Feb 14 mwaka huu kwenye Kata ya Kagongwa wilayani Kahama na Ofisa mwandamizi wa Shirika hilo kutoka makao makuu jijini Dar es salaam kitengo cha Madai ya fidia za magari na kilimo Catherine Nangali, wakati akitoa elimu kwa wakulima wa Kata hiyo juu ya umuhimu wa kujiunga na bima hiyo ikiwamo na ya majanga ya moto.

Alisema baada ya Serikali kuona wakulima wa hali ya chini wanakabiliwa na changamoto nyingi kwenye kilimo, ndipo wakaona kuna umuhimu wa kuanzisha bima ya kinga ya mazao, ambapo mkulima pale mazao yake yatakapokuwa shambani na kushambuliwa na wadudu, ukame, mbegu kutoota,kuzidiwa na mvua, atalazimika kulipwa hasara hiyo.

“Bima hii ya kinga ya mazao tutaizindua june mwaka huu, ambayo itamsaidia mkulima kufidiwa hasara zake pale anapozipata kwenye kilimo chake kwa kukosa mavuno ya uhakika, ambapo pia tunatarajia kuanza kutoa mikopo kwa wakulima, ili kuwawezesha kulima mashamba makubwa na kuinuka kiuchumi,”alisema.

Aliongeza kuwa kinachopaswa kwa mkulima atakaye jiunga na bima hiyo, ni kutunza kumbukumbu zake za mavuno kila msimu wa kilimo, ambapo siku mazao yake yakiandamwa na matatizo aweze kufanyiwa Tathimini na hatimaye kulipwa fidia ya hasara aliyoipata, na kumuokoa kutumbukia kwenye janga la umaskini.

Naye Ofisa wa shirika hilo la bima ya taifa kutoka makao makuu Prosper Peter kitengo hicho hicho cha bima za magari na kilimo, alitoa tahadhari kwa wakulima watakaojiunga na bima hiyo, kutotengeneza matukio ya kutofauta Sheria na Kanuni za kilimo iliwapate kulipwa fidia ambapo ikibainika hawatolipwa.

Nao baadhi ya wakulima waliohudhulia elimu hiyo Skolastika Laurent, aliipongeza Serikali kwa kuthamini wakulima wadogo kutaka kuwainua kiuchumi, na kubainisha kuwa bima hiyo itakuwa msaada mkubwa kwao, ikiwa kuna baadhi ya misimu ya kilimo imekuwa ikiwatia hasara kwa kukosa mavuno sababu ya mabadiliko ya tabia nchi.


SOMA HABARI PICHA HAPA CHINI


, Ofisa mwandamizi wa shirika la Bima ya Taifa kutoka Makao Makuu jijini dare s salaamu Catherine Nangali kitengo cha Madai ya fidia ya Magari, akiwaeleza wakulima hao ambao watajiunga na Bima hiyo ya Kinga ya Mazao kuwa watapatiwa mafunzo na wataalamu wa kilimo kutoka wizarani ambao wataambatana nao namna ya kulima kilimo cha kisasa na chenye tija ambacho kitawasaidia kupata mavuno mengi pamoja na kusambaziwa pembejeo za kilimo ambazo ni bora zaidi na hazitakuwa na changamoto kwenye kilimo chao, ikiwamo Mbegu na madawa ya kuulia wadudu.

Ofisa wa shirika la Bima la taifa kutoka makao makuu jijini Dar es salaamu Prosper Peter kitengo cha Magari na Kilimo akitoa Tahadhari kwa wakulima watakaojiunga na bima hiyo, kutotengeneza matukio ya kutofuata Sheria na Kanuni za kilimo iliwapate kulipwa fidia ambapo ikibainika hawatolipwa
Ofisa wa Bima ya Taifa kutoka mkoani Shinyanga  Stella Paulo kitengo cha Bima za Mali na Ajali, akitoa elimu kwa wakulima hao juu ya umuhimu wa kujiunga na Bima za majanga ya moto, na kutoa  mfano kunaweza kutokea nyumba zao kupata ajali za moto ama makazi yao au sehemu zao za biashara kuteketea ambapo wataweza kufidiwa kwa kujengewa nyumba mpya na kuwarudisha katika hali zao kama zamani.

Kaimu meneja wa Shirika la Bima ya Taifa Mkoani Shinya nga Fred Magesa akitoa historia ya Bima la Taifa lilivyo anza, kuwa  Shirika hilo mwaka 1963 ndipo lilipoanza kwa muungano wa Tanganyika na makampuni ya kigeni na kuitwa shirika la bima la Tanganyika, lakini mwaka 1965 baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar likawa Shirika la Bima laTanzania, na mwaka 1967 baada ya azimio la Arusha Serikali ilitaifisha hisa zote  na shirika hilo kumiliki hisa hizo kwa asilimia 100 na  kubaki kuwa mali ya serikali, na hivyo  kuwataka watanzania walitumia shirika hilo kwa kuwa wazalendo kwa kupenda vitu vya nyumbani na siyo kwenda kukata bima kwenye mashirika binafsi ilikuweza kuchangia pato la taifa ambalo litasaidia kutatua matatizo ndani ya jamii, ikiwamo miundombinu ya barabara ,huduma za Afya ,elimu Nk.

Mkulima Skolastika Laurent akiipongeza Serikali kwa kuthamini wakulima wadogo kutaka kuwainua kiuchumi, na kubainisha kuwa bima hiyo itakuwa msaada mkubwa kwao, ikiwa kuna baadhi ya misimu ya kilimo imekuwa ikiwatia hasara kwa kukosa mavuno sababu ya mabadiliko ya tabia nchi.

Mkulima wa Kata ya Kagongwa wilayani Kahama Merry Bukwimba akiuliza swali kwenye semina hiyo ya Elimu ya Bima, namna watakavyokuwa wakifaidika na Pembe Jeo ya Mbegu za kilimo ambapo kumekuwa na tatizo hilo kwa wakulima kuuziwa mbegu zisizo na ubora na kusababisha kutoota na kuwatia hasara, na kupewa majibu kuwa wale wakulima wataojiunga  na Bima hiyo ya Kinga ya Mazao watakuwa wakisambaziwa mbegu na mawakala kutoka Bima ya Taifa ambao watakuwa wakifanya nao kazi.

Mwenyekiti wa kikundi cha TAMAKIWAKA  Rachel Malisa ambao wanajihusisha na kilimo cha  Mpunga, Mahindi, Viazi vitamu, Alzet na ufugaji kuku, akiipongeza Serikali kwa kuwapatia elimu hiyo ya bima dhidi ya Kinga ya mazao na kuahidi kujiunga iliwapate kuwa salama pale wanapokuwa wakitegemea kilimo kuwainua kiuchumi.


baadhi ya Wakulima kutoka Kagongwa wilayani Kahama wakisikiliza  Elimu ya Bima ya Kinga ya Mazao kutoka Shirika la Bima la Taifa


Wakulima wakifuatilia kwa makini umuhimu wa kujiunga na Bima ya Kinga ya Mazao

Mwenyekiti wa Kijiji cha Iponya Kata ya Kagongwa wilayani Kahama Joint Wiliamu akifungua semina hiyo ya elimu ya Bima ya Taifa kwa wakulima wa Kagongwa, na kuwataka wakulima hao wajiunge na Bima hiyo ya Kinga ya Mazao, ilikuwa kuwa komboa na janga la umaskini pale mazao yatakapogoma kutoa mavuno ya uhakika na kuwasisitiza elimu hiyo waliyoipata wakawe mabarozi wazuri kwa wenzao ambao hawajafika kupewa elimu hiyo.

Na Marco Maduhu

























Powered by Blogger.