KANGE LUGOLA AKIFUNGA KIWANDA CHA PUNDA SHINYANGA



Naibu waziri wanchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kange Lugola, amekifunga kiwanda cha kuchinja Punda cha Fang Hua kilichopo mjini Shinyanga, kutokana na kukithiri kwa uchafuzi wa mazingira na kuhatarisha afya za wananchi.

Lugola amekifunga kiwanda hicho jana June 6,2018 alipofanya ziara ya ukaguzi wa mazingira kwenye kiwanda hicho, baada ya kusikia malalamiko ya wananchi wa mjini humo kuwa kimekuwa kikichafua mazingira sababu ya kutapakaza hovyo mabaki ya wanyama hao, mara wanapomaliza kuwa chinja, ikiwamo mifupa na utumbo wa punda hao.

Alisema kutokana na kujionea mwenyewe uchafuzi huo wa mazingira, ameamua kukifunga kwa muda hadi pale watakapo tekeleza maagizo ya Serikali ya kuweka mifumo mizuri ya kuzuia uchafuzi huo wa mazingira, ndipo watakapo ruhusiwa tena kuendelea na shughuli hizo za uchinjanji Punda.

“Serikali ya awamu ya tano tunapenda sana wawekezaji na tunawahitaji lakini sio kukeuka sheria za nchi na kutaka kutuumizia wananchi wetu kwa kuharibu afya zao na kutuingiza kwenye gharama zingine za kununua madawa, fedha ambazo zinge kwenda kutekeleza miradi mingine,”alisema Lugola.

“Kuanzia sasa kiwanda hiki nasitisha shughuli zake za uchinjaji punda hadi pale Serikali kupitia baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) itakapo jiridhisha na ufuatwaji wa sheria za mazingira ndipo tutakapo ruhusu tena muendelee na uchinjanji punda ,”aliongeza.

Pia aliwataka viongozi wa kiwanda hicho cha Punda kuacha tabia ya kuwa wakaidi, ambapo wamekuwa wakipewa maagizo na Serikali juu ya kufanya maboresho pamoja na kupigwa faini, lakini wamekuwa wagumu kutekeleza pamoja na kutolipa faini hizo, huku wakiendelea na shughuli zao za uchinjaji Punda.

Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, alitoa wiki moja katika machinjio ya Ng’ombe yaliyopo Nguzo Nane mjini humo, yafanyiwe marekebisho ya uzibuaji wa mitaro ambayo imezibwa na uchafu, pamoja na kuondoa mlundikano wa mavi ya mifugo hao ndani ya machinjio hiyo, na kwenda kumwaga kwenye mashamba.

Kwa upande wake msimamizi wa kiwanda hicho Dk Isaya Gabriel alikiri kuwepo na makosa hayo ya ukweukwaji wa Sheria za utunzanji wa mazingira, na kuahidi suala hilo kulifanyia kazi, pamoja na kufukua mizoga ya punda ambao walikuwa wamefukiwa kwenye mashimo ya kina kifupi na kutoa funza pamoja na harufu kali.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kange Lugola mwenye Track Suti ya Blue akiamulu lifukuliwe Shimo ambalo lilikuwa limedaiwa kutofukia kitu na kubainika kulikuwa na mabaki ya mifupa ya Punda ambayo ilikuwa ikitoa harufu pamoja na funza kuwapo kwa juu.

Mifupa ambayo ilikuwa ikizagaa katika maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho ambapo Kisheria ni Kosa kwani ilitakiwa kuchomwa moto.

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kange Lugola mkono wa kulia akiwa na daktari msimamizi wa kiwanda hicho cha Punda dk Isaya Gabriel wakiangalia wanyama hao Punda ambao huchinjwa na kusafirishwa kwenda nchini Kenya.

Mifupa ya wanyama hao Punda ikiwa imezagaa hovyo ndani ya kiwanda kicho.

Ndege wakitafuta vyakula vya mizoga kwenye kiwanda hicho cha Punda.

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kange Lugola, mwenye Track suti ya blue akiendelea na ziara ya kukagua mazingira.

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kange Lugola, mwenye Track suti ya blue akiendelea na ziara ya kukagua mazingira.

Ndege wakiwa wanasubiri kula mizoga kwenye kiwanda hicho cha Punda.

Uchafu ukiwa ndani ya mfumo wa maji kwenye kiwanda hicho cha Punda.

Mifupa ikionekana kuendelea kuzagaa hovyo.

Ndege wakisubili kula mizoga ya punda.

Utumbo wa Punda ukionekana kuzagaa ndani ya kiwanda hicho.

Wanyama Punda wakiwa ndani ya kiwanda tayari kwa kusubiliwa kuchinjwa ambapo kwa wastani kwa siku moja wanatakiwa kuchinjwa Punda 20 lakini hua wanazidishwa hadi kufikia Punda 75.

Ufukuaji wa mizoga ya Punda ukiendelea.


Ziara ikiendelea kwenye kiwanda cha Punda.

Naibu waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kange Lugola mkono wa Kushoto akiwa na Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, kwenye kiwanda hicho cha Punda FANG HUA Mjini Shinyanga,

Msimamizi wa kiwanda hicho cha Punda Dk Isaya Gabriel akitoa maalezo ya kwanini kiwanda hicho hakifuati sheria za kutunza mazingira.

Wanyama Punda wakiwa kwenye Zizi ndani ya kiwanda hicho cha FANG HUA Kilichopo Ibadakuli mjini Shinyanga.

Msimamizi wa kiwanda hicho cha Punda Dk Isaya Gabriel akitoa maelekezo namna Punda hao wanavyopelekwa kuchinjwa.

Msimamizi wa kiwanda hicho cha Punda Isaya Gabriel akikiri makosa ya kiwanda hicho kukeuka sheria za utunzaji wa mazingira.

Kaimu ofisa mazingira wa manispaa ya Shinyanga Ezra Majerenga akielezea namna kiwanda hicho kinavyo keuka Sheria hizo za utunzaji wa mazingira licha kukipiga faini na kutoa maelekezo ya kufanya ,bali wamekuwa wakaidi na kutotii maagizo ya Serikali na kuendelea kuchafua mazingira.

Ofisa mifugo wa manispaa ya Shinyanga Velan Mwaluko akizungumza kuwa kiwanda hicho kinafanya makosa makubwa juu ya utunzaji wa mazingira ambapo na yeye ni mmoja wa wakaguzi lakini chaa ajabu amekuwa akizuiwa kuuingia humo.

Ofisa mifugo wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Velan Mwaluko akiendelea kutoa maelezo kuwa hata mifumo yao ya kuchakata maji kwenye kiwanda hicho siyo sahihi.

Mifupa ya Punda ikiwa imezagaa hadi kwenye Mitaro ya kutililishia maji.

Ukaguzi wa mazingira ukiendelea.

Punda wakiwa ndani ya kiwanda hicho.

Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho wakiwa wamevaa sare mpya mara baada ya Ziara hiyo ilikuficha mapungufu ,ambapo ilidaiwa wamekuwa wakifanya kazi bila ya kuvaa vifaa vya usalama.

Wafanyakazi wa kiwanda hicho cha Punda wakiwa kwenye nguo mpya.

Mkuu wa Idara ya mifugo manispaa ya Shinyanga Laurent Kyalugaba mkono wa kushoto akimuonyesha Naibu waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kange Lugola namna inavyofanya kazi ikiwa kwa wastani inatakiwa kuchinja Ng'ombe 10, lakini zinachinjwa hadi 40.

Ng'ombe wakiwa kwenye zizi katika machinjio hayo ya Nguzo Nane wakisubili kuchinjwa tayari wa kitoweo.

Mfereji wa machinjio ukiwa mchafu.

Mamalishe Sofia Sungura akielezea namna mavi hayo ya Ng'ombe yanavyo toa harufu na kuharibu biashara zao.

Naibu waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kange Lugola akitoa maelekezo kwa uongozi wa manispaa ya Shinyanga kuwa Mitaro yote kwenye machinjio hayo ifukuliwe.

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kange Lugola awali wakiwasili mkoani Shinyanga akizungumza na viongozi wa mkoa huo aliwataka kusimamie Sheria za utunzaji wa mazingira kwa vitendo.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kange Lugola akiendelea kutoa malekezo kwa uongozi wa mkoa huo na kupiga Marufuku matumizi ya mikaa na kuni kwenye Taasisi za Serikali na Umma zikiwamo Vyuo, Magereza, na Jeshi.

Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akiahidi kusimamie utekeelzaji wa maagizo hayo.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua matamko ya Serikali kutoka kwa Naibu waziri ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazigira Kange Lugola mara baada ya kuhitimisha ziara yake na kubaini mji wa Shinyanga siyo msafi kimazingira.

Na Marco Maduhu ,mbaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.
Powered by Blogger.