MADIWANI WALIA NA UCHAFU WA MACHINJIO YA NGUZO NANE



Baraza la madiwani la halmashauri ya manispaa ya Shinyanga limetupia lawama uongozi wa manispaa hiyo kwa kushindwa kutekeleza azimio lao la ukarabati wa machinjio ya Nguzo Nane, ambalo  ni chafu na lina hatarisha afya za wananchi.


Madiwani wamezungumza hayo leo April 24, 2018 kwenye kikao cha baraza hilo cha Kawaida, wakati wa kujadili taarifa ya mkurungenzi na yatokanayo kwenye kikao kilicho pita , kuwa Azimio lao bado halijatekelezwa kwa usahihi la ukarabati wa machinjio hiyo.

Mmoja wa madiwani hao Shela Mshandete wa Vitimaalumu alisimama kuuliza hatima ya machinjio hayo ambapo ukarabati wake haukufanyika ipasavyo kama iliyo azimiwa, ambalo bado ni chafu na halifai kuchinjiwa mifugo ikiwa lina hatarisha afya za wananchi.

Naye Diwani wa Kata ya Kambarage Hassani Mwendapole, amesema anasikitshwa na uongozi wa halmashauri hiyo kwa kushindwa kutekeleza maazimio ya madiwani hao kwa wakati uliopangwa , ambapo chinjio hilo lina hali mbaya, na kuhofia siku mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) ikitembelea Sehemu hiyo lazima walifunge.

Aidha Ofisa mifugo wa Halmashauri hiyo Laurent Kangamba amesema pesa zilizotolewa kukarabati chinjio hilo zilikuwa kidogo Shilingi Milioni Nane, na hivyo kushindwa kufanyiwa matengezo makubwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Geofley Mwangulumbi, amesema ukarabati wa chinjio hilo utafanyiwa matengenezo mkubwa na kuwa la kudumu, sababu ujenzi wa Chinjio la Kisasa ambalo linajengwa Kata ya Ndembezi kukamilika kwake litachukua muda mrefu.

Hata hivyo kwa upande wake Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya, aliomba madiwani hao kutoa muda wa Chinjio hilo likarabatiwe, na kutoa ndani ya mwezi mmoja, huku akisema hoja hiyo isiwepo tena kwenye vikao vingine, bali azimio hilo litekelezwe haraka ili kunusuru afya za wananchi.



Diwani wa Viti maalumu Shela Mshandete akiuliza swali kwenye baraza hilo la halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, juu ya uchafu uliopo katika machinjio ya mifugo nguzo Nane ambayo ina hatarisha afya za wananchi.

Diwani wa Kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga Hassani Mwendapole ,naye akichangia mada hiyo ya uchafu wa mchinjio ya nguzo Nane, na kufikia hatua ya kuomba pendekezo la kuwepo na kamati ya madiwani ya kuwa wanafuatilia utekelezaji wa maazimio yao, hoja ambayo ilipingwa.

Diwani wa Kata ya Ndembezi Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga David Nkulila naye akichangia mada ya uchafu wa machinjio hayo, na kuonyesha masikitiko ya kutojengwa haraka machinjio ya kisasa ambayo ndiyo Suluhisho ya kulinda afya za wananchi, kwa kuepuka kupatwa na magonjwa ya mlipuko kutoka katika machinjio hiyo ya Nguzo Nane.

Diwani wa Viti maalumu Mariamu Nyangaka naye akichangia hoja ya machinjio hayo, na kuonyesha kusikitishwa na uongozi wa halmashauri hiyo ya manispaa ya Shinyanga kwa kushindwa kutekeleza maazimio yao kwa wakati.

Ofisa mifugo wa Halmashauri hiyo ya manispaa ya Shinyanga Laurent Kangamba amesema pesa zilizotolewa kukarabati chinjio hilo zilikuwa kidogo Shilingi Milioni Nane, na hivyo kushindwa kufanyiwa matengezo makubwa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Geofley Mwangulumbi amesema ukarabati wa chinjio hilo utafanyiwa matengenezo mkubwa na kuwa la kudumu, sababu ujenzi wa Chinjio la Kisasa ambalo linajengwa Kata ya Ndembezi kukamilika kwake kutachukua muda mrefu.

Naibu Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Agness Machiya naye alionyesha kusikitishwa na uongozi wa Halmashauri hiyo kwa kushindwa kulikalabati Chinjio hilo kwa kiwango cha kuridhisha , na hivyo kuwaomba madiwani watoe Muda chinjio hilo lifanyiwe matengenezo na kutolea ndani ya Mwezi Mmoja liwe Tayari.

Madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye baraza lao la Kawaida wakijadili ajenda mbalimbali kwa lengo la maendeleo ya manispaa hiyo.

Madiwani wakiendelea na kikao.

Kikao kikiendelea.

Wataalamu wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakipitia nyaraka za Ajenda mbalimbali kwenye Baraza hilo ,ambapo wakwanza mkono wa kulia ni Ofisa Utumishi Magedi Magezi.

Diwani wa Kata ya Kambarage Hassani Mwendapole akisikiliza kwa makini uwasilishwaji wa Ajenda kwenye Baraza la Madiwani.

Watendaji wa Kata nao wakiwa kwenye Baraza hilo la Madiwani.

Diwani wa Kata ya Ndala manispaa ya Shinyanga Wiliamu Shayo naye akichangia hoja kwenye Baraza hilo na kuwasilisha kilio chake cha Ubovu wa miundombinu ya Barabara .

Wataalamu na viongozi wa Serikali za Mitaa wakiwamo wenyeviti wa Mitaa nao wakiwa kwenye Baraza hilo.

Wataalamu wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakisikiliza kwa makini Ajenda za Kwenye baraza hilo.

Wataalamu wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakisikiliza kwa makini Ajenda za Kwenye baraza hilo.







Powered by Blogger.