RC SHINYANGA APIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA MANGE KIMAMBI







Serikali mkoani Shinyanga imepiga marufuku watu ambao wanaotaka kuandamana sikukuu ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, ambayo yana ratibiwa na mwana Dada Mange Kimambi kupitia mitandao ya kijamii, kuwa watakaofanya hivyo waage kabisa familia zao ikiwa watashughulikiwa .


Hayo yalibainishwa jana na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack, kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Saratani ya mlango wa kizazi mkoani hapa, kuwa siku hiyo wananchi wote wa mkoa huo wanatakiwa wajipange kwa ajili ya shughuli za kufanya usafi mjini mzima, na siyo kufanya maandamano yasiyo na Tija.

Alisema anasikitishwa na kitendo cha mwana Dada huyo Mange Kimambi ambaye anaishi nchini marekani , kuhamasisha wananchi wafanye maandamano ya kuvuruga Amani ya nchi, na kutoa onyo kwa wakazi wa mkoa huo kuwa watakaoandamana wajipange kwa kushughulikiwa na kufungwa jela.

“Wale ambao mnataka kuandamana naomba kabisa muage na familia zenu ikiwa mimi kama mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa, sitakubali upuuzi huo uendelee kwenye mkoa wangu, ambapo nitawashughulikia wote watu ambao wanataka kuvunja amani ya nchi yetu,” alisema Telack.

“Bila nchi yetu kuwa na amani watu wote tusinge kuwepo mahari hapa ,tusinge fanya hata shughuli za kilimo, hivyo tukimaliza kufanya shughuli za usafi siku hiyo twendeni mashambani tukavune mazao yetu, na wanaofanya biashara waende kwenye biashara zao, na siyo kufanya maandamano hayo ambayo yatagharimu maisha yenu,”aliongeza.

Pia alitoa wito wa wasichana walio na umri wa miaka 14 kwenda kupewa chanjo hiyo ya Saratani ya mlango wa kizazi, ambayo itakuwa kinga dhidi ya ugonjwa huo, na kuwafanya wabaki kuwa salama ikiwa saratani hiyo ni kinara kwa muaji ya wanawake hapa nchini.

Kwa upande wake mganga wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dk Rashid Mfaume, alisema kuwa mkoa huo unatarajia kutoa Chanjo hiyo kwa wasichana 29,479 walioko majumbani na ma mashuleni, ambapo huduma hiyo itatolewa bure kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akisoma hotuba na kuwataka wasichana wenye umri wa miaka 14 wajitokeze kupatiwa kinga ya ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa kizazi ,pamoja na akina mama wajitokeze kwa wingi kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa hayo ya saratani ikiwamo na yama Titi, huku akipiga marufuku maandamano ya mwana Dada Mange Kimambi sikukuu ya Muungano.

Mganga wa mkoa wa Shinyanga Dr Rashid Mfaume akizungumza kwenye uzinduzi huo alisema jumla ya wasichana 29,479 wanaratajiwa kupewa chanjo hiyo ya kinga ya Saratani ya mlango wa kizazi.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa Nasaha kwa viongozi wa serikali kuanzia ngazi za Kata, madiwani na viongozi wa kidini kutoa elimu wa wananchi juu ya chanjo hiyo ya saratani ya mlango wa kizazi ili kusiwepo na upotoshwaji.

Mwakilishi kutoka Shirika la afya Duniani (WHO) DR Gerald Maro akizungumza kwenywe uzinduzi huo na kuupongeza mkoa wa Shinyanga kwa kuzindua chanjo hiyo mapema.

Mwakilishi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI DR Deogratius Maufi akizungumza kwenye uzinduzi huo naye alipongeza mkoa wa Shinyanga kwa kuzindua kampeni hiyo mapema.

Muunguzi wa huduma ya afya kutoka Zahanati ya kanisa la KKKT Mjini Shinyanga Modesta Jitanga akimuonyesha mkuu wa mkoa namna wanavyoweka dawa hiyo ya chanzo ya saratani ya kinga mlango wa kizazi, mkono wa kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.

Muunguzi wa afya kutoka Zahanati ya Kanisa la KKKT mjini Shinyanga Modesta Jitanga akimpatia chanjo ya Saratani ya kinga ya mlango wa kizazi mwanafunzi Jesca Kashinje(14) kutoka shule ya Sekondary Mwasele.
Wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye uzinduzi huo wa Chanjo ya Saratani ya Mlango wa kizazi.
Wanafunzi wa Shule mbalimbali za Sekondari manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye uzinduzi wa chanjo hiyo ya Saratani ya Mlango wa kizazi.
Wadau wa afya na wazazi wakiwa kwenye uzinduzi wa Chanjo hiyo ya Saratani ya mlango wa kizazi.

Kikundi cha ngoma kikitoa burudani kwenye uzinduzi huo wa Chanjo ya Saratani ya Mlango wa kizazi.

Kwaya ya AICT Shinyanga nao wakitoa burudani kwenye uzinduzi huo wa Chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi.


Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.











Powered by Blogger.