VETA SHINYANGA YAZINDUA MAFUNZO MAPYA YA UPATIKANAJI WA AJIRA MIGODINI,TANROAD
Barozi wa Canada nchini Tanzania Nathalie Garon Mkono wa kushoto akikata utepe wa kuzindua mafunzo mapya ya utengenezaji
wa mitambo mikubwa (Heavy duty Equipment Mechanics Work Shop) katika chuo cha Veta mkoani Shinyanga akiwa na
mkurugenzi wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi Stadi kutoka wizara ya ya
elimu sayansi na tecknolojia Mhandisi Thomas Katebalirwe mkono wa kulia.
SOMA HABARI KAMILI
Chuo cha ufunzi
stadi Veta mkoani Shinyanga, kimezindua mafunzo mapya ya utengenezaji wa
mitambo mikubwa (heavy duty equipment mechanics work shop) ambayo
yatasaidia vijana wengi kupata ajira kwa urahisi ndani ya Migodi na Tanroad
sababu mafundi wa mitambo hiyo wapo wachache hapa nchini.
Zoezi la
uzinduzi wa mafunzo hayo mapya (Course mpya) limefanyika februari 19 mwaka huu
chuoni hapo, ambapo vifaa vya mafunzo ya utengenezaji wa mitambo hiyo yakiwa
yamefadhiliwa na Serikali ya Canada, kwa mlengo wa Serikali ya Tanzania
kuongeza idadi kubwa ya wataalamu wake ndani ya nchi, kwa kupata mafundi wa
mitambo hiyo pamoja na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa Course hiyo mpya mkuu wa chuo cha Veta mkoani Shinyanga
Afridon Mkhomoi, alisema baada ya kuona mkoa wa Shinyanga umezungukwa na migodi
mingi, na wanapokuwa wakipeleka vijana wao kufanya kazi kwa vitendo kwenye
migodi hiyo, wamekuwa wakipokea chagamoto ya kwanini wasiwe na course ya
utengenezaji wa mitambo chuoni hapo ambayo itawasaidia vijana wengi kupata
ajira kwa urahisi ,na hivyo kuamua kuanza mchakato wa kuianzisha na hatimaye
wamekamilisha.
Alisema baada ya
kupokea changamoto hiyo, ndipo wakapata ufadhili wa vyuo vya Veta kutoka nchini
Canada kwa kupewa vifaa hivyo vya mafunzo ya utengenezaji wa mitambo mikubwa, na
mpaka sasa wamesha dahili wanafunzi 20 ,wakike wakiwa Wanne na wakiume 16,na usomaji wake utachukua Miaka
Mitatu, na kubainisha Mwanafunzi kama akifikisha miaka miwili pia anaweza
kwenda kufanya kazi, huku akimalizia mwaka wake wa mwisho polepole.
“Natoa wito kwa
vijana mkoani Shinyanga kuichangamkia Course hii mpya ambayo itawapatia ajira
kwa urahisi ndani ya migodi kwa kutengeneza mitambo ambayo itakuwa ikiharibika
sababu wataalamu wake ni wachache,” alisema.
Naye Kaimu
mkurugenzi wa masoko mipango na maendeleo kutoka Veta makao makuu Hildegardis
Bitegera, akimwakilisha kaimu
mkurugenzi wa Veta kutoka makao makuu Dk Ndazi Bwile, aliwataka vijana
wanaosoma mafunzo hayo wawe na bidii ya kusoma ikiwa fani hiyo inafaida kwenye
soko la Ajira .
Kwa upande wake
mkurugenzi wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi Stadi kutoka wizara ya ya
elimu sayansi na tecknolojia Mhandisi Thomas Katebalirwe, alisema wao kama
wizara walipitisha mafunzo hayo tangu mwaka 2015, na matarajio ya Serikali
katika Course hiyo mpya ni kupata watalamu wengi hapa nchini wa Mitambo hiyo.
Aidha Meneja wa
mradi wa vifaa vya kutengenezea mitambo
hiyo kutoka nchini Canada katika chuo cha College of New Colidonia (CNC)Romana Pasca,
alisema wameamua kufadhili vifaa hivyo ili tanzania ipate kuongeza idadi kubwa ya wataalamu wake ndani
ya nchi wa kutengeneza mitambo, pamoja na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
Nao baadhi ya
wanafunzi wanaosoma mafunzo hayo mapya akiwamo Calvin Msafiri, waliipongeza
Serikali kwa kushirikiana na nchi ya Canada kuanzisha Course hiyo mpya ambayo
itawapatia ajira kwa urahisi na kuinua uchumi wa maisha yao.
SOMA PIA HABARI PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa chuo cha Veta mkoani Shinyanga Afridoni Mkhomoi akisoma taarifa ya chuo hicho juu ya mafunzo hayo mapya ya utengenezaji wa mitambo mikubwa, na kuishukuru Serikali ya Canada na chuo cha College of New Colidonia (CNC) kwa ufadhili walioutoa wa vifaa hivyo vya kujifunzia kutengenezea mitambo hiyo ambayo itatoa fursa kubwa ya vijana kupata ajira hasa migodini na Tanroad.
Kaimu
mkurugenzi wa masoko mipango na maendeleo kutoka Veta makao makuu Hildegardis
Bitegera, akimwakilisha kaimu
mkurugenzi wa Veta kutoka makao makuu Dk Ndazi Bwile, akiwataka vijana
wanaosoma mafunzo hayo ya utengenezaji wa mitambo mikubwa, wawe na bidii ya kusoma ikiwa fani hiyo inafaida kwenye
soko la Ajira .
mkurugenzi wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi Stadi kutoka wizara ya ya
elimu sayansi na tecknolojia Mhandisi Thomas Katebalirwe, akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo mapya, na kusema kuwa serikali inatarajia matokeo makubwa ya kupata wataalamu wake wengi wa ndani ya nchi wa kutengeneza mitambo hiyo mikubwa.
Meneja wa
mradi wa vifaa vya kutengenezea mitambo
hiyo kutoka nchini Canada katika chuo cha College of New Colidonia Romana Pasca,
akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo mapya na kusema wameamua kufadhili vifaa hivyo ili tanzania ipate kuongeza idadi kubwa ya wataalamu wake ndani
ya nchi wa kutengeneza mitambo mikubwa pamoja na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
mjumbe
wa bodi wa chuo hicho cha Veta mkoani Shinyanga Elias Kasitila, ambaye pia ni meneja wa Acacia wa kampuni ya uchimbaji
madini ya dhahabu Buzwagi, akiwataka vijana wanaosoma chuoni hapo kujenga tabia ya kujiajiri wenyewe na wasiwe na dhana ya kuwa wote wata ajiriwa ikiwa pale watakapohitimu mafunzo yao, ambapo tayari wanakuwa na ujuzi ambao wata utumia kuwa ingizia kipato pamoja na kuweza kuunda vikundi vya ujasiriamali, na kupata mikopo ambayo itawasaidia kuanzisha hata viwanda vyao na kuwaingizia kipato kizuri na kuendesha maisha yao bila shida.
Baadhi ya vifaa ambavyo vijana watakuwa wakijifunzia kutengeneza mitambo mikubwa katika mafunzo hayo mapya ya heavy duty equipment mechanics work shop.
Wageni waalikwa na wakufunzi wa chuo hicho wakiangalia vifaa vya kujifunzia namna ya kutengeneza mitambo mikubwa, ambavyo vimefadhiliwa na Serikali ya Canada kupitia chuo cha College of New Colidonia (CNC).
Baadhi ya mitambo ambayo wanafunzi wa chuo hicho cha Veta mkoani Shinyanga ambayo hujifunzia kutengeneza barabara.
Mwalimu wa Library Ezekiel Joachimu kutoa chuo cha Veta mkoani Shinyanga mkono wa kulia akimuonyesha vitabu vya mafunzo ambavyo husomea wanachuo wa Veta Dkt Alan Copeland ambaye ni mshauri mkuu wa taasisi ya Cican ya Canada inayotekeleza mradi wa Istep.
Mshauri mkuu wa taasisi ya Cican ya Canada inayotekeleza mradi wa Istep Dkt Alan Copeland, akiwa na mwalimu wa Library kutoka chuo cha Veta mkoani Shinyanga Ezekiel Joachimu ,wakiwa katika Library ya vitabu chuoni hap0.
Mwalimu wa mafunzo ya ukataji wa madini ya Vito na ung'alishaji Yona Mwambopa, akielezea namna wanafunzi chuoni hapo wanavyojifunza mafunzo hayo ambayo pia yatawapatia ajira migodini kwa urahisi.
Baadhi ya Vifaa ambavyo hujifunzia wanafunzi wa chuo cha ufundi Veta mkoani Shinyanga, namna ya kukata na kug'arisha madini hayo ya Vito.
Baadhi ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo mapya ya kutengeneza mitambo mikubwa katika chuo cha Veta mkoani Shinyanga ,wakiangalia namna madini hayo ya vito jinsi yalivyokatwa kitaalamu pamoja na kung'arishwa.
Muonekano wa madini hayo ya Vito yakiwa tayari yameshakatwa na Kung'arishwa kama unavyo yaona ambayo baadhi yake ni Amethyst, Quart, Tourmaline, Agate a Citrinr.
Mwanachuo cha Veta mkoani Shinyanga akitoa burudani ya kuruka sarakasi kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa mafunzo mapya ya utengenezaji wa mitambo mikubwa Heavy Duty Equipmet Mechanics work Shop.
Mwanafunzi wa Veta, Mkapa Malijani anayesoma fani ya Computer and Secretary akielezea wageni waalikwa namna wanavyosoma fani hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Veta wanaosoma Fani ya Computer and Secretary chuoni hapo.
Mshauri mkuu wa taasisi ya Cican ya Canada inayotekeleza mradi wa Istep Dkt Alan Copelanda akiahidi kuendelea kushirikiana na chuo hicho cha Veta mkoani Shinyanga katika suala zima la kuboresha mafunzo ambayo yatawapatia ajira vijana.
Wanafunzi wa chuo cha Veta wakiendelea kutoa burudani.
wanafunzi wa chuo cha Veta wakisikiliza Nasaha mbalimbali kutoka kwa wageni waalikwa ikiwamo ya kujenga dhana ya kujiajiri wenyewe ikiwa ujuzi wanao wa kufanya kazi na kuwaingizia kipato
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Veta Shinyanga wakiwa wamevaa Tshit ya chuo cha College of New Colidonia (CNC) ambacho ndicho kimefadhili vifaa hivyo vya kujifunzia kutengeneza mitambo mikubwa.
Tunasikiliza Nasaha mbalimbali kutoka kwa wageni waalikwa
wanafunzi wa chuo cha Veta Shinyanga wakiwa makini kuyashika yale wanayoambiwa na wageni waalikwa namna ya kutumia ujuzi wao wanaoupata kuwaingizia kipato na kuendesha maisha yao bila hata ya kutegemea kuajiriwa.
wafadhili wa vifaa vya mafunzo ya kujifunzia utengenezaji wa mitambo mikubwa kutoka nchini Canada, wakiwa na wageni waalikwa pamoja na viongozi wa chuo cha Veta Shinyanga na makao makuu, pamoja na baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Marco Maduhu ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti kubwa hapa nchini la Nipashe soma kila siku Gazeti lako pendwa uhabalike.