DC MATIRO APIGA MARUFUKU MAKAMPUNI KUNUNUA ZAO LA PAMBA
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amepiga marufuku makampuni, watu binafsi kununua zao la pamba kwa wakulima, ikiwa atakaye bainika kwenda kinyume na maagizo hayo ya Serikali itamchukulia hatua kali za kisheria.
Amesema Serikali imeshatoa maagizo kuwa Pamba yote ya Mkulima itauzwa kupitia vyama vya ushirika (AMCOS), ambavyo vimeshaundwa na kufufuliwa vile vilivyokuwa vimeshakufa kwenye vijiji vyao, kwa lengo la kuondoa changamoto ya kumyonya mkulima na kumuinua kiuchumi.
Akizungumza leo Mei, 2018 wakati akitoa hamasa kwa wakulima wa Kata ya Iselamagazi Shinyanga vijijini kwenye mkutano wake wa hadhara juu ya umuhimu wa kujiunga kwenye vyama vya ushirika, kuwa marufuku uuzaji wala ununuzi wa zao la pamba Kiholela, na atakaye bainika kukeuka maagizo hayo atashughulikiwa.
“Waziri mkuu Kasimu Majaliwa alishapiga marufuku zao la Pamba kuuza ama kununua kiholela, bali liuzwe kupitia vyama vya ushirika, na sisi kama wasaidizi wa Serikali tunalitilia mkazo agizo hilo, na ndio maana tumeshaunda vyama vya ushirika kila kijiji pamoja na kuvifufua vile ambavyo vilikuwa vimeshakufa,” alisema Matiro.
“Kufuatia utekelezaji wa agizo hilo, hivyo marufuku Kampuni, mtu binafsi kununua Pamba kwa wakulima, na atakaye bainika kwenda kinyume na agizo hilo Serikali itamchukulia hatua kali za kisheria, tunataka mkulima wa zao la pamba ainuke kiuchumi pamoja na kurudisha heshima ya dhahabu nyeupe,”aliongeza.
Pia alitoa wito kwa wakulima kufungua akaunti kwenye taasisi za kifedha (Mabenki) ikiwa katika msimu wa mwaka huu hakuna mkulima ambaye atalipwa pesa mkononi, bali zitakuwa zikilipwa kupitia akaunti zao, kwa lengo la kulinda usalama wa maisha yao na kuondoa matumizi ambayo siyo ya lazima.
Naye Ofisa ushirika wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini Shija Mwika, alisema mpaka sasa kwenye halmashauri hiyo kuna vyama ushirika 45 huku vingine vikiendelea kuundwa, na kutoa msisitizo kwa wakulima kuendelea kujiunga, ikiwa watapata faida nyingi ikiwamo na kupata pembejeo kwa wakati.
Nao baadhi ya wakulima wa Pamba kwenye Kata hiyo Emmanuel Sospeter ambaye amelima zao hilo Hekali Mbili na Nusu, ameipongeza Serikali kwa kupiga marufuku hiyo ya ununuzi wa Pamba Kiholela, kitendo ambacho kilikuwa kikimyonya mkulima hasa kwenye upujwaji wa Kilo na kumkandamiza kiuchumi.
TAZAMA HABARI PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wananchi wa Kata ya Iselamagazi Shinyanga vijijini juu ya umuhimu wa kujiunga na Vyama vya Ushirika ambavyo ndiyo vitatumika kununua zao la Pamba na siyo makampuni wala watu binafsi kama ilivyozoeleka katika miaka ya nyuma, ilikuondoa changamoto zilizokuwa zikilikabili zao hilo, likiwamo na suala la wakulima kupunjwa Kilo na kuendelea kuwa maskini.
Ofia Ushirika wa halmashauri ya wialya ya Shinyanga vijijini Shija Mwika amesema mpaka sasa kwenye halmashauri hiyo kuna vyama vya ushirika 45, huku vingine vikiendelea kuundwa kwa lengo kuu la kumuinua mkulima kiuchumi, kama kauli mbiu ya vyama vya ushirika inavyosema "Ushirika pamoja tujenge uchumi".
Ofisa kilimo na mratibu wa zao la Pamba kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini Ibrahimu Bundo anasema katika halmashauri hiyo limelimwa zao la Pamba Hekali 9,447 huku matarajio yalikuwa ni kulimwa Hekali 15,000, lakini kutokana na changamoto ya hali ya hewa baadhi ya mashamba yalizama kwenye maji na hivyo mazao kuharibika.
Meneja wakala wa Vipimo mkoani Shinyanga Elias Nyanda akionyesha wakulima hao wa zao la pamba kuwa watakapo kwenda kuuza Pamba yao kwenye vyama hivyo ya Ushirika watumie mizani ambazo zimeshadhibitishwa na wakala hao ya Digitali, ambapo Mizani ya Kwanza ni NAGATA.
Meneja wakala wa vipimo mkoani Shinyanga Elias Nyanda akionyesha Mizani ya Pili ambayo imedhibitishwa na wakala hao, kuwa ni SALTER ambayo ndiyo inafaa kutumika kununu Pamba ya Mkulima kwenye vyama hivyo vya Ushirika.
Meneja wakala wa vipimo mkoani Shinyanga Elias Nyanda akionyesha Mizani ya Tatu ambayo imedhibitishwa na wakala hao, kuwa ni CARONI ambayo ndiyo inafaa kutumika kununu Pamba ya Mkulima kwenye vyama hivyo vya Ushirika.
Meneja Mauzo kutoka taasisi ya kifedha benki ya (NMB) Trifon Melkiory akizungumza kwenye mkutano huo na kueleza kuwa Akaunti ambayo itafunguliwa na wakulima hao ni Bure haina Gharama wala makato ya kila mwezi hakuna na hivyo kuwataka wakulima hao wachangamkie fursa hiyo ikiwa fedha ambazo watakuwa wakiuza pamba kwenye vyama vya Ushirika hawata lipwa Mkononi (CASH) Bali watalipwa kupitia akaunti.
Ofisa huduma mauzo na wateja kutoka Benki ya (CRDB) Abel Dai naye akisema kuwa akaunti ambazo watafungua wakulima hao ni Bure na hazina Gharama zozote wala makato ya kila mwezi.
Awali Candinda Misonge akikaimu nafasi ya mwenyekiti, ambapo akifungua mkutano huo wa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga juu ya kutoa Elimu ya wananchi kujiunga na vyama vya Ushirika.
Awali Ofisa Tawala wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Charles Maugila akitambulisha msafara ambao mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alioambatana nayo, wakiwamo na watalaamu juu ya kutoa elimu kwa wakulima kujiunga na vyama vya ushirika ambavyo ndiyo vitanunua Pamba yao.
Diwani wa Viti maalumu kutoka Kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini Chausiku Salum akizungumza kwenye mkutano huo na kuipongeza Serikali kwa kupiga marufuku hiyo ya kuuza ama kununua pamba Kiholela ili mkulima apate kuinuka kiuchumi na kuondoa tatizo la unyonyaji hasa kwenye wizi wa upunjwaji wa mizani na kutoa pia wito kwa wakulima kutolichafua zao hilo kwa kuweka maji wa mchanga ikiwa mkombozi ameshapatikana.
Wakulima wa zao la pamba katika Kata ya Iselamagazi Shinyanga vijijini wakisikiliza Nasaha za mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro juu ya umuhimu wa kujiunga na vyama hivyo vya ushirika pamoja na kufungua Akaunti Benk.
Joseph Siguli mkazi wa Kata ya Iselamagazi akiuliza swali kuwa mazao yoyote yanaweza kuuzwa kwenye vyama hivyo vya ushirika ukitoa zao la Pamba? ambapo alipewa Jibu kuwa mazao yoyote yanaruhusiwa kuuzwa kwenye vyama vya Ushirika.
Wananchi wa Kata ya Isemagazi wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro juu ya umuhimu wa kujiunga na vyama vya Ushirika, pamoja na kuhamashishwa pia Kujiunga na mfuko wa BIMA YA AFYA CHF iliyoboreshwa ili kuwapunguzia gharama za matibabu.
Katibu wa chama cha Ushirika kutoka katika kijiji cha Ichongo Kata hiyo ya Iselamagazi, amsema kuwa vyama hivyo ana amini vitakuwa mkombozi mkubwa kwa mkulima katika kumiunua kiuchumi.
Wananchi wa kata ya Isemagazi wakiendelea na mkutano.
Zaharani Abdala mwanachi wa Kata ya Iselamagazi akihoji juu ya viongozi wa zamani wa vyama vya Ushirika ambao walitafuna fedha kuwa wameshachukuliwa hatua gani? na kupewa majibu kuwa wote wanashughulikiwa ikiwa na baadhi yao wameshaanza kujisalimisha na kurudisha pesa hizo mmoja baada ya mwingine.
Emmanuel Sospeter mkulima na mkazi wa Kata hiyo ya Iselamagazi akiipongeza Serikali kwa kuzuia uuzwaji na ununuzi huo wa Pamba Kiholela ikiwa itawasaidia kuondokana na tatizo la Kupunjwa Kilo.
Marco Shigulushaboke akiiomba Serikali kutengeza Maghala ya kutunzia mazao ambayo yameshaharibika ilikuondoa usumbufu kwa vyama hivyo vya Ushirika kununua Pamba kwenye za kukodi pamoja na kuwaondolea changamoto wakulima ya kutembea umbari mrefu kwend kuuza Pamba hiyo.
Wananchi wa kata ya Iselamagazi wakiwa kwenye mkutano wa hamasa ya kujiunga na vyama vya ushirika.

Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.