WABUNGE 176 KUMNG'OA MADARAKANI WAZIRI MKUU


Leo June 1, 2018 na kusogezea stori kutoka Hispania ambapo Waziri Mkuu, Mariano Rajoy yuko katika hatari ya kuondolewa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani naye kufuatia sakata la rushwa katika Serikali yake.


Wabunge 176 wanatarajiwa kuunga mkono azimio hilo wakiwamo 5 kutoka chama tawala. Kiongozi wa Upinzani, Pedro Sanchez anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo.

Kashfa ya rushwa inayomuandama kiongozi huyo inahusisha utoaji wa mikataba ya tenda za Serikali. Mpaka sasa watu 29 waliohusika wamefungwa jela.

Tangu kuingia kwake madarakani mwaka 2011, Mariano Rajoy anasifiwa kwa kuimarisha uchumi ingawa tatizo la ajira na kukuwa kwa tofauti ya kipato kati ya walionacho na wasionacho.
Powered by Blogger.