MBUNGE WA CCM AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI
Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe amefiwa na Mama yake Mzazi, Zainab Abdi aliyekuwa anapatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam.
Bashe amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kutoa taarifa hiyo.
"Ndugu zangu nimeondokewa na mama yangu mpendwa.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un"
Naye, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amempa pole Mbunge huyo kwa kuandika “Inna lilah waina ilaih raajiun. Mola akupe subra ndugu yangu @HusseinBashe katika mtihani huu mkubwa wa kufiwa na mama yako mzazi.”
Zitto ameongeza kwa kuandika “Inna lilah waina ilaih raajiun. Mola akupe subra ndugu yangu Hussein Bashe katika mtihani huu mkubwa wa kufiwa na mama yako mzazi. Poleni sana Sheikh Mohammed, Ibrahim Mohamed Bashe, Abubakar, Kauthar na ndugu na jamaa huko Nzega. Tupo pamoja nanyi na Mola awape nguvu.”