MBUNGE MAYENGA AWATAHADHARISHA AKINA MAMA KUBEZA VIKUNDI


Mbunge wa viti maalumu mkoani Shinyanga Lucy Mayenga, amewataka akina mama kuacha tabia ya kubeza kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali, ambayo ndiyo chachu ya maendeleo kwao kwa kuwainua kiuchumi.

Mayenga amebainisha hayo leo April 27,2018 wakati alipokutana na kikundi cha ujasiriamali cha akina mama wa Soko la nguzo Nane mjini Shinyanga, kutekeleza ahadi yake ya kuwanga mkono ya kuwachangia Shilingi Milioni Moja Taslimu(1,000,000), ilikuongeza mfuko wao na waweze kukopeshana ili kupanua biashara zao.


Alisema hua anasikitishwa na baadhi ya akina mama ambao wamekuwa na tabia ya kujiunga katika vikundi na baadae kujitoa kwa sababu mbalimbali na kutoa wito kwao wasiwe waoga kwenye kuthubutu kutafuta maendeleo pamoja na kutobeza vikundi.

“Natoa wito kwa akina mama muache kubeza vikundi, na msiwe waonga kuthubutu kutafuta maendeleo, na kikundi hiki cha wajasiriamali wa nguzo nane nakipongeza sana kwa umoja wenu ambao mnaendelea nao, na leo nimekuja kutekeleza ahadi yangu nawapatia hapa hapa Shilngi Milioni Moja Taslimu,”alisema Mayenga huku akitoa pesa hiyo.


“Naomba pia kikundi hiki cha akina mama wa soko la nguzo nane mkisajili kikundi chenu, muunde katiba yenu, muwe waaminifu katika pesa, na mundelee kukopeshana ,na mimi sitachoka kuwasaidia nitakuwa na wasiliana na viongozi wenu, endeleeni kufanya kazi ili muinuke kiiuchumi,”aliongeza.


Naye katibu wa kikundi hicho Frola Silvester ,akisoma taarifa alisema walianza March 3 mwaka huu kwa kuhamasishwa na mbunge huyo, na walikuwa 103 lakini wengine walijitoa, na hivyo kubakia wanachama hai 84 mpaka sasa kwenye mfuko wao wanajumla ya Shilingi Milioni 2,6 ikijumlishwa na pesa ya mbunge, na wamekuwa wakikopeshana kwa riba nafuu.


Kwa upande wake mwenyekiti wa Soko hilo la Nguzo Nane Hassani Baruti alimpongeza mbunge huyo kwa kutekeleza ahadi yake, ambapo tayari kulianza maneno kwa baadhi ya akina mama hao kuwa wamedanganywa kusaidiwa, na kufikia hatua wengine kujiondoa.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Shinyanga Lucy Mayenga akizungumza na akina mama wajasiriamali wa Soko la Nguzo Nane mjini Shinyanga, na kuwataka wasiwe waoga katika kuthubutu kwenye utafutaji wa maendeleo, pamoja na kujiunga kwenye vikundi ilikupeana nguvu ya kupanua wigo wa biashara zao kwa kukopeshana sanjari na kuweza kupata mikopo kwa urahisi kupitia fedha za halmashauri za maendeleo ya jamii asilimia Tano.
Mbunge wa Viti maalumu mkoani Shinyanga Lucy Mayenga akionyesha pesa Taslimu Shilingi Milioni moja( 1,000,000) ambayo aliahidi kuwapatia akina mama hao kwa kuwaunga mkono kwenye kikundi chao.

Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Shinyanga Lucy Mayenga akimkabidhi pesa hiyo Shilingi Milioni Moja mwenyekiti wa Soko hilo la Nguzo Nane Hassani Baruti, kwa ajili ya kuwaunga mkono akina mama hao wajasiriamali.

Katibu wa umoja wa wanawake CCM (UWT) Wilaya ya Shinyanga mjini Roda John Madaha akimpongeza mbuge huyo kwa kutekeleza ahadi yake, na kuunga juhudi za Rais John Magufuli za kusaidia watu wanyonge kuwainua kiuchumi.

Mwenyekiti wa umoja wa wanawake CCM (UWT) Wilaya ya Shinyanga mjini Shumbuo Katambi, akizungumza kwenye hafla hiyo fupi amempongeza mbunge huyo, na kuwataka akina mama ambao hawapo kwenye vikundi wajiunge ili wapate kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha biashara za uzalishaji mali.
Diwani wa Viti maalumu manispaa ya Shinyanga Mariamu Nyangaka naye akimpongeza mbunge huyo kwa kutekeleza ahadi yake ya kusaidia kikundi hicho cha akina mama wajasiriamali wa soko la Nguzo Nane, na kuwataka waendelee kujituma kufanya kazi ikiwa maendeleo hayaji kwa kukaa nyumbani.
Akina mama wajasiriamali wa soko la Nguzo Nane mjini Shinyanga wakiwa kwenye hafla yao fupi na mbunge huyo Lucy Mayenga ya kutekeleza ahadi yake ya kuwapatia shilingi Milioni moja kwa ajili ya kuwa unga mkono, ahadi aliyoitoa mwezi uliopita huku pesa hiyo ikiwa imepokelewa na mwenyekiti wa soko la nguzo Nane Hassani Baruti.

Akina mama wajasiriamali wa soko la nguzo Nane mjini Shinyanga wakiendelea kusikiliza Nasaha za mbunge huyo pamoja na viongozi alioambatana nao, juu ya umuhimu wa kujiunga kwenye vikundi na faida ya kujituma kufanya kazi.

Akina mama wakiendelea na kusikiliza jumbe mbalimbali kutoka kwa mbunge wa Viti maalumu mkoani Shinyanga Lucy Mayenga na kuwa ahidi kuendelea kuwasaidia iliwapate kujikwamua kiuchumi kupitia kikundi chao.

Akina mama hao wakiendelea kusikiliza maneno ya faraja na kutakiwa kutobeza kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali ikiwa umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu.



Akina mama wajasiriamali wa Soko la Nguzo Nane mjini Shinyanga wakiendelea kusikiliza nasaha kutoka kwa Mbunge Lucy Mayenga wakati akitekeleza ahadi yake ya kuwapatia Shilingi Milioni Moja ya kuwaunga mkono kwenye kikundi chao.




Katibu wa kikundi hicho Frola Silvester ,akisoma taarifa alisema walianza March 3 mwaka huu kwa kuhamasishwa na mbunge huyo, na walikuwa 103 lakini wengine walijitoa, na hivyo kubakia wanachama hai 84 mpaka sasa kwenye mfuko wao wanajumla ya Shilingi Milioni 2,6 ikijumlishwa na pesa ya mbunge, na wamekuwa wakikopeshana kwa riba nafuu.
Mwenyekiti wa Soko hilo la Nguzo Nane Hassani Baruti akimpongeza mbunge huyo kwa kutekeleza ahadi yake, ambapo tayari kulianza maneno kwa baadhi ya akina mama hao kuwa wamedanganywa kusaidiwa, na kufikia hatua wengine kujiondoa.

Akina mama wajasirimali wa Soko la Nguzo Nane mjini Shinyanga wakimpongeza Mbunge huyo wa Viti maalumu mkoani Shinyanga Lucy Mayenga kwa kuwaunga mkono kwenye kikundi chao kwa kuwapatia fedha hiyo Shilingi Milioni Moja Taslimu.

Akina mama wajasiriamali wa soko la Nguzo Nane mjini Shinyanga wakimkumbatia pia Mwenyekiti wa umoja wa wanawake CCM (UWT) Wilaya ya Shinyanga mjini, Shumbuo Katambi ambaye aliambatana na Mbunge huyo wa Viti Maalumu Lucy Mayenga kutekeleza ahadi yake ya kusaidia akina mama hao kuwa unga mkono kwenye kikundi chao kwa kuwachangia pesa shilingi Milioni Moja.



Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.

Powered by Blogger.