MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI ADAIWA KUBAKWA KWA KUDANGANYIWA MAANDAZI
Mwanafunzi anayesoma darasa la Pili katika shule ya Msingi Ndala ‘A’manispaa ya Shinyanga (jina limehifadhiwa), mwenye umri wa miaka (9) mkazi wa Kata hiyo ya Ndala mjini hapa, amedaiwa kubakwa na mwanaume aliyetajwa kwa jina la Amosi Meshack mfanyabiashara wa kuuza pemba.
Akizungumzia tukio hilo leo mama mzazi wa mtoto huyo Fatuma Ally, alisema limetokea jana majira Saa Saba mchana, ambapo aligundua mwanae huyo akiwa amebakwa mara baada ya kuona nguo zake za ndani zikiwa zimefichwa nyuma ya kitanda, huku chupi ikiwa na damu pamoja na mbegu za kiume na yeye kuonekana kuwa mnyonge.
Alisema baada ya kumbana mwanaye huyo, alisema kuwa amebakwa na Baba Amani ambaye ndiye Amosi Meshack, na kuwa huo ndio mchezo wake wa kila siku ambapo wakati akianza uchafu huo alikuwa akimpatia Pipi, na safari hii alimnunulia Maandazi na kisha kumvutia ofisini kwake na kumbaka tena.
“Baada ya mwanangu kumtaja mwanaume huyo nilitoa taarifa Polisi pamoja na kwa Mwenyekiti wa mtaa kisha tukaenda eneo la tukio kumkamata mtuhumiwa ambapo alimbakia kwenye ofisi yake ya kutengenezea Pemba, na sasa ana shikiliwa na jeshi la Polisi,” alisema mama mzazi wa mtoto huyo.
“Pia nilimpeleka kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwenda kupimwa, na majibu ya daktari yalivyotoka ilibainika kweli mwanangu amebakwa na mchezo huo amekuwa akifanyiwa kila mara na siyo mara moja, na hali yake anaendelea vizuri,”aliongeza.
Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kamishina msaidizi wa Polisi Simoni Haule, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na mtuhumiwa wanamshikilia, ambapo upelelezi ukikamilika watamfikisha mahakamani kujibu Shitaka linalo mkabili.
Na Marco Maduhu ambaye pia ni Mwandishi wa gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.