AUA KICHANGA KWA KUKICHIMBIA SHIMONI
![]() |
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Mika Nyange |
SOMA HABARI KAMILI
Mwanamke
anayefahamika kwa jina la Mariamu Shabani(21) mkazi wa mtaa wa Sango kata ya
Nyasubi wilayani Kahama mkoani Shinyanga anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la
Kumuua Mtoto wake Mchanga baada ya kujifungua na Kumchimbia Shimoni.
Tukio hilo
limetokea june 18 mwaka huu ambapo mwanamke huyo ni Muhudumu wa baa ya Sosho
Mjini Kahama ambaye alijifungulia nyumbani na kisha kuchimba Shimo na kukifukia
Kichanga hicho ambacho kiliokolewa na majirani na kukimbizwa hospitali ambapo
baada ya Muda mfupi Kilifariki dunia.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Graphton
Mushi kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi hilo Mika Nyange, alisema baada ya Kichanga
hicho kuokolewa na Majirani na kukimbizwa hospitali ya Wilaya hiyo na kufariki,
hivyo mzazi huyo anashitakiwa kwa kosa la Mauji.
Mushi alisema
Mwanamke huyo hivi sasa yupo chini ya Jeshi hilo na anatarajiwa kufikishwa
Mahakamani kujibu Shitaka linalomkabili la Mauji ililiwe fundisho kwa wazazi
wengine wenye tabia kama hiyo, na kukomesha Matukio ya kikatili mkoani
Shinyanga. ambayo yameonekana kushika kasi.
Katika tukio
jingine Jeshi la Polisi linamshikilia Mwanaume Balele Zanzibar mkazi wa Songwa kata
ya Mwigumbi Wilayani Kishapu kwa kosa la Kumuodhesha Mtoto wake ambaye ni Mwanafunzi wa darasa la Sita Unisi Balele kwa kupokea Ng’ombe 14 na
kumuachisha Masomo yake.
Akielezea tukio
hilo Kamanda Mushi alisema zoezi la kutimbua ndoa hiyo na kumkamata Mzazi huyo
na Muoaji lilifanyika june 18 kwa kushirikiana na Shirika la kutetea haki za
watoto Agape ambao ndio walitoa taarifa kwa Jeshi hilo na kufika eneo la tukio
na kukuta ndoa ya Kimila ikifungwa na kufanikiwa kuwa kamata wahusika wote.
“Baada ya kufika
eneo la tukio tulikuta ndoa ya Kimila ikifungwa na hivyo kuwakamata Baba wa
mtoto, na Muoaji ambaye ni Sena Sungwa
mkazi wa Maswa Simiyu kwa kosa la kuodhesha na Kuoa Mwanafunzi wa darasa la
Sita jambo ambalo ni kosa Kisheria,”alisema Mushi
Aidha Mushi
alisema watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani ilikujibu Shitaka
linalo wakabili na kupewa adhabu kali ya Kisheria, huku akitoa wito kwa wazazi
na walezi mkoani Shinyanga kuacha tabia ya kuthamini Mifugo na kukatisha Ndoto
za watoto wao kwa kuwaodhesha wakiwa na umri mdogo
Na Marco Maduhu -Shinyanga