BABA AMGEUZA MKE MTOTO WAKE WA MIAKA MITATU
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Maganzo wilayani Kishapu wakiwa kwenye Kituo cha Polisi Maganzo wakishuhudia tukio hilo la Kinyama |
SOMA HABARI KAMILI KWA CHINI
Kishapu.
Mwanaume
anayefahamika kwa jina la Ngasa Sekwa mkazi wa Kijiji cha Masagala kata ya
Maganzo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa
tuhuma za kumgeuza Mke mtoto wake wa miaka mitatu ambaye amekuwa akimbaka mara
kwa mara na kumsababishia Maumivu makali sehemu zake za siri.
Mtuhumiwa huyo
ambaye amesha achana na mke wake (2015 ) ambapo mtoto wake alimpeleka kuishi
kwa Bibi yake, lakini alikuwa akimfuata kila siku mtoto huyo ambaye (jina
limehifadhiwa) na kwenda kumbaka na kisha kumrudisha majira ya jioni kwa Bibi
yake Mahari anapolelewa.
Akizungumza
mbele ya mkuu wa wilaya ya Kishapu Hawa Ng’humbi Kwenye kituo cha Polisi
Maganzo, Bibi wa mtoto huyo Milembe Luhende alisema Baba yake alikuwa akimfuata
mtoto kila Siku, Pale anapotoka kwenye Shughuli zake za ulinzi na kwenda naye
kwake na kisha kumrudisha jioni ambapo Siku Moja alimuona Mjukuu wake akiwa tofauti.
“Baba ambaye
amembaka mtoto wake ni Mtoto wangu mimi wa kumzaa hivyo siwezi kumsingizia na
nimekasilishwa sana na unyama aliokuwa akimfanyia Mjukuu wangu na kufikia hatua
ya Kumshitaki iliachukuliwe hatua kali za Kisheria maana huwezi kumgeuza Mke Mtoto
wa miaka mitatu,”alisema Luhende
Aliongeza” Siku
ya tarehe 7/6/2016 ambapo mjukuu wangu alipochukuliwa na baba yake
aliporudishwa nilimuona akiwatofauti akijikuna sehemu za siri na nilipoanza kumuogesha
nilimuona amevimba huku akitokwa na uchafu ambazo ni Mbegu za Kiume na
kushitukia mchezo huo mchafu aliokuwa akifanyiwa.”
Aidha bibi huyo
alifafanua kuwa mara baada ya kuona hali hiyo alitoa taarifa kwa uongozi wa
Kijiji na Kata na kuchukua hatua ya kwenda kushitaki pia kwenye Kituo cha
Polisi ambapo walimchukua mtoto na kumpeleka kwenye kituo cha afya na kubaini
Mjukuu wake alikuwa amebakwa.
Kwa upande wake
Kaimu mkuu wa kituo cha Polisi Maganzo Osca Shani alikiri kufanyiwa uchunguzi
wa kitalaamu mtoto huyo, na kubainika kubakwa ambapo pia walimuuliza Maswali na
kumtaja Baba yake kumfanyia kitendo hicho, na kisha Kumkamata Mtuhumiwa na
Kumsweka Rumande ilisheria ichukue Mkondo wake.
Aidha Mkuu huyo
wa wilaya ya Kishapu Hawa Ng’humbi ambaye alifika kushuhudia tukio hilo
alivitaka vyombo vya dola kutoichezea Kesi hiyo nakutaka Mtuhumiwa huyo
afikishwe Mahakamani haraka na kufungwa Jela ilikuondoa Matatizo ya ubakaji
wilayani humo ambapo mpaka sasa watoto 5 wameshabakwa
.
Na Marco Maduhu-ambaye pia ni Mwandishi wa Nipashe -Shinyanga cont 0758059936