HATIMAYE WATOTO ALBINO WAPATIWA TIBA YA KUNGUNI, NI MATOKEO BAADA YA KURUSHA HABARI HIYO



Mtalamu wa mifugo kutoka Manispaa ya Shinyanga akipulizia dawa ya kuuwa wadudu aina ya Kunguni kwenye kituo cha kulea watoto Albino kilichopo mjini Shinyanga ambapo watoto hao walikuwa wakikimbia Vitanda na Kulala nje kukwepa wadudu hao kuendelea kudhohofisha afya zao kwa kuwang'ata

Mtaalamu akichanganya dawa ya kuuwa Kunguni
Upuliziaji wa dawa ya kuuwa Kunguni Ukiendelea
Magodoro ya watoto hao Albino yakiwa Nje wakati upulizaji dawa ya Kunguni ukiendelea
Watoto hao albino wakifurahia baada ya wadudu hao Kunguni Kupuliziwa dawa ya kuwa maliza maana ilikuwa Kero kwao

June 17 Blog hii na kupitia Gazeti lake la Nipashe na kusambaza taarifa zingine kwenye vyombo mbalimbali vya habari juu wa watoto hao Albino Kushambuliwa na Kunguni na Hatimaye habari hizo zimeleta Matokeo Chanya na Hatimaye watoto hao wamepata tiba baada ya Serikali Kupuliza dawa hiyo ya kuuwa Kunguni  

HABARI ILIYO RUSHWA HII HAPA CHINI

WATOTO ALBINO WATESWA NA KUNGUNI

Na Marco Maduhu
Shinyanga.

Watoto wenye ualbino wanaolelewa kwenye kituo cha buhanghija Mjini Shinyanga wameendelea kushambuliwa na wadudu aina ya Kunguni kituoni hapo, hali ambayo imekuwa ikiwalazimu kukimbia vyumba vyao na kulala nje nyakati za usiku sababu ya kuteswa na wadudu hao.

Kituo hicho cha watoto Albino 431 Kimekuwa kikishambuliwa na Kunguni mara kwa mara na kuwafanya kuishi maisha ya tabu kituoni hapo licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali lakini wadudu hao wameonekana kuwa kero kwao pamoja na kuwa athiri Kiafya.

Wakizungumza  jana na Nipashe Kituo hapo wakati Chama cha walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Shinyanga kilipotembelea kwenye kituo hicho kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika na kutoa Misaada Mbalimbali ikiwamo Chakula na Nguo, kuwa kero kubwa ambayo imebaki ikiwakabili ni Wadudu hao Kunguni.

Mmoja wa Watoto hao Emmanuel Deusi alisema kutokana na wadudu hao kuendelea kuwatesa imefikia Kipindi wamekuwa wakikimbia kulala vyumbani na kumalizia usingizi wao nje ya Vibaraza vya Majengo yao kwa ajiri ya kuwakwepa Kunguni wasiendelee kudhoofisha afya zao.

“Kunguni hawa wamekuwa kero kwetu wanatushambulia sana hivyo tunaomba wadau wajitokeze kutusaidia kupuliza dawa ambayo itamaliza tatizo hili maana kanisa la (KKKT) Mjini Shinyanga lilisha kuja kupuliza dawa Kipindi cha nyuma lakini hawakufa na kuendelea kutushambulia,”alisema Deusi

Naye Mlezi wa kituo hicho Sasu Nyange alisema Kunguni hao wamekuwa wagumu kufa maana kila Mwezi wamekuwa wakipuliziwa dawa lakini hawafi, huku akitoa wito kwa wataalamu wa mifugo kujitokeza Angalau kuwasaidia Dawa Kali ambayo itawamaliza wadudu hao na kutoendelea tena kuwa tafuna watoto hao.

Kwa upande wake Mwakilishi wa kitengo cha walimu wanawake mkoani Shinyanga kutoka kwenye Chama cha walimu Tanzania mkoani hapa (CWT), Neema Obed, alisema Jukumu la kuwalea watoto hao nila wananchi wote, hivyo ni vyema jamii ikiwa na Moyo wa kujitolea kuwamalizia matatizo yao.

Aidha Mkurungenzi wa halmashauri hiyo ya Manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna alikiri kusikia tatizo hilo la Kunguni na kuahidi kulifanyia utatuzi wa haraka ilikunusuru afya za watoto kuendelea kushambuliwa na wadudu hao.

MWISHO
     





















Powered by Blogger.