MCHUNGAJI ALAANI WANANCHI KUABUDU WAGANGA WA KIENYEJI

 Mchungaji wa Kanisa la Asseblies of God la Ngokolo Mjini Shinyanga Amosi Ng'osha akitoa Mahubiri kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Bugoyi 'A' Mjini humo na kuwataka wakazi wa mkoa wa Shinyanga na Kanda ya ziwa kwa ujumla kuacha kuendekeza Imani za Kishirikina na kuabudu waganga wa Kienyeji ambao wamekuwa wakiwapigia Ramli Chonganishi na kusababisha Mauji ya Vikongwe na Albino.

Hapa ni Mwibaji Simoni Yohana Kutoka Kongo akitoa buruduni ya Nyimbo za Kumsifu bwana kwenye Mahubiri hayo
 Hapa ni Mwibaji Fanue Singu anayetamba na kibao cha Yesu ni zaidi ya Kikombe Cha Babu naye akitoa burudani ya Nyimbo za Injiri kwenye Mahubiri hayo ambayo yamelenga kumaliza Tatizo la Mauji ya watu wasio na hatia.
 Mwimbaji wa nyimbo za Injiri hapa nchini Enock Jonas mwenye kibao kilicho vuma cha Zunguka Zunguka naye hakuwa nyuma kutoa burudani za nyimbo za bwana kwenye mkutano huo wa Neno la Bwana , ambao utamalizika Siku ya Jumapili.
 Mwimbaji Enock Jonas akiendelea kutoa burudani kwa wananchi wa Mji wa Shinyanga waliofika kwenye mkutano huo wa Neno la Bwana huku akiwa na Kijana wake ambaye alikonga nyoyo za watu waliofika kupata toba kwenye Mahubiri hayo.
 Baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye Mahubiri hayo walipendezwa na Kijana wa Mwimbaji huyo Mwenye Kibao cha Zunguka Zunguka Jinsi anayocheza Nyimbo hiyo ya Injiri na kuamua kumpatia zawadi ya Pesa.
 Burudani za Nyimbo za Bwana zikiendelea
Hapa ni Mwimbaji Jaklini Sikamwe mwenye wimbo anaotamba nao wa Dada wa Kkudance na Yesu naye hakuwa Nyumba kutoa burudani ya nyimbo za kumsifu bwana kwenye Mhubiri hayo
Pia kwenye Mahubiri hayo watu Mbalimbali walifanyiwa maombi ya kuponywa Matatizo yao


Maombezi yakiendelea huku baadhi ya watu wakitolewa Mapepo ambayo yamekuwa yakiwasumbua




 SOMA HABARI KWA KINA


Mchungaji wa kanisa la Kipentecoste Asseblies of God la Ngokolo Mjini Shinyanga  Amosi Ng’osha amelaani tabia ya wakazi wa mjini hapa, kuendekeza Masuala ya Imani za Kishirikina ambazo zimekuwa zikisababisha mauaji ya watu wasio na hatia yakiwamo ya vikongwe na Albino.

Ng’osha amekema tabia hiyo kwenye Mahubiri yake anayoyaendesha Mjini humo ya siku 7  kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Bugoyi ‘A’yenye lengo la kukemea mauji ya watu wasio na hatia Kanda ya Ziwa, ambayo kwa asilimia kubwa yamekuwa yakisababishwa na Imani za Kishirikina.

Ng’osha akitoa mahubiri hayo kwa wakazi wa mji wa Shinyanga aliwataka kuachana na dhana ya kuwaabudu waganga wa Kienyeji kwa kuwapelekea Matatizo yao wakiamini kuwa wamelongwa hali ambayo imekuwa ikisababisha Mauji ya watu hao wasio na hatia baada ya kupigiwa Ramli Chonganishi.

“Tatizo la Mauji ya Vikongwe na Albino kanda ya ziwa yamekuwa yakisababishwa na wananchi wenyewe kwa kuendekeza Masuala ya Imani Potofu za Kishirikina na hivyo kukimbilia kwa wanganga wa Kienyeji ambao wamekuwa wakiwapigia Ramli Chonganishi na kutekeleza mauji ya watu wasio na hatia,”alisema Ng’osha

Aliongeza”Katika Mahubiri yangu haya yaliyolenga kumaliza tatizo hili la Mauji ya Wazee na Albino endapo wananchi wakilishika Neno la Bwana Vizuri na kuacha kuhusudu Imani za Kishirikina, Mauji haya Mkoani Shinyanga na Kanda ya Ziwa yote yatakoma kabisa na kubaki kuwa historia tu.”

Aidha Mchungaji huyo akiendelea na Mahubiri yake pia alilaani Matukio ya Mauji ya Kinyama yaliyotokea hivi karibuni mkoani Mwanza,Geita na Tanga ya watu wasio na hatia kuuawa kwa kukatwa Mapanga ovyo kama wanyama, na kuwataka wananchi waishi kwa hofu ya Mungu na kutoichafua Amani ya Tanzania.

Pia Ng’osha amelitaka Jeshi la Polisi hapa nchini kuhakikisha linafanya kazi kwa uadilifu mkubwa wa kulinda Raia na Mali zao kwa kuimarisha ulinzi kila kona, pamoja na kuwabaini waharifu ambao wamekuwa wakitekeleza mauaji ovyo na kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Na Marco Maduhu -Shinyanga






Powered by Blogger.