Mwanamke auawa kwa kunyongwa Shingo na Kanga Kisa Wivu wa Kimapenzi
NB-Picha haihusiani na habari hapa chini
Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Rehema Tumbo (32) mkazi wa kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga ameuawa kwa kunyongwa na kanga na Mume wake Raphael Kazembe kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi ambapo mwanamke huyo alichelewa kurudi nyumbani kwake.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa tano usiku ambapo mwanamke huyo baada ya kurudi nyumbani kwake alikuta mlango umefungwa kwa ndani huku Mume wake akimsubiri, na alipogonga hakufunguliwa.
Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog baada ya mumewe kugoma kufungua mlango,mwanamke huyo alilazimika kwenda kulala kwenye chumba cha watoto ambapo mume wake alimfuata na kuanza kumshushia kichapo kisha kumnyonga kwa kanga shingoni.
Akielezea tukio hilo mtoto wa marehemu Godfrey Raphael (15) ambaye ni mtoto wa kufikia kwa mume wake alisema mama yake huyo alikuwa amesindikiza wageni na aliporudi nyumbani majira hayo ya saa tano, alikuta baba yake amefunga mlango kwa madai alikuwa ametoka kwa wanaume na ndipo ugomvi ulipoanza.
“Baada ya Mama kuona baba hafungui mlango mama alitugongea sisi tukamfungulia ili aje kulala kwenye chumba chetu lakini baba alimfuata na kumpeleka chumbani kwake na kuanza kumpiga, na baada ya kuona Mama anazidi kupigwa huku akikoroma ni kakimbia kwa mwenyekiti kutoa taarifa”,alisema Raphael.
Mwenyekiti wa mtaa huo wa Ndala Edward Mihayo aliiambia Malunde1 blog kuwa, baada ya kupokea taarifa hiyo kutoka kwa mtoto wa marehemu alifika eneo la tukio na kumkuta Mwanamke huyo amelala chini huku akiwa na kanga shingoni tayari ameshakufa, na hivyo kuamua kupiga filimbi kukusanya wananzengo pamoja na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi.
Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Graiftoni Mushi alikiri kutokea kwa tukio hilo la mauaji na maiti imehifadhiwa mochwari kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa huo na kwamba jeshi linamtafuta mtuhumiwa ambaye amekimbia mara baada ya kufanya mauaji.

Na Marco Maduhu Shinyanga