WAKANDARASI WATAKAOJENGA MIRADI YA MAENDELEO CHINI YA KIWANGO KUNYIMWA TENDA HALMASHAURI
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Steven Masele katika Mwenye flekta ya Zambarau akitoa maelekezo kwa Mashauri wa Mradi wa ujenzi wa barabara tanroad kwa kiwango cha Lami Km 2.3 aliyepo kulia kwake Paulo Saitabau kuwa barabara hiyo ijengwe kwa kiwango bora .
Mbunge Steven Masele akiendelea kutoa Ushauri wa Ujenzi huo wa barabara kwa Kiwango cha Lami kujengwa kwa kiwango kinachotakiwa.
Mbunge Masele akipiga picha ya Pamoja na wakandarasi wa ujenzi huo wa Lami Chini ya Tanroad |
Ukaguzi wa barabara za katikati ya Mji wa Shinyanga ukiendelea |
Ukaguzi ukiendelea huku wakibadilishana Mawazo |
Ukaguzi wa barabara kwa kiwango cha Lami katika ya mji ukiendelea huku kazi ikifanyika |
Ukaguzi Mwingine wa ujenzi wa Matundu ya choo 18 katika Shule ya Sekondari Masekelo Manispaa ya Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele akiwa na mkurungezi wa halmshauri ya manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna wakikagua matundu vya vyoo 18 vilivyomalizika kunjengwa katika shule ya sekondari Masekelo iliyopo katika manispaa hiyo.
Zoezi la kukagua matundu ya vyoo likiendelea
Mheshimiwa Masele akikagua choo
Mheshimiwa Masele (kulia) akiteta jambo na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna
Mheshimiwa Masele na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga wakielekea kwenye eneo panapojengwa nyumba ya walimu
Mheshimiwa Masele akikagua ujenzi wa nyumba ya walimu ambayo itahifadhi walimu sita itakayokamilika mwezi Julai mwaka huu na kughalimu shilingi milioni 150 ambapo ndipo amebaini matofari na kukoto zinazotumika kujenga nyumba hiyo hayana ubora na kuagiza tofari na kukoto ziondolewe ziletwe zenye kiwango bora. Mheshimiwa Masele akiwa eneo la ujenzi na mhandisi wa ujenzi wa manispaa ya Shinyanga Simon Ngagani .(aliyenyoosha mkono) akitoa maelekezo.
Masele kushoto katikati Mkurugenzi mwisho mhandisi Simon Ngagani (kulia) wakiangalia darasa lililomalizaka kujengwa kwenye shule hiyo ya Masekelo .
Mheshimiwa Masele akiwa nje ya darasa hilo Mheshimiwa Masele akizungumza na wanafunzi wa shule ya Masekelo na kuwataka wasome kwa bidii il iserikali hapo baadae ipate wataalamu wake pamoja na kufanikiwa katika maisha yao na kusaidia wazazi wao.
Mheshimiwa Masele akizungumza na wanafunzi wa shule ya Masekelo na kuwataka wasome kwa bidii il iserikali hapo baadae ipate wataalamu wake pamoja na kufanikiwa katika maisha yao na kusaidia wazazi wao.
SOMA HABARI KWA KINA
Mbunge wa jimbo
la Shinyanga Mjini Steven Masele ameonya wakandarasi wanaojenga miradi ya
maendeleo chini ya Kiwango jimboni kwake,
na kutaka miradi hiyo waijenge kwa hadhi ya juu kulingana na pesa wanazopewa na
siyo kuilipua na kuingizia hasara serikali fedha za matengenezo ya mara kwa
mara.
Masele alitoa
kauli hiyo wakati akikagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa jimboni mwake na
kukuta Mradi Mmoja wa ujenzi wa nyumba ya walimu katika Shule ya sekondari
Masekelo ambayo itakuwa na uwezo wa kuhifadhi walimu Sita, kutaka kujengwa
Chini ya Kiwango kutokana na Matofari na kokoto kutokuwa na ubora.
Akizungumza
wakati akikagua Miradi ya ujenzi huo wa nyumba za walimu, Madarasa Mawili, Matundu
ya vyoo 18 katika shule hiyo ya Masekelo, na ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya
Tanroad km 2.3 na zile zinazojengwa katikati ya mji Km 13.1 na kuwataka
wakandarasi wote kujenga Miradi hiyo kwa kiwango kinachotakiwa.
“Mkurugenzi
mkandarasi huyu anayetaka kujenga nyumba hii ya walimu Chini ya kiwango, kwanza
Tofari na hizi Kokoto aziondoe aweke tofari zingine tena na ujenzi wake
asimamiwe kikamilifu maana asije akalipua kazi na hapo baadae nyumba hii ikaja
kuleta maafa,” alisema Masele na kuongeza kuwa
“Pia naagiza
wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ya Maendeleo kwenye jimbo langu waijenge
kwa kiwango kinachotakiwa na siyo kulipua kazi ili miradi hii ipate kudumu kwa
muda mrefu na kutekeleza miradi Mingine ambayo itaondoa kero kwa wananchi na
kuufanya mji wa Shinyanga kuwa wa Kisasa na kukua kiuchumi.”
Naye Mkurugenzi
wa halmashauri hiyo ya Manispaa ya Shinyanga Kalinjuna Lewis amesema Mkandarasi
anayejenga nyumba hiyo ya walimu alisha mwambia aondoe Tofari hizo na Kokoto
lakini amekuwa mkaidi, huku akibainisha kwa Mkandarasi atakaye jenga miradi
chini ya Kiwango atakuwa amejiondoa kupata kazi tena .
Na Marco Maduhu ambaye pia ni Mwandishi wa Theguardian na Nipashe- Shinyanga