WANANCHI WAMFUNGIA BARABARA MKANDARASI KWA MAGOGO,MAWE
![]() |
Mgomo ukiendelea huku Jeshi la Polisi Likiimarisha Ulinzi na Usalama. |
![]() |
Mgomo Ukiendelea |
SOMA HABARI KWA KINA
Wananchi wa kata
ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga wamemzuia mkandarasi anayesomba Moramu kwenye
eneo hilo (JASCO) kwa kufunga barabara kwa Magogo,Miti, Kamba na Mawe ilikumzuia
asiendelee na Shughuli hiyo kwa madai ya kutishia usalama wa Maisha yao baada
ya Magari yake kukimbia kwa mwendo kasi na kutimua vumbi kali kwenye makazi yao.
Tukio hilo
limetokea jana majira ya Saa moja asubuhi ambapo wananchi hao wakishilikiana na
viongozi wao akiwamo diwani wa kata hiyo Samweli Sambayi walifunga barabara
hiyo ndani ya Masaa Sita, huku wakizuia Magari ya Mkandarasi huyo yasifanye
shughuli ya kusomba Moramu mpaka pale watakapo hakikishiwa usalama wao.
Wakizungumza na
Waandishi kwenye tukio hilo baadhi ya Wananchi hao Asha Rajabu, Emmanuel
Masanja na Salu Nkwabi walisema Magari ya Mkandarasi huyo yamekuwa yakitimua
Vumbi Kali kwenye Mkazi yao huku
yakikimbia Mwendo Kasi hali iliyowalazimu kuifunga barabara hiyo.
Masanja alisema
Magari ya Mkandarasi huyo yamekuwa kero kwenye eneo lao ambayo yanasomba Moramu
na kupelekea Mjini Kwenye ujenzi wa barabara za Lami km 13, lakini kutokana na
vumbi hilo Tayari wameshaanza kupatwa na Magonjwa ya Kikohozi kisicho Isha Kuugua Kifua pamoja na kuhofia maisha yao kwa
kugongwa na Magari.
“Tunachotaka
sisi huyu Mkandarasi Jasco atengeneze kwanza barabara hili kwa kulikwangua
pamoja na kumwaga Maji mara kwa mara ilikupunguza vumbi litatumaliza,
pamoja na
Madereva wake wapunguze Mwendo kasi wa Magari ilikunusuru maisha yetu,”alisema Masanja
Naye Diwani wa
Kata hiyo ya Masekelo Samweli Sambayi alisema wameamua Kufunga barabara hiyo
ilitatizo lao litatuliwe haraka sababu wameshapeleka Malalamiko yao kwenye
uongozi wa halmashauri na Mkandarasi huyo, lakini wamepuuzia na kuendelea
kutishia usalama wa maisha ya wananchi wake.
Kwa upande wake
Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya Jasco inayosomba Moramu kwenye Kata hiyo Vasanth
Kumar, alikiri Malalamiko hayo Kuyafahamu huku akianza ukarabati wa barabara
hiyo mara moja nakuahidi kulimwagia maji muda wote pamoja na kuwazuia Madereva
wake kutoendesha Magari kwa Mwendo Kasi.
Na Marco Maduhu, Msukuma Blog