WATOTO WENYE ALBINO WASHAMBULIWA NA KUNGUNI KITUONI WAKIMBIA VITANDA

Baadhi ya watoto wenye ulemavu wa Ngozi Albino wanaolelewa kwenye Kituo cha Buhanghija Mjini Shinyanga wakiwa  wamelala nyakati za mchana baada ya kuchoka na Pilikapilika za hapa na pale ambapo wametandikiwa Shuka Safi baada ya wageni kuwatembelea kwenye Kituo hicho, lakini wamekuwa wakilala kwenye Mazingira Sio Rafiki huku wakishambuliwa na Wadudu aina ya Kunguni na kuwafanya Kutofurahia usingizi wao hususani Nyakati za Usiku.
Hapa ni wageni ambao ni Walimu wanaotoka kwenye Kitengo cha Chama cha walimu wanawake kutoka  UWT Mkoani Shinyanga wakiadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika kwenye kituo hicho cha Albino kwa kupika Chakula Pamoja na kula nao ilikuwaonyesha Furaha kwao ikiwa Asilimia kubwa watoto hao wameshatelekezwa na wazazi wao kwenye kituo hicho na hivyo kuhudumiwa na wasamaria wema kwa asilimia kubwa.

CWT Wakiendelea na Mapishi ya Chakula kwenye Kituo hicho, huku wakitoa zawadi mbalimbali zikiwamo na Nguo.

Baada ya Chakula kuiva Umoja huo wa walimu wanawake kutoka Mkoa wa Shinyanga wakigawachakula kwa watoto Albino kwa aajiri ya kusheherekea siku ya Matoto wa Afrika kwa furaha na upendo.
Mwakilishi wa Walimu hao wanawake Neema Obedi akigawa maji ya kunywa kwa watoto Albino ilikula Chakula hicho vizuri na kuboresha afya zao ikiwa asilimia kubwa watoto hao Chakula Chao kikubwa ni Ugali na Maharage usiku na mchana.

Watoto Albino wakiendelea kula chakula walichoandaliwa na Walimu.
Watoto Albino walewakubwa wakichukua Chakula kilicho andaliwa na Walimu wanawake mkoa wa Shinyanga.

Chakula kikiendelea kuliwa                         
Wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna naye hakuwa nyuma kuwatembelea watoto hao, na kuahidi kuwapanulia Kituo kwa kujenga Majengo Mengine ya Kisasa ilikuwaondolea Msongamano na kulala kwa kubanana, ambapo Tayari Milioni 350 zimeshatengwa kwa ajiri ya maendeleo, pesa ambazo zitamaliza Matatizo ya uhaba wa Majengo kwa watoto hao, na aliyepo mbele ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro naye akijumuika kusheherekea na watoto hao Chakula kilicho andaliwa na Walimu.

Picha ya Pamoja mkuu wa wilaya Shinyanga Josephine Matiro (Wanne Kushoto) akiwa na Mkurungenzi wake Lewis Kalinjuna Mwenye mkoti pamoja na Walimu hao wanawake mara baada ya kumaliza kula chakula cha pamoja na watoto Albino.




 SOMA HABARI KWA KINA


Watoto wenye ualbino wanaolelewa kwenye kituo cha buhanghija Mjini Shinyanga wameendelea kushambuliwa na wadudu aina ya Kunguni kituoni hapo, hali ambayo imekuwa ikiwalazimu kukimbia vyumba vyao na kulala nje nyakati za usiku sababu ya kuteswa na wadudu hao.

Kituo hicho cha watoto Albino 431 Kimekuwa kikishambuliwa na Kunguni mara kwa mara na kuwafanya kuishi maisha ya tabu kituoni hapo licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali lakini wadudu hao wameonekana kuwa kero kwao pamoja na kuwa athiri Kiafya.

Wakizungumza  Kituo hapo wakati Chama cha walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Shinyanga kilipotembelea kwenye kituo hicho kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika na kutoa Misaada Mbalimbali ikiwamo Chakula na Nguo, kuwa kero kubwa ambayo imebaki ikiwakabili ni Wadudu hao Kunguni.

Mmoja wa Watoto hao Emmanuel Deusi alisema kutokana na wadudu hao kuendelea kuwatesa imefikia Kipindi wamekuwa wakikimbia kulala vyumbani na kumalizia usingizi wao nje ya Vibaraza vya Majengo yao kwa ajiri ya kuwakwepa Kunguni wasiendelee kudhoofisha afya zao.

“Kunguni hawa wamekuwa kero kwetu wanatushambulia sana hivyo tunaomba wadau wajitokeze kutusaidia kupuliza dawa ambayo itamaliza tatizo hili maana kanisa la (KKKT) Mjini Shinyanga lilisha kuja kupuliza dawa Kipindi cha nyuma lakini hawakufa na kuendelea kutushambulia,”alisema Deusi

Naye Mlezi wa kituo hicho Sasu Nyange alisema Kunguni hao wamekuwa wagumu kufa maana kila Mwezi wamekuwa wakipuliziwa dawa lakini hawafi, huku akitoa wito kwa wataalamu wa mifugo kujitokeza Angalau kuwasaidia Dawa Kali ambayo itawamaliza wadudu hao na kutoendelea tena kuwa tafuna watoto hao.

Kwa upande wake Mwakilishi wa kitengo cha walimu wanawake mkoani Shinyanga kutoka kwenye Chama cha walimu Tanzania mkoani hapa (CWT), Neema Obed, alisema Jukumu la kuwalea watoto hao nila wananchi wote, hivyo ni vyema jamii ikiwa na Moyo wa kujitolea kuwamalizia matatizo yao.

Aidha Mkurungenzi wa halmashauri hiyo ya Manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna alikiri kusikia tatizo hilo la Kunguni na kuahidi kulifanyia utatuzi wa haraka ilikunusuru afya za watoto kuendelea kushambuliwa na wadudu hao.

Na Marco Maduhu- Shinyanga 



Powered by Blogger.