RAIS MAGUFULI ATOA ZAWADI YA CHAKULA KAMBI YA WAZEE KOLANDOTO SHINYANGA
HABARI KWA KINA
Kambi hiyo
inalea wazee 23 pamoja na watoto wao, ambapo wamekuwa wakikabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwamo moja kubwa ya ubovu wa majengo, ambayo baadhi yao
yamesha anza kuanguka menyewe sababu ya kuchakaa na hivyo kuhofia usalama wa
maisha yao.
Akizungumza kambini hapo mwenyekiti wa wazee hao Samweli Maganga mara baada ya kupokea
zawadi hiyo ya chakula, alisema anampongeza Rais Magufuli kwa kujali makundi
maalumu, huku akiiomba serikali pia iwatatulie tatizo la ujenzi wa majengo
mapya ikiwa yaliyopo yamesha choka.
“Tunaipongeza
serikali ya awamu ya tano chini ya rais Magufuli hasa kwa kujali makundi
maalumu kwa kututatulia changamoto zetu, ikiwa baadhi zimeshatatuliwa ambapo
tumefungiwa umeme, maji yapo na suala la matibabu hatupati shida kama zamani, na
kero hii ya majengo mabovu tuna amini itatatuliwa tu,”alisema Maganga
Aliongeza”
kutokana na utendaji kazi anaouonyesha Magufuli tunamuombea kwa mwenyezi mungu
aendelee kuinyoosha nchini katika uimara wake na aiishi maisha marefu bila hata
ya kupata maradhi wala vikwanzo maana ni mkombozi wa watu wanyonge.”
Aidha akikabidhi
chakula hicho kwa niamba ya Rais Magufuli katibu tawala la mkoa wa Shinyanga
Albert Msovela, alisema wametoa mchele kilo 100, mafuta lita 20 pamoja na mbuzi
wawili, huku akiahidi serikali kuendelea kuzitatua changamoto moja baada ya
nyingine ilikuhakikisha wazee hao wanaishi mahari salama.
Naye mganga mkuu
wa mkoa wa Shinyanga dkt Ntuli Kapologwe ambaye aliambatana na katibu tawala
huyo kukabidhi zawadi hizo za chakula kambini hapo, alisema pia serikali
itafanya mkakati wa kuhakikisha wazee hao wanapatiwa kadi za bima ya afya ambazo
zitawasaidia pia kupata matibabu kwa urahisi.
Na Marco Maduhu- Msukuma Blog