RC ASHANGHAA SHINYANGA KUDUMAA KIMAENDELEO

Mkuu wa mkoa mpya wa Shinyanga Zainabu Tareck


SOMA HABARI KWA KINA

Mkuu wa mkoa wa shinyanga Zainabu Tareck ameskikitishwa na mkoa huo kuwa nyuma kimaendeleo huku wananchi wake wakikabiliwa na hali ya umaskini licha ya kuzungukwa na rasilimali nyingi, zikiwamo dhahabu, almasi na viwanda hali ambayo imemlazimu kuwaagiza wakuu wa wilaya kufanya kazi ya kuuinua kiuchumi.

Tareck amezungumza hayo july 4 mara baada ya kumaliza zoezi la kuwa apisha wakuu hao wa wilaya ambao ni Nyambonga Taraba (Kishapu), Fadhili Nkulu (Kahama) na Josephine Matiro (Shinyanga), na kuwataka wafanye kazi kwa kujituma ilikuuletea maendeleo mkoa wa shinyanga na kutatua kero za wananchi.

Alisema ni jambo la kusikitika na kushaghaza mkoa kama wa shinyanga ambao unasifika kuwa na rasilimali nyingi za madini ya dhahabu na almasi, lakini umedumaa kimaendeleo huku wananchi wake wakiwa maskini, kitendo ambacho amekipinga na kuahidi kuubadilisha kuwa kama jiji la madini.

“Haiwezekani mkoa kama huu wenye madini chungu nzima harafu unakuwa nyuma kimaendeleo, hivyo naomba na kuagiza wakuu wote wa wilaya na watendaji wa serikali tufanye kazi kwa juhudi zote ilituubadilishe mkoa wa shinyanga uonekane kama mji kweli wenye madini.”alisema Tareck

Aidha mkuu huyo wa mkoa pia aliwagiza wakuu hao wa wilaya wafanyekazi ya kurudisha heshima ya zao la pamba, ambalo limeonekana kupotea ikiwa zao hilo kwa asilimia kubwa ndio lilikuwa mkombozi wa mkulima kumuinua kichumi kwa kutatua kero zote zinazowakabili wakulima.

Nao wakuu hao wa wilaya watatu wakizungumza mara 
baada kula kiapo walimwahidi mkuu huyo wa mkoa sanjari na Rais John Magufuli, kutowaangusha kwa kuhakikisha wanafanyakazi ya kuwaletea maendeleo wananchi pamoja na kumalizia tatizo la uhaba wa madawati na kuendelea kufichua watumishi hewa.

Na Marco Maduhu- Msukuma Blog





Powered by Blogger.