SHULE YAFUNGWA KUNUSURU VIFO YA WANAFUNZI 900
![]() |
Wanafunzi wa shule ya msingi bugoyi B wakiwa eneo la vyoo vya shule hiyo pamoja na baadhi ya wazazi wao kama unavyoona wakitahamaki jinsi wanavyohatarisha usalama wa maisha yao . |
![]() |
Wazazi wakiendelea na ukaguzi wa vyoo vya shule ambavyo vishatitia na muda wowote vinaweza kuaguka baada ya kujengwa chini ya kiwango. |
![]() |
Hapa ni Mwenyekiti wa mtaa wa mbuyuni kata ya ndembezi Abdala Sube akifungua kikao cha wazazi juu ya kujadili mstakabali wa vyoo hivyo na kunusuru maisha ya watoto wao. |
![]() |
Aliyesimama ni Diwani wa kata ya Ndembezi David Nkulila akituliza mzuka wa wazazi wawe wapole ilikujadili hatima ya choo hicho. |
![]() |
Wazazi wakisikiliza neno kutoka kwa viongozi wao na hivyo kuridhia shule hiyo ifungwe hadi pale ujenzi wa choo utakapo kamilika ilikunusuru maisha ya watoto wao |
SOMA HABARI KAMILI
Shule ya msingi
bugoyi “B” iliyopo kata ya ndembezi manispaa ya Shinyanga imefungwa na idara ya
afya baada ya vyoo vyake kutitia na kuhatarisha
maisha ya wanafunzi 909 kwa kufukiwa
wakati wakijisaidia.
Siku ya jumatatu
shule zote hapa nchini zilifunguliwa baada ya likizo ya mwezi wa sita, lakini
zimepita siku mbili shule hiyo ya bugoyi imefungwa na wanafunzi kuamuliwa
kurudi makwao kasoro darasa la Saba ambao wanakabiliwa na mtihani wa kihitimu
masomo yao septemba 7 na watakuwa wanajisaidia na walimu kwenye choo kimoja.
Akisoma barua ya
kuifunga shule hiyo mbele ya wazazi na kamati ya shule afisa afya wa kata hiyo
ya ndembezi Costancia Michael, alisema walifanya ukaguzi wa vyoo vya shule hiyo
julai 12 mwaka huu wakati wanafunzi wakiwa rikizo nakukuta vyoo vya shule
vikiwa katika hali mbaya huku vikianza kuanguka.
“Kwamujibu wa
sheria ya afya ya mwaka 2009 kifungu cha 163 shule hii inapaswa kufungwa sababu
ya vyoo vyake kuwa vibovu hali ambayo ni hatari kwa maisha ya wanafunzi na
kuweza kusababisha vifo yakiwamo na magonjwa ya mlipuko kutokana na kujisaidia
ovyo kwenye uzio wa shule hiyo,”alisema Michael.
Nao wazazi
wanaosomesha watoto wao kwenye shule hiyo walikubaliana na uamuzi huo wa
kufungwa kwa shule, huku wakiitupia lawama halmashauri kwa uzembe walioufanya
wa kusimamia choo hicho kujengwa chini ya kiwango bila ya kuwekwa nondo chini
yake na kusababisha kutitia na kuhatarisha maisha ya watoto wao.
Aidha wazazi hao
waliitaka halmashauri ijenge vyoo hivyo haraka na wao hawawezi kuchangia
chochote juu ya ujenzi huo, ikiwa hapo awali mwaka (20o4 ) walichanga fedha na
hatimaye choo kujengwa chini ya kiwango kwa usimamizi wa halmashauri, hivyo wao
ndio wenye jukumu la kujenga vyoo hivyo .
Naye mwalimu
mkuu wa shule hiyo Nkulu Leostadias, alisema kufugwa kwa shule hiyo kutaathili
taaluma ya wanafunzi ikiwa walikuwa wamejipanga kufundisha kwa bidii lakini
alikishukuru wanafunzi wa darasa la Saba kubaki kuendelea na masomo kutokana na
kukabiliwa na mtihani wa kuhitimu masomo yao.
Kwa upande wake
Ofisa elimu wa shule za msingi wa halmashauri wa manispaa ya Shinyanga Yesse
Kanyuma ambaye alihudhulia mkutano huo akimwakilisha mkurungezi Lewis Kalinjuna,
alisema serikali imeshatenga Milioni 5 za kuanzia ujenzi wa vyoo hivyo, lakini
wananchi wanapaswa kuchimba shimo ndio ujenzi uanze, kauli ambayo ilipingwa
vikali na wazazi.
Na Marco Maduhu- Msukuma Blog