Waziri wa Habari Nape Nnauye amevifungia vituo vya redio vya Magic FM na Redio 5 ya Arusha kwa madai ya uchochezi.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametangaza kuvifungia kwa muda usiojulikana vituo vya Radio 5 ya Arusha na Magic FM ya Dar es Salaam kwa sababu za uchochezi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Waziri Nape amesema kuwa vituo hivyo kwa nyakati tofauti vilitangaza habari ambazo ndani yake zina uchochezi.

“Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza leo (Agosti 29 2016) hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake,” alisema Nape.

Aidha, amesema kuwa ameiagiza Kamati ya Maudhui ya vyombo vya habari kuviita vyombo hivyo na kuvihoji kwa kina kisha kumshauri hatua zaidi ya kuchukua.

Waziri huyo ameeleza kuwa Serikali inaendelea kutambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika kuleta amani na ushirikiano nchini na sio vinginevyo.

Hivi karibuni, Nape alitahadharisha kuwa vyombo vya habari vitakavyoripoti taarifa ambazo ni za uchochezi vitakumbwa na rungu la kuhusika kwa uchochezi pia.

Powered by Blogger.