MADIWANI SHINYANGA NUSURA WACHAPANE MAKONDE KWENYE BARAZA
Ofisa wa Jeshi la Polisi akiendelea kutuliza jaziba za madiwani wa chadema |
Muafaka ukiendelea kutafutwa |
Hapa ni awali madiwani wa chadema wakipiga meza, kelele kupinga baraza hilo kuendeshwa kwa madai ya kukeuka kanuni na kutaka kuwa buruza madiwan hao wapinzani. |
STORY KAMILI NA MARCO MADUHU
.Madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wamejikuta wakikosana
kuchapana makonde kwenye kikao chao cha baraza cha kawaida ,mara baada ya
madiwani wa Chadema kuanzisha vurugu kwa madai ya kuonewa kwenye kikao hicho.
Vurugu hizo zilizuka mara pale madiwani hao wa Chadema walipokuwa wakiomba
muongozo wa kanuni kwenye kikao hicho, ambapo Naibu meya Agnes Machiya
aliwapuuza na kuruhusu kikao kundelea ndipo fujo zikaanza .
Wakati fujo hizo zikiendelea Naibu Meya Agnes Machiya alimruhusu diwani wa
kata ya Kambarage Hassani Mwendapole kuendelea kusoma taarifa yake ya kata
,ambapo diwani wa Chadema kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi alikata waya wa kipaza
sauti.
Aidha baada ya waya huo kukatwa huku meza zikiendelea kupigwa kwa fujo ndipo
diwani Mwendapole alijawa na hasira na kutaka kuchapa vibao Ntobi ,ndipo diwani
wa viti maalumu Mariamu Nyangaka alimpo mtuliza Mwendapole na kumtoa eneo la
tukio.
"Haiwezekani ufanye fujo harafu ukate na waya wewe ni mtoto mdogo
nitakulamba makofi, usalama mnafanya nini humu toeni nje hawa sisi tuendelee na
kikao wameshazoea kususa hata dar ilikuwa hivyo CCM tukachukua Umeya,"
alisema Mwendapole
Hata hivyo vurugu hizo ziliendelea mpaka pale Ofisa wa Jeshi la Polisi
aliyekuwepo kwenye kikao hicho kuingilia kati na kutuliza ghasia hizo.
Baraza hilo la madiwani limejadili ajenda mbalimbali ambapo kitakaa ndani ya
siku mbili kwa kusoma taarifa mbalimbali kwa mstakabali wa maendeleo ya
wakazi wa mjini Shinyanga.
MSUKUMA BLOG