Jacob Zuma kuondoka Madarakani leo?
Jacob Zuma kuondoka Madarakani leo?
Stori kubwa inayoshika headlines Johannesburg kwa ‘Tata Madiba’ leo February 12, 2018 ni kuhusu Kiongozi wa Chama tawala nchini Afrika kusini cha ANC na Makamu wa Rais Cyril Ramaphosa amethibitisha kuwa chama kitafanya uamuzi wa mwisho juu ya hatma ya Rais Jacob Zuma.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Ca
pe Town, Ramaphosa amedokeza kuwa Rais Zuma atatakiwa kujiuzulu. Amesisitiza kuwa wala rushwa wote wanatakiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria, kitu ambacho anasema Nelson Mandela, baba wa taifa hilo alikitaka. Ramaphosa alikuwa akizungumza katika kumbukumbu ya miaka 28 toka Rais wa kwanza mzalendo wa nchini hiyo Nelson Mandela alipolihutubia taifa, mara tu baada ya kuachiwa gerezani