MCHINJA MBUZI AJINYONGA MACHINJIONI KWA MADAI MAISHA NI MAGUMU




Mwili wa marehemu Wandiba John (26)Mkazi wa Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, ukiwa umening'inia kwenye choo cha machinjio ya Mbuzi ya Ndembezi.
SOMA HABARI KAMILI

Kijana aliyefahamika kwa jina la Wandiba John (26), mkazi wa Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, amefariki dunia kwa kujinyonga katika eneo lake la kufanyia kazi kwenye machinjio ya mbuzi kwenye Kata hiyo, kwa kile kilichodaiwa kuwa maisha ni magumu.

Tukio hilo limetokea leo alfajiri majira ya saa 10 usiku wa kuamukia leo kwenye machinjio hayo ya mbuzi Kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga, ambapo marehemu huyo amekutwa na wenzake akiwa amejinyonga kwenye kolido la choo cha machinjio hayo, na hivyo kusababisha shughuli za uchinjaji mbuzi kusitishwa.

Wakizungumza na Shinyanga News Blog wachinja mbuzi wa eneo hilo Dankani Buti, alisema walipofika kufanya shughuli zao za uchinjanji mbuzi majira ya saa 11 asubuhi, ndipo wakaona mwili wa mwezao akiwa amejinyonga kwenye choo cha machinjio hayo, na kutoa taarifa Polisi ambao walifika na kuuchukua mwili huo.

“Huyu marehemu kwao kabisa ni Musoma na huku alikuja kutafuta maisha, na alikuwa akikaa ghetto hapa Ndembezi, na alikuwa mywaji sana wa pombe aina ya Gongo na kila siku alikuwa akisema ipo siku atawatia hasara familia yake kwani maisha ni magumu, na hatimaye amekamilisha usemi wake,”alisema Buti.

Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Kamishina msaidizi wa Polisi (ACP) Simoni Haule, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kubainisha kuwa mwili huo wa marehemu umepelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Aidha kwa upande wake Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga Geogre Masigati, alithibitisha kuupokea mwili huo wa marehemu majira ya saa 11 asubuhi ,na kubainisha kuwa tayari umehifadhiwa kwenye chumba cha maiti, wakisubili ndugu zake kuuchukua kwenda kuuhifadhi kwenye makazi yake ya milele.



Askali wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga wakiutoa Mwili wa marehemu Wandiba John kwenye choo cha Machinjio ya Mbuzi Ndembezi, Mahali ambapo amejinyonga kwa madai ya kukabiliwa na ugumu wa maisha, huku wananchi na wachinja mbuzi wenzake wakishuhudia tukio hilo.

Baadhi ya wachinja mbuzi wa eneo la Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, wakiwa wamesitisha shughuli zao za uchinjaji mbuzi, mara baada ya mwezao kujinyonga na kufariki dunia majira ya saa 10 alifajiri usiku wa kuamkia leo.
 
Na Marco Maduhu ,ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga Soma Nipashe kila siku upate habari za uhakika.
 
 
 
Powered by Blogger.