MIHEMUKO YA KISIASA YATAJWA KUDUMAZA UKUAJI WA MAENDELEO SHINYANGA
Mhadhiri kutoka chuo cha mipango ya maendeleo vijijini Dodoma Dkt Titus Mwageni ambaye ndiye Mwongozaji wa kikao cha wadau kutoa maoni ya kujadili maandalizi ya mpango mkakati wa miaka Mitano wa maendeleo ya halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kuelekea kuwa jiji. hadi kufikia 2023.
SOMA HABARI KAMILI
Wadau wa
maendeleo mjini Shinyanga ,wamewatupia lawama baadhi ya wanasiasa ambao
wamekuwa wakiendekeza masuala ya siasa kwenye maendeleo, na kuufanya mji huo kudumaa
kimaendeleo, kutokana na kuendelea kukabiliwa na changamoto ambazo husababisha
ukuaji wa kiuchumi kudhorota.
Walisema mji huo
umekuwa haubadiliki kimaendeleo miaka nenda rudi, na hata kuzidiwa na wilaya
yake ya Kahama, kutokana na wanasiasa mjini humo kutanguliza siasa mbele kuliko
maendeleo, ambapo wamekuwa wakikwamisha baadhi ya miradi kushindwa kutekelezeka,
kisa eneo husika lina tawaliwa na upinzani.
Waliyabainisha hayo
Februari 24/2018 kwenye kikao cha wadau
wa maendeleo wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, kilichokuwa na mlengo wa
kujadili na kutoa maoni juu ya nini kifanyike katika maandalizi ya mpango
mkakati wa miaka mitano wa halmashauri
hiyo, ilikufikia uchumi wa Kati.
Mmoja wa wadau hao
Mohamed Saguti kutoka Kata ya Masekelo mjini Shinyanga, alisema ili mji huo
upate kufanikiwa kukua kimaendeleo, ni lazima wanasiasa wakaweka vyama vyao
Kando na kutanguliza maendeleo mbele, pamoja na kuacha kuingilia kazi za
wataalamu, ndipo mfanikio ya mpango huo mkakati yataonekana.
“Mfano unakuta
kuna mradi mkubwa ambao unataka kupelekwa kwenye Kata ambayo inaongozwa na
upinzani, ili kuupanua mji na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana na
kuongeza kipato cha wananchi, lakini una shaghaa una kwamishwa
na wanasiasa na kushindwa kutekelezwa moja kwa moja,” alisema.
Aliongeza kwa
kutolea mfano miundombinu ya barabara, ambayo ndio kichocheo kikubwa cha uchumi,
ambazo mara nyingi zimekuwa zikitengenezwa kila mara zile barabara ambazo Kata zake
zinaongozwa na Chama tawala, lakini zile za upinzani hua ni mbovu, na hivyo
kudumaza kuwepo na mzunguko wa pesa, na mji kuwa nyuma kimaendeleo.
Naye Marcelina
Saulo kutoka Sekta binafsi akichangia mada kwenye kikao hicho, alisema pale
vikundi vya vijana vinapoundwa kwa ajili ya kuwezeshwa kimkopo, wengi wao wamekuwa
wakitoka chama tawala ,na hivyo kusababisha vijana wengi kuendelea kukabiliwa
na tatizo la ajira kutokana na mihemuko hiyo ya kisiasa.
Aidha mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Shinyanga Abobakari
Mkadamu, aliwatoa wasiwasi wadau hao kuwa suala la maendeleo halina Chama, ikiwa mji wa Shinyanga ni wa wote, na kuwataka
kuendelea kujikita kuchangia mada ambazo zitaufanya mji huo kukua kimaendeleo.
Alisema baadhi
ya vitu ambavyo vinapaswa kutekelezeka kwenye mpango huo mkakati, ni kuelimisha
makundi ya vijana kuwapatia elimu ya ujasiriamali na walemavu, kutatua migogoro
ya ardhi, watendaji washirikishwe kwenye utekelezaji wa shughuli za maendeleo,
pamoja na kuboresha huduma za afya.
Kwa upande weka mwendeshaji
wa kikao hicho Dkt Titus Mwageni Mhadhiri kutoka chuo cha mipango ya maendeleo vijijini mkoani
Dodoma, naye alitoa tahadhari ya kuchanganya siasa na maendeleo, na kuwataka
wanasiasa wawe na umoja katika kutatua changamoto zinazokwamisha ukuaji wa
maendeleo, ndipo watafanikiwa kufikia uchumi wa Kati na Tanzania ya viwanda.
Alisema mpango
huo mkakati ndio dira ya maendeleo ya halmashauri katika utendaji kazi na
kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa Kati, kwa kutatua matatizo yanayo wakabili
wananchi, ikiwamo kutengeneza miundombinu ya barabara, kuboresha huduma za
afya,kukaribisha wawekezaji kujengwa viwanda,,kuondoa tatizo la ajira kwa
vijana, kupunguza Kaya masikini na kuongeza vipato ndani ya familia.
Aliongeza bila halmashauri kuwa na mpango wake mkakati
ulio imara, Serikali haiwezi kupeleka fedha za maendeleo kwenye halmashauri
hiyo, na hivyo kuwataka wadau hao wachangie kutoa maoni yao, ilikufanikisha
zoezi hilo ambalo litaleta maendeleo katika mji wa Shinyanga .
TAZAMA HABARI
PICHA NA MAONI YA WADAU JUU YA HUO MPANGO MKAKATI WA KUIFANYA SHINYANGA KUWA
JIJI.
Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Geofley Mwangulumbi, akifungua kikao hicho cha wadau wa maendeleo na kuwakaribisha kuchangia maoni yao ya nini kifanyike kwenye mapango huo makakati wa miaka Mitano (2018 - 2023) ili kuleta maendeleo katika mjini wa Shinyanga na kuonekana kuwa hadhi ya jiji.
Mmoja wa wadau hao Mohamed Saguti kutoka Kata ya Masekelo mjini Shinyanga, akichagia mada kwenye kikao hicho alisema kwenye mpango mkakati huo kinachopaswa kuwepo na uimarishwaji kwanza ya miundombinu ya barabara, sababu ndio kichocheo kikubwa cha maendeleo na uchumi kukua, pia kudhibiti masoko holela wafanyabiashara watengewe maeneo ili halmashauri ipate mapato , pamoja na wanasiasa kutochanganya siasa na maendeleo kwa kuendekeza uitikadi wa vyama na kukwamisha baadhi ya miradi kutotekelezeka, ndipo mpango huo mkakati utafanikiwa na kuubadili mjini wa Shinyanga .
Marcelina
Saulo kutoka Sekta binafsi, alisema ili mjini huo wa Shinyanga upate kuchangamka na kukua kimaendeleo, kuwepo na High Shool ya Serikali, pamoja na vijana kuwezeshwa kwenye vikundi vya ujasiriamali ili wawe na shughuli za kufanya za uzalishaji mali na kuwaingizia kipato, huku akitoa tahadhari vikundi hivyo vi siundwe kisiasa sababu kumekuwa na tabia ili kijana uwe kwenye kikundi lazima utoke CCM, na kudai ikiendekezwa hivyo mpango huo mkakati hauwezi kufanikiwa, kama wasipokuwa na umoja na kuweka makandokando ya vyama vyao vya siasa pembeni.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Abobakari Mkadamu akizungumza kwenye kikao hicho aliwatoa wasiwasi wadau hao kuwa maendeleo hayana chama, hivyo kwenye mpango mkakati huo utatekelezwa kama ulivyokusudiwa ikiwa Shinyanga ni ya wote, na kutoa maoni yake kuwa ilikifanyike kwenye mpango huo ni kuelimisha
makundi ya vijana kuwa patia elimu ya ujasiriamali, na walemavu, kutatua migogoro
ya ardhi, watendaji washirikishwe kwenye utekelezaji wa shughuli za maendeleo,
pamoja na kuboresha huduma za afya.
Mtendaji wa Kata ya Chamaguha Deogratius Masalu, akichangia mada kwenye kikao hicho alisema ili mji wa Shinyanga upate kukua kimaendeleo na kupaa kiuchumi, lazima kwanza kuwekeza kwenye Kilimo cha Umwagiliaji ili kupata malighafi za uhakika ambazo zitatumika kuendeshea viwanda na kuongeza pato la watu binafsi na Serikali,pia kurudisha vyama vya ushirika sababu ndio vilikuwa nguzo ya mkulima kimafanikio,kuondoa migogoro ya ardhi, kuzui ufisadi kwenye minara ya simu ambayo huwekwa mashuleni,kufufua kiwanda cha nyama ambacho kwa sasa kimebaki kuwa gofu ili mzunguko wa pesa upatikane kwa wananchi,pia kukaribisha wawekezaji wa kiwanda cha nguo, kudhibiti unywaji wa Pombe aina ya Gongo ambayo imekuwa ikimaliza nguvu kazi ya vijana ambao wamekuwa wakishindwa kuchimba hata mitaro,pamoja na kudhibiti madangulo ambayo ndio yamekuwa chanzo cha ongezeko la watoto mitaani na kufanya walengwa wa Tasaf kuongezeka na kurudisha maendeleo nyuma.
Dastan Sechuli ambaye ni mkazi wa Kata ya Ngokolo mjini Shinyanga, alisema pia kuna paswa kurudishwa elimu ya watu wazima, ili wananchi wapate kujielewa na kupambanua mambo, sababu baadhi yao hushindwa kuelewa nini maana ya maendeleo licha ya kupewa elimu, na akili zao hubaki kuwa palepale na kujikuta wakiendelea kuwa maskini na kudumaza ukuaji wa maendeleo.
Mratibu wa miradi ya ulinzi wa mtoto kutoka Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga Alex Enock, akichangia mada kwenye kikao hicho, alisema pia kwenye mpango huo mkakati lazima liwepo suala la ulinzi wa mtoto sababu kwenye ukuaji wa maendeleo ndipo vitendo vya kikatili dhidi ya watoto hushamili, pamoja na kuboreshwa miundombinu ya watoto mashuleni ili mji wa Shinyanga upate kuwa na wasomi wengi ambao ndio chachu ya maendeleo.
Ofisa ufundi kutoka Sido mjini Shinyanga Ally Mtwale alitoa maoni kuwa yale maeneo ambayo halmashauri imesha yatenga kwa ajili ya uwekezaji, inatakiwa kuwekeza hata viwanda vidogovidogo vya uzalishaji mali ilikuongeza pato la Serikali.
Naye Mdau Emmanuel Masanyiwa, alisema ili mji wa Shinyanga upate kukua kimaendeleo, lazima pia usafiri wa daladala za baiskeli ziondoke kufanya shughuli zao katikati ya mji na kuwepo basi ndongo (HAICE), ilikuupa hadhi mji pamoja na kuwepo na mzinguko wa fedha.
Katibu wa timu ya Stand United ya mkoani Shiynyanga Kened Nyangi, alisema ili mji huo wa Shinyanga upate kukua kimaendeleo pia kuwepo na viwanja vya michezo (open space) ilikuibua vipaji vya vijana kimchezo na kupata ajira, pia Serikali iwe na mchango katika Timu ya Standi na siyo kuwa achia tu wanasiasa, sababu timu hiyo inapokuwa ikicheza ligu kuu na kuja kuchezewa kwenye uwanja wake wa nyumbani, mji hua unachangamka watu watafanyabiashara mbalimbali na kujiingizia kipato, lakini wakiicha na kushuka daraja lazima maendeleo yatapoa.
Naye msanii wa Bongo Movie mjini Shinyanga Songoro Gaddafi, alisema kwenye mpango huo mkakati wanaiomba Serikali iwashike mkono vijana waigizaji iliwaweze kupata mafanikio ikiwa hiyo ni ajira kwao, pamoja na kuwatumia kutangaza utalii wa mkoa wa Shinyanga kupitia sanaa yao, ambayo itafanya watu wengi wageni kuingia Shinyanga na kuongeza pato la Serikali na hatimaye mji kukua kimaendeleo na kiuchumi pia.
Meneja wa Shirika la Save The Children Benet Malima, akichangia maoni kwenye mpango huo mkakati, alisema pia kunapaswa kuboreshwa miundombinu mashuleni,kuzia ukatili dhidi ya watoto,kuondoa mimba mashuleni,kuwepo na mpango wa kushughulikia vyanzo vya matatizo na siyo kutatua tatizo,pia kuwepo na dampo la uchafu nje ya mji, ili Shinyanga ionekane kuwa safi, pamoja na kutolewa elimu kwa wadau juu ya masuala ya ukatili, ikiwa vitu vyote hivyo vikawa sawa ndipo maendeleo Shinyanga yataonekana.
Wadau wa maendeleo wakiwa kwenye kikao cha mpango mkakati wa maendeleo wa manispaa ya Shinyanga, wa kipindi cha miaka mitano ijayo, mara baada ya ule mkakati wa awali kuisha.
wadau wakiendelea kusikiliza maoni juu ya nini kifanyike ili mkakati huo upate kufanikiwa na kuufanya mji wa Shinyanga kuwa Jiji
Wadau wa maendeleo wakiendelea kusikiliza mawazo mbambali ya wenzao juu ya mpango huo mkakati wa kuleta maendeleo katika mji wa Shinyanga.
Wadau wa maendeleo wakitafakari juu ya nini kifanyike ili mji wa Shinyanga upate kukua kimaendeleo.
Mhadhiri kutoka chuo cha Mipango cha maendeleo vijiji mkoani Dodoma Dkt Titusi Mwageni, akipitia mada ya kueleza kwanini halmashauri lazima iwe na mpango mkakati wake wa kimaendeleo pamoja na kushirikisha wadau wake, na kubainisha kuwa ikiwa hakutokuwa na mapango huo ambao asilimia kubwa una takiwa kugusa kutatua matatizo ya kijamii, kukuza vipato na kuondoa umaskini kwenye Kaya, halmashauri hiyo itaweza kukosa fedha za maendeleo kutoka Serikali kuu,ikiwa mpango huo ndio dira ya maendeleo.
wadau wa maendeleo wakiwa ukumbini wakiendelea na kikao.
Baadhi ya wadau wa maendeleo wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, wakiandika Mawili Matatu juu ya kufanikisha mpango huo mkakati ili upate kuwa na tija kimaendeleo.
Baadhi ya watendaji wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, wakiandika maoni ya wadau juu ya nini kifanyike ili mpango huo mkakati upate kufanikiwa na kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika mji wa Shinyanga na kukua kiuchumi.
Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa Gazet la Nipashe mkoani Shinyanga.