MABINTI WALIOHITIMU MAFUNZO YA USHONAJI NGUO WASISITIZWA KUJIUNGA KWENYE VIKUNDI KUPEWA MIKOPO
Mgeni Rasmi katika mahafari ya wanafunzi wanaohitimu mafunzo ya ushonaji nguo kutoka Agape, Mwanamsiu Dosi ambaye ni Ofisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, akimkabidhi cheti mwanafunzi Rebeka Emmanuel cha kuhitimu mafunzo hayo.
SOMA HABARI KAMILI
Mabinti waliohitimu mafunzo ya ushonaji nguo katika Kituo kilichopo mtaa wa Mwinamila
Kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga (AGAPE TAILORING CENTER), wameaswa kuunda
kikundi chao cha umoja, ambacho kitawasaidia kupata mikopo kwa haraka asilimia
Tano za vijana, fedha ambazo zitawapatia mitaji.
Hayo yalizungumza
Februari 23, 2018 na Ofisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya manispaa ya
Shinyanga Mwanamsiu Dosi, ambaye alikuwa mgeni Rasmi kwenye mahafari ya Tatu ya
kuhitimu wanafunzi 18 wa kituo hicho cha ushonaji nguo Agape.
Alisema ili mabinti hao wapate kufanikiwa katika kuendeleza ujuzi wao na kujikwamua kimaisha,
wanatakiwa waunde kikundi chao cha uzalishaji mali kupitia ujuzi wao wa kushona
nguo, jambo ambalo litawasaidia kupata mikopo ya vijana ya halmashauri asilimia
Tano kwa urahisi, na hatimaye kukuza mitaji yao na kuendesha maisha bila
wasiwasi.
“Mtakapojiunga
kwenye kikundi chenu cha Ujasiriamali, kwa kuwa mimi ndio Ofisa maendeleo hivyo
nitawapa kipaumbele kupata mkopo wa asilimia zile tano za vijana, ilimpate
mitaji na kuendesha maisha yenu bila ya kuwa tegemezi tena na kuepukana na
changamoto za kupewa mimba za utotoni na hata kuambukizwa VVU,”alisema.
Aliongeza kwa
kutoa ahadi ya kuwafungulia akaunti benki kwa vikundi vitatu kila kikundi
Shilingi 50,000, na kumwagiza Ofisa
mtendaji wa Kata hiyo ya Ngokolo mahari
kilipo chuo hicho, awasaidie mabinti hao kuwaunga kwenye vikundi, kwa kufuata
taratibu zote iliwapate kukopesheka kwa uharaka .
Naye mkuu wa
kituo hicho cha ushonaji Nguo Yohana Munisa, ambaye pia ni mwenyekiti wa mtaa
wa Mwinamila Kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga, alisema chuo hicho
alikianzisha mwaka 2016, mara baada ya kuona mabinti wengi kwenye mtaa huo
hawana kazi, na wengine kupewa mimba za utotoni ndipo akaamua kunzisha chuo
hicho cha ushonaji nguo na kufadhiliwa na Shirika la Agape.
Nao Mabinti
waliohitimu mafunzo hayo ambao wengi wao ni wafanyakazi wa ndani, waathirika wa
ndoa za utotoni,pamoja na kuishi mazingira hatarishi akiwamo Rebeka Emmanuel,
alisema mafunzo hayo ya ushonaji nguo bila malipo yata kuwa msaada mkubwa kwao
kimaisha pamoja na kutunza watoto wao.
TAZAMA HABARI PICHA HAPA CHINI
Ofisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Mwanamsiu Dosi, akilipongeza Shirika la Agape kwa kuendelea kushirikiana na Serikali kutatua baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili mabinti wa Kike, hususani katika suala la kurudisha ndoto zao ambazo zilikuwa zimepotea, pamoja na kupinga suala la mimba na ndoa za utotoni, na mabinti ambao tayari ni waathirika wa vitendo hivyo kwa kuwachukua na kuwapatia elimu ya mafunzo mbalimbali, na wengine kuwasomesha masomo ya sekondari na kutimiza ndoto zao zilizotaka kuzimwa.
Mkuu wa
kituo hicho cha ushonaji Nguo Yohana Munisa, ambaye pia ni mwenyekiti wa mtaa
wa Mwinamila Kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga, akizungumza kwenye mahafari hayo alisema kituo hicho
alikianzisha mwaka 2016, mara baada ya kuona mabinti wengi kwenye mtaa huo
hawana kazi, na wengine kupewa mimba za utotoni na kutumikishwa kazi za ndani kwenye majumba ya watu, na baadhi yao kunyanyasika kutoka kwa waajiri wao, ndipo akaamua kunzisha chuo
hicho cha ushonaji nguo na kufadhiliwa na Shirika la Agape kwa kupewa vyerehani 25.
Mwanafunzi Groly Mansury akisoma Risala ya kuhitimu mafunzo hayo ya ushonaji nguo, alisema walianza wakiwa wanafunzi 30 ambao wengi wao ni wafanyakazi za ndani kwenye majumba ya watu, waathirika wa mimba na ndoa za utotoni, kuishi mazingira Magumu, na wamefanikiwa kuhitimu wakiwa 18, ambapo wengine walikwama kutokana na kuzuiwa na waajiri wao kusoma na kuambulia kupewa kazi nyingi na hatimaye kuacha mafunzo.
Pia alitoa wito kwa wadau wa maendeleo wajitokeze kuwasaidia changamoto zinazokikabili kituo hicho cha ushonaji nguo kwa kuwajengea madarasa, na hasa kwa wanafunzi wanaobaki pamoja na kuwapatia vifaa vya kujifunzia vyerehani, sambamba na wao ambao wameshahitimu mafunzo hayo ikiwa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vyerehani vya kuanzia kazi .
Mkurugenzi wa Shirika la Agape mjini Shinyanga Bw, John Myola ambaye ndiye mfadhili mkuu wa kituo hicho cha ushonaji nguo, akizungumza kwenye mahafari hayo aliwataka mabinti hao kuzingatia Nasaha za mgeni Rasmi za kwenda kuunda kikundi, ambacho kitawasaidia kufanya kazi kwa umoja na hatimaye kufanikiwa, huku akitoa ahadi ya kuwa patia Shilingi 100,000 pamoja na vyerehani Vitano vya kuanzia kazi, pamoja na kuungwa mkono na mdau kutoka Docta with Africa ambao nao walitoa Shilingi 150,000.
Wahitimu wa mafunzo ya ushonaji nguo wakisikiliza kwa makini Nasaha mbalimbali kutoka kwa viongozi walioalikwa kwenye mahafari yao, na kusisitizwa kuunda kikundi ambacho kitakuwa msaada mkubwa kwao kuweza kupewa mikopo.
Wahitimu wakiendelea kusikiliza Nasaha za viongozi mbalimbali, na kusisitizwa pia kuendeleza ujuzi huo walioupata na siyo kurudi kule walipotoka na kujikuta wakiambulia kupewa ujauzito na hata kupata maabukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi VVU.
Wahitimu wakitoa burudani ya kuimba nyimbo yenye ujumbe mbalimbali .
Wanafunzi wapya wa mafunzo hayo ya ushonaji nguo nao wakiwa kwenye mahafari hayo, na kusikiliza Nasaha za viongozi mbalimbali waliofika kwenye sherehe hiyo, kuwa wazingatie sana mafunzo hayo ambayo ndiyo yatakuwa mkombozi katika maisha yao, ambayo yatawapatia kipato na kuendesha maisha yao.
Muhitimu wa mafunzo ya ushonaji nguo Catherine Mussa, akionesha mtindo wa vazi la ki Nigeria ambalo ameshona yeye mwenyewe kwa mikono yake.
Wahitimu wakionesha mitindo ya mavazi mbalimbali ambayo wameshona wenyewe kwa mikono yao.
Wahitimu wakiimba Shairi
Wahitimu wakicheza Ngoma za Asili.
Muhitimu Catherine Mussa, akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo ya ushonaji nguo kutoka kwa mgeni Rasmi Ofisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Mwanamsiu Dosi.
Muhitimu Veronica Abel ,akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo ya ushonaji nguo kutoka kwa mgeni Rasmi Ofisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Mwanamsiu Dosi.
Muhitimu wa mafunzo ya ushonaji nguo Catherine Mussa, akionyesha furaha ya kupokea cheti mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo ambayo ana imani yatarudisha ndoto zake za kuwa na maisha yake ya kujitegemea, na siyo kuwa tegemezi tena ambaye ni mfayakazi wa ndani, akipoke cheti hicho kutoka kwa mgeni Rasmi Ofisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Mwanamsiu Dosi.
Mgeni Rasmi kwenye mahafari ya wanafunzi waliohitimu mafunzo ya ushonaji nguo (Katikati) Mwanamsiu Dosi ambaye ni Ofisa maendeleo ya jamii wa halmshauri ya manispaa ya Shinyanga, akitoa burudani kwenye sherehe hiyo akicheza nyimbo.
Wahitimu nao hawakuwa nyuma wakitoa burudani kwa kucheza nyimbo mbalimbali Stly ya Kwaito, wakiongozwa na msanii Samson Mtesigwa, nyimbo yenye ujumbe muache mtoto wa kike asome shule.
Wanafunzi wapya wa mafunzo hayo ya ushonaji nguo nao wakitoa burudani kwenye mahafari ya kuwaaga dada zao.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Agape wakifurahi Jambo kwenye mahafari hayo ya kuwaaga wanafunzi 18 waiohitimu mafunzo ya ushonaji guo.
Wahitimu wa mafunzo ya ushonaji nguo wakiwa katika Picha ya Pamoja na wafanyakzi wa Shirika la Agape, na walimu wao wa mafunzo hayo ya ushonaji nguo.
Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa gazeti la Nipashe Shinyanga.