SHIRIKA LA AGAPE NA KIWOHEDE WAZINDUA MRADI WA AFYA YA UZAZI NA UJINSIA KWA VIJANA UTAKAOTEKELEZWA SHINYANGA NA KAHAMA
Soma habari kamili
Mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Shinyanga Agape na Kiwohede ambayo yanajihusisha na shughuli za kutetea haki za watoto, wamezindua mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana, ambao utakuwa ukitoa elimu y a kiafya kwa vijana waliopo mashuleni na majumbani, kuacha tabia ya kujihusisha na mapenzi katika umri mdogo.
Shirika la Agape kwenye mradi huo litatekeleza kwenye Kata ya Busanda Shinyanga vijijini, ambapo Kiwohede wao watakuwa katika Kata ya Zogomela halmashauri ya Kahama mji, ambapo mradi huo utadumu mwaka mmoja na nusu kuanzia june (2018) hadi June (2019) ,wenye thamani ya Shilingi Milioni 142 kwa ufadhili wa Shirika la SIDA kutoka nchini Sweeden.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola , alisema mashirika hayo mawili yamekuwa yakifanya kazi za aina moja za kutetea haki za watoto na kuwalinda, ambapo kwa sasa wamepata ufadhili wa kutekeleza mradi huo wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana, na kutarajia kuleta matokeo chanya kwao iliwapate kutimiza ndoto zao.
“Mradi huu utakuwa mkombozi kwa vijana wetu hasa wanafunzi wa kike katika kuhakikisha wanatimiza ndoto zao na kuacha kujiingiza kwenye masuala ya kimapenzi katika umri mdogo, ambayo yamekuwa yakizima malengo yao na kuhatarisha afya zao sababu via vyao vya uzazi vinakuwa bado havija komaa,”alisema Myola.
Naye mgeni Rasmi kwenye uzinduzi wa mradi huo Ofisa ustawi wa jamii mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo, akimwakilisha Katibu tawala wa mkoa huo Albert Msovela, alipongeza mashirika hayo kwa kuisaidia Serikali kutatua changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwakabili vijana hususani wa jinsia ya kike.
Alisema kwa mujibu wa sensa ya mwaka (2012 )Tanzania ina vijana 625,000 , na Robo tatu ya wasichana huzaa kabla ya kufikia umri wa miaka 20, na katika mkoa wa Shinyanga asilimia 59 ya wasichana walio na umri kati ya miaka (15-19) wanakuwa tayari wameshaolewa.
Aliongeza kuwa asilimia 33 ya wasichana walio na umri wa miaka (15-19) tayari wanakuwa na mimba ama kuzaa watoto wenzao, jambo ambalo ni hatari kwa afya zao, ambapo wanaweza kupoteza maisha wakati wa kujifungua ama kuharibu kabisa via vyao vya uzazi.
Aidha kufuatia hali hiyo aliyataka mashirika hayo kutoa elimu zaidi kwa vijana na jamii kwa ujumla, juu ya madhara ya kiafya kwa vijana kujihusisha na mapenzi katika umri mdogo, pamoja na wazazi kuacha tabia ya kuwaodhesha ndoa za utotoni, ikiwa via vyao vya uzazi vinakuwa bado havija komaa.
Nao maofisa miradi wa mashirika hayo mawili Agape lucy Maganga, na Kihowede Amosi Juma, kwa nyakati tofauti walisema mradi huo wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana ,utatekelezwa kwa njia mbalimbali ili kufikisha ujumbe wa madhara ya kiafya kwao pale wanapojihusisha na mapenzi katika umri mdogo.
Walisema watatumia njia za mabonanza ya michezo, mijadala ya wanafunzi, Cinema ambazo zitakuwa zikionyesha madhara ya kufanya mapenzi katika umri mdogo, ngoma za asili, matembezi ya Kaya hadi Kaya ambayo yatakuwa yakihusisha mazungumzo ya vijana na wazazi ili kutokomeza vitendo vya mapenzi katika umri mdogo.
Pia walisema elimu hiyo ya afya ya uzazi itakuwa ikitolewa na walimu walezi, viongozi wa kijamii ambao watapewa mafunzo kwanza, na watakuwa wakishirikiana na wahudumu wa afya pamoja na maofisa maendeleo ambao wao tayari ni wataalamu wa masuala hayo.
TAZAMA MATUKIO YA PICHA HAPA CHINI

Mgeni Rasmi wapili kutoka mkono wa kushoto Lidya Kwesigabo ambaye ni Ofisa Ustawi wa jamii mkoa wa Shinyanga akiwa amebeba vitabu vyenye mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana ambao utatekeleza kwenye Kata mbili mkoani humo za Usanda Shinyanga vijijini na Zogomela Kahama na utadumu ndani ya Mwaka mmoja na Nusu, huku Wakwanza mkono wa Kushoto ni Ofisa mradi huo kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga na wakwanza mkono wa Kulia ni Ofisa mradi huo kutoka Shirika la Kihowede Amosi Juma akifuatiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola.

Mkrugenzi wa Shirika la Agape John Myola akielezea namna mradi huo utakavyo kuwa na tija kwa vijana ambao utawasidia kutimiza ndoto zao, pamoja na kutokemeza mimba na ndoa za utotoni, sanjari na kuwaepusha vijana kupata maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi VVU ,kutokana na kuacha kufanya mapenzi katika umri mdogo.

Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mradi huo wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana Lidya Kwesigabo ambaye ni Ofisa ustawi wa jamii mkoa wa Shinyanga akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo aliyataka mashirika hayo pia yakaunde clabu za vijana mashuleni ambazo zitasaidia kuendeleza elimu hiyo ya afya ya uzazi pale mradi utakapo koma kufanya kazi.

Ofisa mradi huo kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga, akiwasilisha namna mradi utakavyo fanya kazi kwenye Kata hiyo ya Usanda Shinyanga vijijini, alisema wanatarajia kufikia wanafunzi 1,500 wa shule zote za msingi na sekondari waliokati ya umri wa miaka (10- 18), vijana walionje ya shule kati ya miaka (19 -24), 100, wanajamii 8,000 pamoja na viongozi a kijamii 50,ambao watapatiwa elimu hiyo ya afya ya uzazi na ujinsia.

Ofisa mradi huo kutoka Shirika la kihowede Amosi Juma. akiwasilisha namna mradi huo utakavyo fanya kazi katika Kata ya Zogomela wilayani Kahama ,kuwa watakuwa wakitumia mbinu za kutoa elimu hiyo ya afya ya uzazi na ujinsia kupitia mabonanza ya michezo, ngoma za asili, Cinema, mijadala,mikutano, matembezi ya Kaya kwa Kaya , kuunda vilabu vya wanafunzi pamoja na kwenda nao kwenye bunge la jamhuri wa muungano wa Tanzania, kuwasilisha mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971, ambayo imekuwa mwiba kwenye ndoa za utoto ambayo inaruhusu mtoto aliyechini ya umri wa miaka 18 kuolewa kwa ridhaa ya wazazi au mahakama, ambayo ina kinzana na sheria ya mtoto ya mwaka 2009 ambayo ina mtaka mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18 ahudhulie shule.

Ofisa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga Groy Mbia akichangia mada kwenye uzinduzi wa mradi huo wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana , aliyataka mashirika hayo pia kuhusisha elimu hiyo kwenye mabaraza ya vijana, ambayo nayo yatakuwa mabarozi wazuri kusambaza elimu hiyo, na kutokomeza vitendo vya wanafunzi kufanya mapenzi katika umri mdogo.

Mdau wa masuala ya afya kutoka Shirika la Thubutu Afrika Initiative Jonathani Kifunda, akichangia mada kwenye uzinduzi wa mradi huo, alilipongeza pia shirika hilo la Agape kwa kufanikisha kujenga chumba cha kujistili wanafunzi wa kike pindi wanapokuwa kwenye hedhi katika shule ya msingi Shingida, ambapo na yeye kama mdau aliahidi kuchangia upatikanji wa Pedi kwa wanafunzi Shuleni hapo.

Mwanafunzi Jackline Ghuba kutoka shule ya Sekondari Isunuka Kahama kidato cha Nne akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo, aliwataka wazazi kuacha tabia ya kuwa chanzo cha watoto wao kujiingiza kwenye masuala ya mapenzi katika umri mdogo, kwa kuwafanya vitega uchumi vyao, bali wajitume kufanya kazi za kuwaingizia vipato, pamoja na kuwatimizia mahitaji yao yote ya shule.

Mtendaji wa Kata ya Usanda Emmanuel Maduhu ,mahari ambapo mradi huo wa afya ya uzazi na ujinsia unatekelezwa kwenye eneo lake, alilipongeza Shirika hilo kwa kuzindua mradi huo ambapo utasaidia kutokomeza tatizo la mimba na ndoa za utotoni.

Diwani wa Kata ya Usanda Forest Nkole akichangia mada kwenye uzinduzi wa mradi huo ambao utatekelezwa kwenye Kata yake ambao utasaidia kutokomeza tatizo la mimba na ndoa utotoni pamoja na kuondoa suala la ukatili wa kijinsia.

Wadau wa afya wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana.

wadau wakiendelea kuchukua mawili matatu kwenye uzinduzi wa mradi huo wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana.

Wadau wakiendelea na Kikao cha uzinduzi wa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia.
Ofisa maendeleo ya jamii Deusi Mhoja mkono wa kushoto kutoka halmashauri ya Shinyanga vijijini akiwa na Ofisa mtendaji wa Kata ya Usanda Emmanuel Maduhu, kwenye uzinduzi wa mradi huo wa afya ya uzazi na ujinsia.

Wadau wa masuala ya afya wakiendelea na kikao cha uzinduzi wa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana.

Wadu wakisikiliza kwa makini namna mradi huo wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana utakavyofanya kazi na kuwa mkombozi wa vijana kutimiza ndoto zao na kuwaokoa kupata madhara ya afya ya uzazi pale wanapojihusisha na mapenzi katika umri mdogo.

wadau wakiendelea kusikiliza namna mradi huo utakavyo kuwa mkombozi kwa vijana, ambao pia utatokomeza vitendo vya mimba na ndoa za utotoni kwa wanafunzi wa kike.

Wadau wa masuala ya afya wakiendelea na Kikao cha uzinduzi wa mradi huo wa afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape na Kiwohede.

Keki ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kusheherekea mradi huo wa afya ya uzazi (ASRHR) ambao utakuwa mkombozi kwa vijana.

Mgeni Rasmi Lidya Kwesigabo ambaye ni Ofisa ustawi wa jamii mkoa wa Shinyanga akikata Keki na wadau wa afya wakiwamo na wanafunzi kuashiria mradi huo wa afya ya uzazi utakuwa na tija na kuwakomboa vijana hasa wa kike hususani kwenye kunusuru afya zao.

Diwani wa Kata ya Usanda Forest Nkole akila keki kwenye uzinduzi wa mradi huo ambao utadumu kwenye Kata yake ndani ya mwaka mmoja na Nusu.
Ofisa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga Groy Mbia akilishwa keki na mwanafunzi kwenye ufunguzi wa mradi huo wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana.

Ofisa maendeleo ya jamii Shinyanga vijijini naye kila keki kwenye uzinduzi huo wa mradi.

Ofisa mradi huo wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga naye akila kike ya kuuzindua rasmi mradi huo kuanza kufanya kazi kwenye Kata ya Usanda Shinyanga Vijijini ndani ya mwaka mmoja na Nusu kuanzia June 2018 hadi june 2019.
Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola naye akila Keki kwenye uzinduzi wa mradi huo wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana.

Wafadhili wa mradi huo kutoka shirika la SIDA nao wakila Keki kwenye uzinduzi wa mradi huo wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana.

Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola akiteta jambo na mageni Rasmi Ofisa ustawi wa jamii mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo kwenye uzinduzi wa mradi huo wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana.

Wadu wa masuala ya afya ya uzazi wakifurahia kwa pamoja uzinduzi wa mradi huo.
Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola akionyesha furaha kubwa kwenye uzinduzi wa mradi huo wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana.

Wanafunzi wakiungana kwa pamoja na wadau wa masuala ya afya kufurahia uzinduzi wa mradi huo na kupiga picha ya pamoja .

Mfadhili wa mradi huo kutoka shirika la SIDA ambaye hakutaka jina lake liandikwe kwenye vyombo vya habari. mara baada ya kusikiliza maoni ya wadau ambao walitaka mradi huo upanuliwe kufanya kazi mkoani Shinyanga na usikomee tu kwenye Kata za Usanda na Zongomela, na kuwa hakikishia kuwa endapo matokea yatakuwa mazuri kwenye mradi huo, wapo tayari tena kutoa ufadhili kwenye Kata zingine ambazo zinachangamoto hiyo, na kubainisha kuwa lengo kuu la elimu hiyo ya afya ya uzazi na ujinsia ni kutokomeza mimba na ndoa za utotoni. ili mtoto wa kike apate kusoma.

Ofisa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga Grory Mbia akifunga kikao cha uzinduzi huo wa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia ,ambacho kilifanyika kwenye Hoteli ya Virgmark mjini Shinyanga .
Na Marco Maduhu ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe