TGNP YAKUTANISHA WARAGABISHI KUTOKA MIKOA MITANO KUPANGA MIKAKATI YA KUTATUA MATATIZO NDANI YA JAMII
Mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP) ambao unafanya shughuli za kutatua matatizo mbalimbali ndani ya jamii, pamoja na kuleta usawa wa kijinsia umekutanisha Waraghbishi kutoka mikoa mitano, ambao watakuwa kichocheo cha kuibua matatizo ndani ya jamii pamoja na kuyatafutia ufumbuzi
Waraghbishi hao wametoka katika mikoa ya Shinyanga, Morogoro, Mbeya ,Kigoma na Dar es salaamu, ambao wanajengewa uwezo namna ya kuibua matatizo yanayowakabili wananchi pamoja na kuyatafutia ufumbuzi ,ili jamii ipate kuishi maisha mazuri, sambamba na kukuza uchumi wa kaya zao pamoja na kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Mafunzo ya waraghbishi hao yanaendeshwa jijini Dare es salaamu kwa muda wa siku tano kuanzia Marchi 3 hadi7, kwa kuwakutanisha pia waragabishi wazoefu kutoka Kata za Mwadui Luhumbo (Kishapu),Mwandele( Mbeya), Bwakila chini( Morogoro), pamoja na Kata mpya ambazo ni Itele( Mbeya), Bunambiu(Kishapu), Mgazi( Morogoro) pamoja na Nyansa(Kigoma) ilikubadilisha uzoefu wa utendaji kazi.
Afisa Tambuzi na Utafiti kutoka TGNP Mareen Mboka, akielezea malengo ya semina hiyo ya Uraghbishi kuwa ni kujifunza mbinu mbalimbali za kuibua na kutatua matatizo ndani ya jamii hususani wale waliopembezoni mwa miji mfano masuala ya maji,afya, elimu,pamoja na kuondoa ukatili wa kijinsia.
Afisa programu ujenzi wa nguvu ya pamoja kutoka TGNP Deogratius Temba, alisema mtandao huo ulianzishwa mwaka 1993 na una miaka 25 sasa, ambao kazi yake ni utetezi wa usawa wa kijinsia na haki za wanawake kuanzia ngazi ya kijiji hadi ngazi za juu
Waraghbishi wakiendelea na mafunzo ya siku tano, wakijengewa uwezo namna ya kuibua matatizo ndani ya jamii pamoja na kuyatafutia ufumbuzi.
Mraghbishi Mwezeshaji Mary Nsemwa akitoa somo la MUKTADHA, ambalo linawajengea uwezo waragabishi hao kutoka mikoa hiyo mitano ,namna ya kutambua matatizo ya Kimataifa,Kitaifa hadi ngazi za jamii,Jinsi yanavyoleta athari yakiwamo masuala ya Siasa,,Uchumi,Kijamii na kisha kutoa zoezi(Asengment) kwa wana darasa hao waragabishi kutambua athari za matatizo yao.
Waraghbishi wanadarasa wakiendelea na majadiriano juu ya zoezi hilo la kutambua Matatizo ya MUKTADHA kuanzia ngazi ya Kimataifa,Kitaifa hadi Kijamii.
Vikundi vikiendelea na majadiliano.
Vikundi vikiendelea na majadiliano juu ya swali la MUKTADHA.
Wanakikundi wakiwasilisha majibu juu ya Swali la MUKTADHA Jinsi linavyo athiri kuanzia ngazi ya Kimataifa ,Kitaifa hadi Kijamii, ambapo mmoja wa wanakikundi hao MathaCharles akiwasilisha hoja zao kuwa Kunapokuwa na migogoro ya kisiasa ngazi na Kimatifa huathiri hadi nchi za Kitaifa na ngazi ya jamii , pia kushuka kwa thamani ya pesa napo huathiri nchi za kitaifa hadi ngazi za jamii sababu ya malighafi kukosa soko zuri hususani mazao na kusababisha uchumi wa nchini na jamii kushuka, pia kukithiri kwa viwanda navyo ni tatizo na kusababisha ukame na kuleta athari za janga la njaa ndani ya jamii.
Juma Ngwalu ni mwanakikundi namba Nne naye alitoa maelezo kama ya kikundi cha namba moja ambapo mawazo yote ya wanakikundi yali landana juu ya Swali la Muktadha huo, ambao pia ni mpango wa maendeleo wa kitaifa ndani ya miaka mitano kuanzia (2016 -21).
Mraghbishi Mwezeshaji Annagrace Rwehumbiza akitoa somo la mbinu na zana za uragabishi katika kuibua masuala ndani ya jamii.
Waraghbishi wana darasa wakiendelea kusikiliza elimu ya kujengewa uwezo.
Mraghbishi Mwezeshaji Winston Churchill, akitoa somo la dhana ya uragabishi kinadharia na kivitendo,chimbuko,uasisi na kanuni zake, ikihusishwa na dhana ya ukombozi wa wanawake kimapinduzi, na kubainisha kwa lengo kuu la ugarabishi ni kuleta ukombozi katika jamii kwa kutatuliwa matatizo yao ,likiwamo swala la Kiafya ,Uchumi Elimu na Maji.
Waraghbishi wawezeshaji Mary Nsemwa mkono wa kushoto na Annagrace Rwehumbiza mkono wa kulia, wakibadilishana mawazo na kupitia mada mbalimbali ambazo watazitoa kwa waragabishi kutoka mikoa hiyo mitano, "ambapo neno Uragabishi" ni shughuli za kiharakati katika kutafuta ukombozi na kuleta mafanikio ndani ya jamii.