WANANCHI WAPIGWA MARUFUKU KUOA BILA KUTOA TAARIFA KWA SERIKALI YA KIJIJI
Serikali ya kijiji na Kata ya Nsalala Tarafa ya Itwangi Shinyanga vijijini, kimetunga Sheria ya kutokomeza ndoa za utotoni kwa kupiga marufuku kila mwananchi anayetaka kuoa ama kuozesha lazima atoe taarifa kwa uongozi wa kijiji hicho, ndipo wampatie ridhaa ya kufunga pingu hizo za maisha.
Hayo yamebainishwa leo/ March 30 na mwenyekiti wa kijiji cha Nsalala Sandeko Machungo kwenye mdahalo wa kutoa elimu ya kutokomeza masuala ya ukatili wa kijinsia kupitia mitandao ya kijamii, ulioandaliwa na Shirika la Kivulini linalotetea haki za watoto na wanawake kwa ufadhiri wa shirika la OXFAM.
Amesema viongozi wa Serikali hiyo ya kijiji mara baada ya kupata elimu ya ukatili wa kijinsia kupitia mashirika mbalimbali, ndipo wakaona ni vyema wakatunga Sheria ndogo kijijini humo ya kuzuia wananchi kuoa ama kuodhesha bila ya kutoa taarifa kwenye uongozi huo, kwa lengo la kutokomeza tatizo la ndoa za utotoni.
“Kwenye kijiji changu tumetunga sheria hakuna mwananchi kuoa ama kuodhesha bila ya kuuona uongozi wa kijiji, ambapo sisi tutafuatilia taarifa za mtu anayetaka kuolewa kama hayupo chini ya umri wa miaka 18 na siyo mwanafunzi kwa kuangalia cheti cha kuzaliwa ama kadi ya clinik ndipo tunatoa ruhusa,”Amesema Machungo.
Ameongeza Sheria hiyo waliitunga mwaka jana na wananchi wamekuwa wakifanya hivyo, na tangu ianze kufanyakazi hakuna changamoto tena ya ndoa za utotoni kijiji humo wala mimba kwa wanafunzi, ambapo kila mwananchi amekuwa mlinzi wa mwezake na atakaye bainika kwenda kinyume na sheria hiyo kijiji kitamshughulikia.
Naye kaimu ofisa ustawi wa jamii halmashauri ya Shinyanga vijijini Aisha Omari, ameipongeza Serikali ya kijiji hicho kwa kutunga sheria hiyo ndogo, na kutoa wito kwa vijiji vingine kuiga ikiwa suala la kutokomeza mimba na ndoa za utotoni ni juhudi za wanajamii wenyewe.
Kwa upande wake Kaimu Ofisa maendeleo ya jamii halmashauri ya Shinyanga vijijini Deus Mhoja, amesema Serikali pia imejiwekea mikakati ya kutokomeza masuala ya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto, na kutoa takwimu kuwa tatizo la mimba na ndoa za utotoni limepungua kwa asilimia 33 kutoka 59.
Aidha Ofisa miradi kutoka Shirika hilo la Kivulini Yunis Mayengela, amitaka jamii kuachana na masuala ya ukatili wa kijinsia ikiwamo kuodhesha watoto wadogo, vitendo ambavyo vinapaswa kupingwa na kila mwananchi.
Pia katika mdahalo huo masuala ya ukatili wa kijinsia yaliyotajwa kuwa ni Ukatili wa kiuchumi kwa wanawake pale wanapovuna mazao na kuuza wananume huchukua fedha na kutokomea, kubakwa,kupingwa, kutopewa fursa ya kuwa viongozi, kutomiliki ardhi pamoja na wanafunzi kuodheshwa ndoa za utotoni na kukatishwa masomo yao.
Mdahalo huo ulishirikisha wana mabadiliko wa kupinga masuala ya ukatili wa kijinsia kutoka katika Kata za Nyida, Nsalala na Itwangi halmashauri ya Shinyanga vijijini , waandishi wa mitandao ya kijamii( Bloggers) kutoka dar es salaam na Shinyanga,pamoja na watendaji wa vijiji,kata na maofisa maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii.
TAZAMA HABARI PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa kijiji cha Nsalala Sandeko Machungo akizungumza kwenye mdahalo huo wa kupinga ukatili wa kijinsia, na kubainisha kwenye kijiji chake wameshatunga sheria ndogo ya kutokomiza mimba na ndoa za utotoni, ambapo kila mwananchi anayetaka kuoa ama kuodhesha lazima atoe taarifa kwa Serikali ya kijiji.
Rachel Marco akielezea ukatili ambao upo ndani ya jamii kwenye mdahalo huo, kuwa ni ukatili wa kuwaodhesha wanafunzi wa kike ndoa za utotoni walio na umri chini ya miaka 18 na kukatisha ndoto zao.
Monica Simon akielezea masuala ya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii kuwa ni masuala ya kiuchumi, ambapo wanawake kwa asilimia kubwa wao ndio wanakesha mashambani, lakini mwanaume kazi yake ni kuuza mazao na kisha zile pesa kutozifanyia maendeleo, na kwenda kuzifanyia Anasa Centa, pamoja ukatili mwingine wa kubakwa kwa wanawake.
Mery Christopher akichangia mada kwenye mdahalo huo wa kupinga ukatili wa kijinsia, kuwa wanawake kwa asilimia kubwa hasa kwenye kipindi cha mavuno ndipo wanapofanyiwa ukatili wa kiuchumi kwa kutoshirikishwa na waume zao kwenye upangaji wa maendeleo.
Elzabeth Richard Mmoja wa wanamabadiliko akichangia mada kwenye mdahalo huo.
Mtendaji wa kijiji cha Nyida Daudi Lazaro akichangia mada kwenye Mahalo huo wa kupinga ukatili wa kijinsia na kubainisha kuwa vitendo vya mimba na ndoa za utotoni kwa watoto walio na umri chini ya miaka 18 vimepungua sababu ya kutolewa kwa elimu .
James Masunga akichangia mada kwenye mdahalo huo na kubainisha kuwa ukatili ambao upo ndani ya jamii ni matumizi ya nguvu kwa wanaume sababu ya kuendekeza masuala ya mfumo dume.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Welezo Janet Mabula akichangia mada kwenye mdahalo huo, na kubainisha ukatili ambao upo ndani ya jamii kwa sasa ni ukatili wa kiuchumi kwenye masuala ya mauzo ya mavuno, ambapo kesi zimeanza kuwa nyingi sababu ya wanawake kupata elimu na kuamka usingizini, na kumpinga mumewe kutaka kuuza mazao bila ya kumshirikisha , pamoja na ukatili wa kutopeleka watoto wa kike shule .
Wana mabadiliko wakiwa kwenye madahalo wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii.
Mdahalo ukiendelea wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii.
Mtendaji wa kijiji cha Nsalala Jacob Jomanga akichangia mada kwenye mdahalo huo, amebainisha kuwa ukatili mwingine ambao upo ndani ya jamii ni wanawake kutopewa fursa ya kumiliki ardhi, sababu ya wanaume kuhofia siku wakiachana ataikosa ardhi hiyo .
Kaimu Ofisa ustawi wa jamii halmshauri ya Shinyanga vijijini Aisha Omari ameipongeza Serikali ya kijiji Nsalala kwa kutunga sheria hiyo ndogo, na kutoa wito kwa vijiji vingine kuiga ikiwa suala la kutokomeza mimba na ndoa za utotoni ni juhudi za wanajamii wenyewe.
Wana mabadiliko kutoka Kata tatu Nyida, Nsalala na Itwangi wakiwa kwenye mdahalo wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Wana mabadiliko kutoka Kata tatu Nyida, Nsalala na Itwangi wakiwa kwenye mdahalo wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Wanambadiliko kutoka Kata tatu Nyida, Nsalala na Itwangi wakiwa kwenye mdahalo wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Wana mabadiliko wakiwa kwenye mdahalo.
Ofisa maendeleo ya jamii halmashauri ya Shinyanga vijijini Deus Mhoja, akizungumza kwenye mdahalo huo amesema Serikali pia imejiwekea mikakati ya kutokomeza masuala ya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto, na kutoa takwimu kuwa tatizo la mimba na ndoa za utotoni mkoani Shinyanga limepungua kwa asilimia 33 kutoka 59.
Ofisa miradi kutoka Shirika hilo la Kivulini Yunis Mayengela, ameitaka jamii kuachana na masuala ya ukatili wa kijinsia ikiwamo kuodhesha watoto wadogo, vitendo ambavyo vinapaswa kupingwa na kila mwananchi.
Wanamabadiliko wakiendelea na mdahalo wa kupinga ukatili wa kijinsia huku wakichukua mawili matatu ambayo watayafanyia kazi, na kuwa mabarozi kwa wenzao ilikuondokana na mfumo kandamizi.
Wanamabadiliko wakiwaa kwenye mdahalo wa kupinga ukatili wa kijinsia ndani ya jamii.
Wanamabadiliko wakiwa kwenye mdahalo wa kupinga ukatili wa kijinsia ndani ya jamii.
Baadhi ya waandishi wa habari za mitandaoni( Bloggers) kutoka Jijini Dar es salaam wakiwa kwenye mdahalo huo na kusikiliza namna ukatili wa kijinsia ulivyo ndani ya jamii mkoani Shinyanga, na kisha kutoa elimu ya kupinga vitendo hivyo kupitia mitandao.
Ofisa miradi kutoka Shirika la Kivulini Yunis Mayegela akifurahia jambo wakati wana mabadiliko hao wakichangia mada, hasa kwa suala la wanaume kufanyiwa ukatili ambao wao wamebainisha ukatili ambao hufanyiwa ni kunyimwa tendo la ndoa .
Wana mabadiliko wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari za mitandaoni (Bloggers) kutoka Jijini Dar es salaam, wakiwamo na wenyeviti wa vijiji ,watendaji na maafisa maendeleo na ustawi wa jamii.
Na Marco Maduhu ambaye pia ni mwandishi wa gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.