NAIBU WAZIRI APIGA MARUFUKU MADAWA YA SERIKALI KUUZWA KWENYE MADUKA BINAFSI YA DAWA ,AHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA NA CHF ILIYOBORESHWA
Naibu waziri wa afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile, akiwa katika bohari ya dawa kwenye kituo cha afya Kata ya Kambarage mjini Shinyanga, na kupiga marufuku dawa hizo za Serikali kuuzwa kwenye maduka ya dawa ya watu binafsi, ambapo hapo awali kwenye kituo hicho cha afya kulikuwa na tabia hiyo kwa baadhi ya wauguzi kuuza madawa ya Serikali kwenye madukta binafsi tabia ambayo ilikomeshwa na mkuu wa wilaya hiyo Josephine Matiro.
SOMA HABARI KAMILI
Naibu waziri wa afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile, amepiga
marufuku madawa ya Serikali kuonekana yakiuzwa kwenye maduka ya watu binafsi,
ikiwa Serikali haitaki kuingia kwenye matatizo ya uhaba wa dawa kwenye sehemu
zake za kutolewa huduma ya afya.
Alisema katika bajeti
ya mwaka wa fedha (2017-18) Serikali kwenye bajeti ya wizara hiyo ya afya
imetenga jumla ya Shilingi Bilioni 270, tofauti na mwaka wa fedha (2015-16)
ambapo zilikuwa Bilioni 30 zaidi ya mara Tisa yake, hivyo hawatarajii kusikia
sehemu za kutolewa huduma zake za kiafya kuwa zinaupungufu wa madawa.
Dkt Ndugulile amepiga
marufuku hiyo februari 21 mwaka huu alipokuwa katika ziara yake ya kikazi mkoani
Shinyanga, ya kukagua shughuli za huduma za afya zinavyotolewa kwa wananchi,
pamoja na kutoa hamasa kwa jamii kujiunga na Bima ya afya ya jamii CHF
iliyoboreshwa.
Akiwa katika hospitali
ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga na Kituo cha Afya cha Kambarage manispaa ya
Shinyanga na kukagua bohari za madawa,
alitoa tahadhari kwa wauguzi kuwa ni
marufuku dawa hizo za Serikali kukutwa zinauzwa kwenye maduka ya watu binafsi,
na ikibainika watachukuliwa hatua kali.
“Serikali ya awamu hii
ya tano imedhamilia kuboresha huduma za afya hapa nchini, na ndio maana hata
bajeti yake imetolewa ni ya fedha nyingi, hivyo sisi kama wizara husika hatutarajii
kuwepo na mapungufu ya dawa kwenye sehemu za huduma za afya,”alisema.
Pia aliwataka wananchi
kujiunga na Bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, ilikuwa na uhakika wa kupata matibabu hasa
pale watakapo ugua na kukutwa hawana pesa, ambapo wataweza kutibiwa kwa shilingi
hiyo 10,000 na hatimaye kuokoa maisha yake.
Naye kiongozi wa
mradi wa maendeleo ya tuimarishe afya (HPSS) kutoka makao mkuu Dodoma Prof
Manoris Meshack, alisema mradi huo wa Bima ya afya ya jamii CHF ulianza mwaka
2011 mkoani Dodoma, na baada ya kufanya vizuri
mwaka 2015 ukaongezwa katika mikoa miwili ya Shinyanga na Morogoro.
Alitaja takwimu
za Kaya katika mikoa hiyo Mitatu zilizojiunga na CHF iliyoboreshwa hadi sasa
kuwa ni 318,334 sawa na asilimia 26 kati ya Kaya 1,220,413, na hadi kufikia
Dicemba 2017 kupitia uandikishaji wa wanachma wamekusanya shilingi Bilioni
7,027,605,547. ambapo Shilingi bilioni 2,435,194,000 ni malipo ya tele tele.
Nao baadhi ya
wazee Kati ya Kumi wasiojiweza ambao
walikatiwa Bima hiyo ya Afya ya jamii CHF iliyoboreshwa na Naibu Waziri huyo,
Mohamed Mkumbola na Regina Kulwa waliipongeza Serikali kwa kujali makundi hayo
maalumu, na kuomba wazee wote wakatiwe Bima hiyo pamoja na kuendelea kutoa elimu
kwa wananchi wajiunge.
SOMA PIA HABARI PICHA HAPA CHINI
Naibu waziri wa afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile, akiwa ameshika kopo la dawa katika bohari ya dawa kwenye kituo cha afya Kambarage mjini Shinyanga, huku akionyesha Nembo ya dawa za Serikali MSD Kuwa hazitakiwa kutoka nje ya hospitali za Serikali.
Naibu waziri wa afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile, akimsalimia mgonjwa katika kituo cha Afya Kambarage mjini Shinyanga, huku akiangalia dawa alizopewa mgonjwa, na kupiga marufuku wagonjwa kuambiwa dawa hakuna na kwenda kununua kwenye maduka ya dawa ya watu binafsi.
Naibu waziri wa afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile, akikagua chumba cha upasuaji katika kituo cha afya Kambarage mjini Shinyanga, na kuagiza jengo hilo lifanyiwe marekebisho ilikwendana na hadhi ya chumba cha upasuaji, sababu hali ridhishi kwendana na huduma ambayo itakuwa ikitolewa.
Naibu waziri wa afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile, akitoka kwenye jengo la chumba hicho cha upasuaji katika Kituo cha afya Kata ya Kambarage mjini Shinyanga, na kuacha maagizo lifanywe marekebisho.
Naibu waziri wa afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile, akihamasisha wananchi wa Kata ya Kambarage mjini Shinyanga kujiunga na Bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, ilikuwa na uhakika wa kupata matibabu pale watakapo patwa na ugonjwa gafla harafu hawana pesa, ambapo bima hiyo itasaidia kupata tiba na kuokoa maisha yao.
Naibu waziri wa afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile, akitoa hamasa kwa wananchi kwa vitendo juu ya ukataji wa Bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, na kukata Bima hiyo papohapo, na hapo akipigwa picha na Ofisa uandikishaji CHF Kata hiyo ya Kambarage Marry Budigila.
Naibu waziri wa afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile, akijaza taarifa zake wakati akiendelea na zoezi la ukataji Bima hiyo ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, na kutoa hamasa kwa wanachi kujiunga nayo huku akikatia watu 10 bima hiyo ambao hawajiwezi wakiwamo wazee.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro naye akitoa hamasa ya wananchi kujiunga na bima hiyo ya Afya CHF iliyoboreshwa, pamoja na kusaidia kuwa unga watu Watano wasiojiweza kwenye Bima hiyo, na kumuunga mkono Naibu waziri kwa kutoa elimu kwa vitendo, huku akiwataka wadau kujitokeza kusaidia kukatia Bima hiyo watu waliokatika makundi maalumu.
Ofisa uandikishaji wa Bima ya afya CHF iliyoboreshwa Jackson Njau, akiendelea na zoezi la kuingiza taarifa kwa wananchi ambao wamejitokeza kujiunga na Bima hiyo ya afya ya jamii.
Naibu waziri wa afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile, akimkabidhi Kadi ya CHF Mzee Mohamed Mkumbola ambaye ni miongoni mwa watu 10 wasiojiweza aliowakatia Bima hiyo.
Naibu waziri wa afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile, akimkabidhi Kadi ya CHF bi Regina Kulwa ambaye ni miongoni mwa watu 10 wasiojiweza aliowakatia Bima hiyo.
Mzee Mohamed Mkumbola akitoa shukrani kwa Naibu waziri huyo kwa kuwakatia Kadi ya bima ya afya wazee wasiojiweza, huku akimuomba kumsaidia kupata madai yake katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga anayodai, mara baada ya kuacha kufanya kazi,ombi ambalo liliahidiwa kushughulikiwa na kukabidhiwa majukumu hayo katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kambarage mjini Shinyanga, wakisikiliza Nasaha kutoka kwa Naibu Waziri wa afya dkt Faustine Ngugulile ,juu ya kujiunga na Bima hiyo ya afya CHF, ambayo itakuwa msaada mkubwa katika kuokoa maisha yao pale watakapopatwa na magonjwa na kukutwa hawana pesa.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kambarage mjini Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa hamasa ya kujiunga na Bima ya CHF iliyoboreshwa, ambapo mtu akikata Shilingi 10,000 yeye na familia yake watu watano watatibiwa kwa mwaka mzima.
Naibu waziri wa afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile Katikati, akiwa katika hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga kuangalia namna huduma za afya zinavyotolewa dhidi ya wananchi, huku upande wa mkono wa kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro, na mkono wa kulia ni mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Geogre Masigati.
Naibu waziri wa afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile, akiangalia huduma ya mfumo wa malipo ya kielectonic kwenye hospitali hiyo ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, na kukuta mfumo huo haufanyi kazi ambapo hapo awali aliambiwa unafanya kazi na kusababisha kuwepo na upotevu wa fedha.
Naibu waziri wa afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile, akiangalia majalada ya wagonjwa na namna wanavyopatiwa huduma za matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Naibu waziri wa afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile, akimsalimia mzazi katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga, na kumuliza maswali juu ya huduma anazo pewa ikiwamo kama aliagizwa kwenda kununua dawa yoyote ama vifaa kwa ajili ya kujifunguli na kupewa majibu kuwa kahudumiwa vizuri na vitu vyote kapewa hapo hospitalini.
Naibu waziri wa afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile, akipitia taarifa ya hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga na kubaini kuna upotevu mkubwa wa pesa, kutokana na kutofanya kazi mfumo wa ukusanyaji pesa kwa njia ya kielectronic na kuagiza ufanyekazi haraka sana.
Baadhi ya wauguzi katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga, wakisikiliza Ujumbe kutoka kwa Naibu waziri wa afya Dkt Faustine Ndugulile, na kusisitizwa watoe tiba vizuri kwa wananchi pamoja na kutoa kauli Nzuri kwa wagonjwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro, akimkaribisha Naibu Waziri wa afya Dkt Faustine Ndugulile kusikiliza taarifa za huduma ya afya kwa wakurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga na Shinyanga vijijini
Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Geofley Mwangulumbi, akisoma taarifa ya huduma ya afya ya mansipaa hiyo, kuwa kuna vituo Viwili vya afya,Zahanati 28 na hakuna tatizo la uhaba wa dawa, na kutaja takwimu za Kaya zilizojiunga na bima ya afya ya jimii CHF kuwa ni Kaya 7,136 sawa na asilimia 21.2 ya kaya zote, na kaya zilizo hai hadi sasa ni 3,781na zinaendelea kupata huduma ya matibabu sawa na asilimia 11.2, ambapo lengo la kitaifa ni kufikia asilimia 30 na kuwataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiunga na bima hiyo ya CHF.
Mkurugenzi wa halmashuari ya Shinyanga vijijini Bakari Kasinyo, akisoma taarifa ya huduma za afya kwenye halmshauri hiyo, amesema kuna vito vya afya Vitano na Zahanati 35 na hakuna tatizo la dawa, na kutaja idadi ya Kaya zilizojiunga na Bima ya CHF iliyoboreshwa, kuwa ni 10,615 Kati ya Kaya 59,321 sawa na asilimia 11.3 ,na kubainisha mkakati ulipo ni kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi kujiunga na Bima hiyo ya CHF.
Kiongozi wa
mradi wa maendeleo ya tuimarishe afya (HPSS) kutoka makao mkuu Dodoma Prof
Manoris Meshack, akisoma taarifa ya mradi huo wa Bima ya afya ya jamii CHF kuwa ulianza mwaka
2011 mkoani Dodoma, na baada ya kufanya vizuri mwaka 2015 ukaongezwa katika mikoa miwili ya Shinyanga
na Morogoro.
Ametaja takwimu
za Kaya katika mikoa hiyo Mitatu zilizojiunga na CHF iliyoboreshwa hadi sasa
kuwa ni 318,334 sawa na asilimia 26 kati ya Kaya 1,220,413 na hadi kufikia Dicemba
2017 kupitia uandikishaji wa wanachma wamekusanya shilingi Bilioni
7,027,605,547. ambapo Shilingi bilioni 2,435,194,000 ni malipo ya tele tele.
Naibu waziri wa afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile mkono wa Kushoto, akiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakikagua Jengo la Hospitali mpya ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga ambayo inajengwa katika Kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa nje wa jengo jipya la hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga .
Na Marco Maduhu ambaye pia ni Mwandishi wa gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga Soma Nipashe kila siku uhabarike na habari za uhakika.