UCHUNGUZI WABAINI MAREHEMU HAKUTOBOLEWA TUMBO, AZIKWA KWA MARA YA PILI
Mjomba
wa marehemu Sued Mussa, akizungumzia namna kifo cha mpwa wake Ashura Shabani kilivyo msikitisha .
Marehemu Ashura
Shabani (30) ambaye amefukuliwa leo alipokuwa amezikwa katika makabuli ya
Chamaguha manispaa ya Shinyanga, baada ya
kuwepo na mashaka kuwa alitobolewa Tumbo na Madaktari wa Bugando Jijini Mwanza
na kuondolewa baadhi ya viungo vyake vya ndani, uchunguzi wa mwili huo umebainika
marehemu hakutobolewa tumbo bali alichanwa Paja kwaajili ya kuwekwa dawa ili
asihalibike.
Akizungumza na
Shinyanga News Blog Mjomba wa marehemu Sued Mussa, ambaye alikuwa miongoni mwa
walioufanyia uchunguzi mwili huo wa mpwa wake, amesema baada ya kufanya
uchunguzi wa kina hawakukuta Tundu lolote
tumboni kama ilivyodaiwa awali na akina mama ambao waliuosha mwili huo.
Amesema mara
baada ya kubaini hakufanyiwa unyama huo, waliuchukua mwili wa marehemu na
kuuzika tena kwa mara ya pili, huku akitoa lawama kwa madaktari wa Bugando kwa
kumtoa kwenye hospitali hiyo na kumpeleka kwenye hospitali zao binafsi na kufia
huko.
Aidha jana
katika mtaa huo wa Chamaguha kuliibuka Sinto fahamu mara baada ya kuwepo na uvumi
wa marehemu kutolewa viungo vyake vya mwili ndani ya tumbo, kwa madai hakuwa na
malazi ya tumbo ambapo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la Shingo.
SOMA STORY YA
AWALI HAPA CHINI BAADA YA SINTO FAHAMU HIYO
.
Mwili
wa
marehemu Ashura Shabani (30) aliyekuwa mkazi wa Kata ya Chamaguha
manispaa ya
Shinyanga, unatarajiwa kufukuliwa baada
ya kuwepo na mashaka juu ya mwili wake kuwepo na tundu pembeni mwa tumbo
na huenda kuna baadhi ya viungo vyake kutolewa,kwa madai alifariki kwa
ugonjwa wa shingo (Goita) wakati akifanyiwa upasuaji na hakuwa na malazi
ya tumbo.
Inaelezwa
Marehemu alifariki Februari 17 mwaka huu katika hospitali binafsi za madaktari
wa Bugando Jijini Mwanza, ambapo awali inadaiwa alikuwa amelazwa Bugando na kupelekwa
kwenye huko kufanyiwa upasuaji wa Goita Shingoni na kufariki dunia, na kisha
mwili wake kurudishwa tena Bugando kwenye chumba cha maiti.
Akielezea tukio
hilo jana Mjomba wa marehemu Sued Mussa, alisema marehemu alikuwa anaumwa Goita
Shingoni na alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga,
na kupewa Rufaa kwenda Bugando Jijini Mwanza na hatimaye mauti kumfika, na
kwenda kuuchukua mwili wake kwa maziko.
“Wakati wakina
mama walipokuwa wakiuosha mwili wa marehemu waliona pembeni ya tumbo kuna tundu,
na wakati marehemu alikuwa na tatizo shingoni lakini hawakusema hadi tuna mzika
juzi (februari 18), ndipo wakaanza minong’ono kuwa wamekuta tundu hilo.”alisema.
Aliongeza baada
ya taarifa hiyo ndipo wakaenda kutoa taarifa Polisi wakitaka mwili wa ndugu yao
ufukuliwe, ili uweze kufanyiwa uchunguzi (Postmoterm) kujiridhisha kama kweli
ametobolewa tumbo, na kupewa taarifa kwanini alifanyiwa hivyo na wakati tatizo
lake lilikuwa ni Shingoni.
Naye mwenyekiti
wa mtaa huo wa Chamaguha Kata ya Chamaguha Madaraka Mohamedi, alisikitishwa na tukio hilo na kubainisha kuwa wanafanya
ufukuaji wa mwili huo, ili kubaini huenda labda kuna viungo vya marehemu
vimetolewa sababu hakuwa na tatizo la malazi ya tumbo.
Kwa upande wake mkuu
wa upelelezi wa makosa ya jinai wa Jeshi la Polisi Jijini Mwanza John Mwaulemi,
ambaye alifika mkoani Shinyanga kwa ajiri ya kusimamia uchunguzi wa mwili huo wa marehemu , alisema baada ya kumalizika
kufanyika zoezi hilo ndipo watatoa taarifa kamili juu ya tukio hilo kama kweli
viungo vyake havipo ama ni uzushi, ambapo imeshabinika kuwa marehemu hakutobolewa tumbo.
Aidha Mwili huo
wa marehemu unatarajiwa kufukiliwa leo kwenye makaburi ya Chamaguha manispaa ya
Shinyanga Tayari kwenda kufanyiwa uchunguzi kama kweli baadhi ya viungo vyake
ndani ya mwili vilitolewa na madaktari.
TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Baadhi
ya wananchi wa Mtaa na Kata ya Chamaguha manispaa ya Shinyanga wakiwa
katika ofisi ya mtaa huo kwa ajili ya kusubili maelekezo ya kwenda
kuufukua mwili wa marehemu Ashura Shabani, ambaye ameacha watoto watano,
kwa ajiri ya kwenda kufanyiwa uchunguzi ilikujiridhisha kama amezika
huku baadhi ya viungo vyake vya ndani ya mwili vikiwa vimetolewa na
Madaktari huko Jijini Mwanza.
Akina
mama nao hawakuwa nyuma kushuhudia tukio hilo, ambao wao ndio inaelezwa
waliona tundu hilo pembeni mwa tumbo la marehemu wakati wakiuosha mwili
kwa ajili ya maziko, lakini walinyamaza kimya hadi marehemu Ashura
Shabani anazikwa, ndipo wakaanza minong'ono kuwa wameona tundu tumboni
mwa marehemu ,na wakati alifariki kwa ugonjwa wa Shingo Goita wakati
akifanyiwa upasuaji.
Wananchi
wa Mtaa na Kata ya Chamaguha wakiwa eneo la ofisi ya Mtaa huo majira ya
saa moja na Nusu usiku wakisubili maelekezo ya kwenda kuufukua mwili wa
marehemu Ashura Shabani, kwa ajili ya kwenda kufanyiwa uchunguzi juu ya
kuwepo na mashaka hayo huenda viungo vyake vimetolewa na Madaktari
Jijini Mwanza alipokuwa akipatiwa matibabu.
Wananchi
wa Mtaa na Kata ya Chamaguha manispaa ya Shinyanga wakiwa katika ofisi
za mtaa huo, ambapo walipewa maelekezo na mwenyekiti wao Madaraka
Mohamed kuwa usiku umeingia hivyo leo majira ya asubuhi ndipo wataufukua
mwili huo wa marehemu, ilikwenda kufanyiwa uchunguzi kama kweli Pembeni
mwa Tumbo lake pamepasuliwa na kutolewa baadhi ya viungo vyake, kwa
lengo la kupata ukweli juu ya taarifa zilizotolewa na akina mama wakati
wakiuosha mwili wa marehemu.
Na Marco Maduhu
ambaye
pia ni Mwandishi wa Gazeti kubwa hapa nchini la Nipashe mkoani
Shinyanga, soma Nipashe kila siku uhabalike kwa habari zenye uhakika na
makini