MAREHEMU KUFUKULIWA SHINYANGA MASHAKA YA VIUNGO KUTOLEWA NDANI YA MWILI NA MADAKTARI MWANZA ALIPOKUWA AKIPATIWA MATIBABU


 Mjomba wa marehemu  Sued Mussa, akielezea jinsi tukio la Ashura Shabani alivyofariki hadi kuwepo na mashaka huenda baadhi ya viungo vyake ndani ya mwili vimetolewa na madkatari jijini Mwanza alipokuwa akipatiwa matibabu, mara baada ya kuwepo na taarifa kuwa kumekutwa tundu pembeni ya tumbo lake ,na wakati marehemu alifariki dunia kwa ugonjwa wa Shingo (Goita) wakati akifanyiwa upasuaji.


SOMA HABARI KAMILI
.
Mwili wa marehemu Ashura Shabani (30) aliyekuwa mkazi wa Kata ya Chamaguha manispaa ya Shinyanga, unatarajiwa kufukuliwa  baada ya kuwepo na mashaka juu ya mwili wake kuwepo na tundu pembeni mwa tumbo na huenda kuna baadhi ya viungo vyake kutolewa,kwa madai alifariki kwa ugonjwa wa shingo (Goita) wakati akifanyiwa upasuaji na hakuwa na malazi ya tumbo.

Inaelezwa Marehemu alifariki Februari 17 mwaka huu katika hospitali binafsi za madaktari wa Bugando Jijini Mwanza, ambapo awali inadaiwa alikuwa amelazwa Bugando na kupelekwa kwenye huko kufanyiwa upasuaji wa Goita Shingoni na kufariki dunia, na kisha mwili wake kurudishwa tena Bugando kwenye chumba cha maiti.

Akielezea tukio hilo jana Mjomba wa marehemu Sued Mussa, alisema marehemu alikuwa anaumwa Goita Shingoni na alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga, na kupewa Rufaa kwenda Bugando Jijini Mwanza na hatimaye mauti kumfika, na kwenda kuuchukua mwili wake kwa maziko.

“Wakati wakina mama walipokuwa wakiuosha mwili wa marehemu waliona pembeni ya tumbo kuna tundu, na wakati marehemu alikuwa na tatizo shingoni lakini hawakusema hadi tuna mzika juzi (februari 18), ndipo wakaanza minong’ono kuwa  wamekuta tundu hilo.”alisema.

Aliongeza baada ya taarifa hiyo ndipo wakaenda kutoa taarifa Polisi wakitaka mwili wa ndugu yao ufukuliwe, ili uweze kufanyiwa uchunguzi (Postmoterm) kujiridhisha kama kweli ametobolewa tumbo, na kupewa taarifa kwanini alifanyiwa hivyo na wakati tatizo lake lilikuwa ni Shingoni.

Naye mwenyekiti wa mtaa huo wa Chamaguha Kata ya Chamaguha Madaraka Mohamedi, alisikitishwa na  tukio hilo na kubainisha kuwa wanafanya ufukuaji wa mwili huo, ili kubaini huenda labda kuna viungo vya marehemu vimetolewa sababu hakuwa na tatizo la malazi ya tumbo.

Kwa upande wake mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wa Jeshi la Polisi Jijini Mwanza John Mwaulemi, ambaye alifika mkoani Shinyanga kwa ajiri ya kusimamia uchunguzi wa mwili  huo wa marehemu , alisema baada ya kumalizika kufanyika zoezi hilo ndipo watatoa taarifa kamili juu ya tukio hilo kama kweli viungo vyake havipo ama ni uzushi.

Aidha Mwili huo wa marehemu unatarajiwa kufukiliwa leo kwenye makaburi ya Chamaguha manispaa ya Shinyanga Tayari kwenda kufanyiwa uchunguzi kama kweli baadhi ya viungo vyake ndani ya mwili vilitolewa na madaktari.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


 Baadhi ya wananchi wa Mtaa na Kata ya Chamaguha manispaa ya Shinyanga wakiwa katika ofisi ya mtaa huo kwa ajili ya kusubili maelekezo ya kwenda kuufukua mwili wa marehemu Ashura Shabani, ambaye ameacha watoto watano, kwa ajiri ya kwenda kufanyiwa uchunguzi ilikujiridhisha kama amezika huku baadhi ya viungo vyake vya ndani ya mwili vikiwa vimetolewa na Madaktari huko Jijini Mwanza.
 Akina mama nao hawakuwa nyuma kushuhudia tukio hilo, ambao wao ndio inaelezwa waliona tundu hilo pembeni mwa tumbo la marehemu wakati wakiuosha mwili kwa ajili ya maziko, lakini walinyamaza kimya hadi marehemu Ashura Shabani anazikwa, ndipo wakaanza minong'ono kuwa wameona tundu tumboni mwa marehemu ,na wakati alifariki kwa ugonjwa wa Shingo Goita wakati akifanyiwa upasuaji.
 Wananchi wa Mtaa na Kata ya Chamaguha wakiwa eneo la ofisi ya Mtaa huo majira ya saa moja na Nusu usiku wakisubili maelekezo ya kwenda kuufukua mwili wa marehemu Ashura Shabani, kwa ajili ya kwenda kufanyiwa uchunguzi juu ya kuwepo na mashaka hayo huenda viungo vyake vimetolewa na Madaktari Jijini Mwanza alipokuwa akipatiwa matibabu.
Wananchi wa Mtaa na Kata ya Chamaguha manispaa ya Shinyanga wakiwa katika ofisi za mtaa huo, ambapo walipewa maelekezo na mwenyekiti wao Madaraka Mohamed kuwa usiku umeingia hivyo leo majira ya asubuhi ndipo wataufukua mwili huo wa marehemu, ilikwenda kufanyiwa uchunguzi kama kweli Pembeni mwa Tumbo lake pamepasuliwa na kutolewa baadhi ya viungo vyake, kwa lengo la kupata ukweli juu ya taarifa zilizotolewa na akina mama wakati wakiuosha mwili wa marehemu.

Na Marco Maduhu 
ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti kubwa hapa nchini la Nipashe mkoani Shinyanga, soma Nipashe kila siku uhabalike kwa habari zenye uhakika na makini








Powered by Blogger.