WALIMU WA SEKONDARI KUPELEKWA KUFUNDISHA MSINGI
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala bora
Dkt. Laurean Ndumbaro akiwa katika kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya
Mji wa Makambako.
SOMA HABARI KAMILI
Katibu mkuu ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na utawala bora Dkt Laurean Ndumbaro, amesema walimu wa Shule za Sekondari kupangiwa
kufundisha Shule za msingi ni moja ya hatua katika kuleta ufanisi na mgawanyo
sawa wa walimu katika shule hizo.
Amsema hatua
hiyo ya walimu wa Sekondari kupelekwa kufundisha msingi haimaanishi kuwa ndio wameshushwa vyeo.
Dk Ndumbaro ametolea ufafanuzi huo katika kikao kazi
na watumishi wa halmashauri ya mji wa makambako, na kusisitiza kuwa lengo la serikali ni kuondoa upungufu wa
walimu katika shule za msingi, na kuimarisha utoaji wa elimu hapa nchini.
Amesema mabadiliko hayo yasionekane ni jambo la
ajabu kwa mwalimu wa Sekondari mwenye kiwango cha Shahada kwenda kufundisha
shule ya msingi.
Aidha amewaambia watumishi hao wa umma, maendeleo katika sekta yeyote
ikiwamo ya elimu yanakuja na mabadiliko, hivyo wapokee mabadiliko na kufanya
kazi iliwafikie malengo.
TAZAMA HABARI PICHA HAPA CHINI
Mmoja wa watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako
akitumia fursa ya kuwasilisha hoja kwa Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro
(hayupo pichani) wakati wa kikao kazi mjini Makambako.
Sehemu ya watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako walioshiriki kikao kazi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani). Watumishi walipata fursa ya kuuliza
masuala mbalimbali ya kiutendaji na kupewa ufafanuzi.
IMEANDALIWA NA MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA.