WARAMI WAPINGANA NA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT NCHINI
Mkurugenzi wa Utafiti wa Tasisi ya Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka (WARAMI), Philipo Mwakibinga akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kukosoa tamko lililotolewa na Maaskofu wa KKKT nchini.
Mkurugenzi wa Utafiti wa Tasisi ya Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka (WARAMI), Philipo Mwakibinga akizungumza
na Waandishi wa Habari juu ya kukosoa tamko lililotolewa na Maaskofu wa
KKKT nchini katika ukumbi wa Traventine Magomeni.
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
WATETEZI
wa Rasilimali wasio na Mipaka-WARAMI wameupinga waraka wa Ujumbe wa
pasaka kutoka kwa baraza la maaskofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri
Tanzania (KKKT) uliotolewa jana, kwa madai kuwa ulikuwa wa kisiasa wenye
lengo la kukososa utendaji wa serikali na kuleta hofu kwa jamii.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Da res Salaam, Mkurugenzi wa Utafiti WARAMI,
Philipo Mwakibinga amedai kuwa maskofu kama viongozi wa dini wanatakiwa
kujikita katika masuala yanayohusu dini na si siasa.
“WARAMI
tunaamini kwamba wajibu wetu ni kuhakikisha jamii inapata haki pasipo
upendeleo wowote, kufuatia hili tumeona si sahihi kukaa kimya, tukaona
tupaze sauti kuona tunaijenga jamii kulingana na tofauti zao. Kwenye
nafsi zao wanavyo vyama vyao mbali na uongozi wa kidini. Hisia za
kivyama zisilete mtafaruku kwenye Imani. Wajitafakari kuchagua aina ya
maneno wanayotoa kwa jamii ili kulinda na kukuza amani,” amesema na
kuongeza.
“Tunashangaa
kwa nini waraka huu wa salamu za pasaka haukujikita katika kuwasisitiza
waumini wake kujikita katika kuabudu, kumnyenyekea Mungu, kusoma biblia
na maandiko mengine ya dini na badala yake wanajikita katika maoni
yanayong’ata na kupuliza.”
Mwakibinga
amedai kuwa, Miongoni mwa masuala yaliyoandikwa katika waraka huo ni
malalamiko kuhusu mchakato wa katiba mpya na uhuru wa kutoa maoni, ambao
ulikwamishwa na wansiasa wa upinzani waliosusia kushiriki mchakato
huo.
“Maaskofu
wamezungumzia kuhusu utekwaji na mauaji ikiwemo utiaji wa hofu lakini
hawajajikita kuelezea kwa kina kisa hasa ni kipi. Sisi tunafahamu kuwa
wapo walioathirika moja kwa moja na matukio ya kutekwa na kuteswa kwa
baadhi ya vijana ambayo yalipaswa kukemewa tangu siku ya kwanza ya
kutokea kwake na si kuyasubiri mpaka leo,” amesema.