ZIARA YA RAIS MAGUFULI SHINYANGA ULINZI KILA KONA
Picha siyo ya ziara husika
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya ujio huo wa Rais Magufuli mkoani Shinyanga.
SOMA HABARI KAMILI
Rais wa jamuhuri wa muugano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, anatarajiwa kesho kufaya ziara ya kikazi mkoani Shinyanga katika wilaya ya Kahama.
Ziara hiyo ya Rais Magufuli itaanza majira ya saa Nane mchana, ambapo atafungua barabara ya kiwango cha Lami kutoka Isaka kwenda Lusahunga Ushirombo, pamoja na kufanya mkutano wa hadhara na wananchi, na baada ya hapo atafungua kiwanda cha Kahama Oil Mil.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack juu ya ujio huo wa Rais, alisema wananchi wote wanatakiwa kujitokeza kushuhudia matukio hayo yote, pamoja na kuhudhuli kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara ambapo rais atatoa hotuba mbalimbali.
“Nimeita vyombo vya habari ilimuweze kuhabarisha umma kuwa tutakuwa na ugeni mkubwa hapa mkoani kwetu wa ujio wa Rais wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, hivyo nawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kumpokea Rais wetu na kushuhudia matukio hayo.”alisema Telack.
Aliongeza kuwa hizo ndio kazi ambazo atazifanya Rais Magufuli wilayani Kahama mkoani Shinyanga, za ufunguzi wa barabara kwa kiwango cha lami Kiwanda cha mafuta pamoja na kuzungumza na wananchi, na kubainisha kuwa hiyo ndio ratiba yake na kama atafanya tukio jingine mkoa huo utafurahi pia.
Kwa upande wake Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Kamishina msaidizi wa Polisi (ACP) Simoni Haule, aliwatoa hofu wananchi na kuwataka wadhulie kwa wingi kwenye ugeni huo mkubwa wa Rais Magufuli, ikiwa ulinzi ume imarishwa kila kona, na hakuna mtu yeyote ambaye ataweza kutishia kuvuruga amani.
Alisema ugeni huo ni nadra sana na ni bahati kwa wana Shinyanga, bali waitumie furasa hiyo kwenda kutatuliwa kero zao, na wasisite kuhusu suala la ulinzi ambapo doria zimefanyika kila kona hadi kwenye majumba ya kufikia wageni, na katika msafara huo wa Rais kutakuwa na ulinzi mkali.
Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa Nipashe hivyo HABARI hizo pia utazisoma Nipashe.