AGNES MASOGANGE AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 3


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu video queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ kulipa faini ya Shilingi Milioni 1.5 ama kwenda jela miaka 3 baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.
Kutokana na hukumu hiyo, Wakili wa utetezi Nehemiah Nkoko amesema kuwa watalipa faini.


Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amesema kuwa katika ushahidi wa kesi hiyo upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi 3, huku utetezi ukiwa na shahidi 1.


Hakimu Mashauri amesema kuwa ameridhishwa pasina kuacha shaka juu ya ushahidi wa upande wa mashtaka hasa kwa uthibitisho uliotolewa na Mkemia Mkuu wa serikali kwamba mkojo wa mshtakiwa ulikutwa na chembe chembe za dawa za kulevya.


“Kutokana na kujiridhisha na ushahidi huo, namtia hatiani mshtakiwa kwa makosa hayo ya kutumia dawa za kulevya,”-Hakimu Mashauri


Baada ya Masogange kutoa utetezi wake, Hakimu Mashauri amesema kuwa ameusikia utetezi wa mshtakiwa kwamba apewe adhabu ndogo, huku upande wa mashtaka ukitaka apewe adhabu kali.


“Nimesikiliza maelezo ya pande zote, katika kosa la kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin namuhukumu mshtakiwa kulipa faini ya Sh.Mil 1 ama jela miaka 2.

” Katika kosa la pili la kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam, nakuhukumh kulipa faini ya Sh.Laki 5 ama jela miezi 12,” amesema Hakimu Mashauri
 
Powered by Blogger.