AKINA MAMA WA PEMBEZONI WAPIGIWA DEBE KUPEWA MIKOPO



Baraza la madiwani la halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, limeutaka uongozi wa halmashauri hiyo kupitia idara ya maendeleo ya jamii kujikita pia kutoa elimu ya ujasiriamali kwa akina mama waliopembezoni mwa mji huo, pamoja na kuwapatia mikopo ambayo itawainua kiuchumi.

Madiwani walizungumza hayo jana April 26. 2018 kwenye kikao cha Baraza la kawaida wakati wakijadili Taarifa ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo ya miradi ya robo tatu ya mwaka, kuwa akina mama wote walio katikati ya mji na pembezoni wote wapatiwe elimu ya ujasiriamali, na kujiunga kwenye vikundi ili wapewe mikopo.

Mmoja wa madiwani hao kutoka Kata ya Mwawaza ambayo ipo pembezoni mwa mji huo Juma Nkwabi, alisema maofisa maendeleo ya jamii wamekuwa wakifanya kazi kimazoea na kubaki kutoa elimu na mikopo kwa vikundi vya akina mama wa katikati ya mji, lakini wale wa pembezoni wamekuwa hawanufaiki na mikopo hiyo.

“Mikopo hii imekuwa ikinufaisha akina mama wa mjini tu, na wamekuwa wakijirudia mara kwa mara kupewa fedha, lakini ambao wapo pembezoni mwa mji hawafikiwi na elimu hiyo na kushindwa kunufaika na mikopo ya halmashauri,”alisema Nkwabi.

Naye Ofisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwanamsiu Dosi, alifafanua kuwa maeneo hayo ya pembezoni mwa mji ambayo akina mama na vijana hawajapewa elimu ya ujasiriamali na kujiunga kwenye vikundi ilkupewa mikopo, ni zile ambazo hazina maofisa maendeleo wa Kata.

Alisema halmashauri hiyo ina upungufu wa maofisa maendeleo wasaidizi 10, na hivyo kuwepo na ugumu wa kutembelea maeneo yote kutolewa elimu hiyo ya ujasiriamali, na kubainisha katika mwaka wa fedha (2017-18) zimeshatolewa fedha za Mikopo Shilingi Milioni 125 kwa vikundi 20, akina mama vikundi (11) Shilingi 60,000,000, Vijana vikundi (9) Shilingi 65,000,000.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geofley Mwangulumbi, alikiri kuwepo na upungufu wa maofisa maendeleo wasaidizi ngazi ya Kata, na ndio sababu ya kuwepo na changamoto ya baadhi ya akina mama kutopewa elimu na mikopo, na kuahidi suala hilo litafanyiwa kazi.

Diwani wa Kata ya Mwawaza Juma Nkwabi ambayo ipo pembezoni mwa mji wa Shinyanga akizungumza kwenye Baraza hilo na kuomba akina mama ambao wapo pembezoni mwa mji huo wa Shinyanga nao wapewe elimu ya ujasiriamali na kujiunga kwenye vikundi ili nao wapate kupewa mikopo hiyo ya Halmashauri na siyo wa mjini tu.

Diwani wa Kata ya Kizumbi Rubeni Kitinya ambayo nayo ipo Pembezoni mwa mji wa Shinyanga naye akizungumza kwenye Baraza hilo ameomba akina mama na vijana ambao wapo pembezoni mwa mji nao wapatiwe elimu na kujiunga kwenye vikundi ili wapate kunufaika na fedha hizo za mikopo za halmashauri na siyo mji tu, ambao wamekuwa tena wakijirudia mara kwa mara.

Diwani wa Kata ya Ibinzamata Daniel Matemu naye akichangia hoja hiyo na kuuuomba uongozi wa halmashauri hiyo ya manispaa ya Shinyanga kupitia Idara ya maendeleo ya jamii, pia kuwakumbuka watu wenye ulemavu nao wapatiwe kipaumbele kwenye mikopo hiyo.

Diwani wa Kata ya Chamaguha Morisi Mgini akichangia hoja, aliomba pia vikundi ambayo vina kwenda kwenye halmashauri hiyo kufuatilia masuala ya mikopo kusiwepo na usumbufu ambao kwa sasa upo, na umekuwa kero kwenye vikundi hivyo vya akina mama na hatimaye kuwa katisha tamaa.

Diwani wa Kata ya Ndala Wiliamu Shayo, naye akichangia hoja alipongeza kazi inayofanywa na Maofisa maendeleo ya jamii, na kuomba mapungufu madogo madogo ambayo yapo wayafanyie kazi.

Ofisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwanamsiu Dosi, alifafanua kuwa maeneo hayo ya pembezoni mwa mji ambayo akina mama na vijana hawajapewa elimu ya ujasiriamali na kujiunga kwenye vikundi ilkupewa mikopo, ni zile ambazo hazina maofisa maendeleo wa Kata.

Alisema halmashauri hiyo ina upungufu wa maofisa maendeleo wasaidizi 10, na hivyo kuwepo na ugumu wa kutembelea maeneo yote kutolewa elimu hiyo ya ujasiriamali, na kubainisha katika mwaka wa fedha (2017-18) zimeshatolewa fedha za Mikopo Shilingi Milioni 125 kwa vikundi 20, akina mama vikundi (11) Shilingi 60,000,000, Vijana vikundi (9) Shilingi 65,000,000.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geofley Mwangulumbi, alikiri kuwepo na upungufu wa maofisa maendeleo ya jamii wasaidizi ngazi ya Kata, na ndio sababu ya kuwepo na changamoto ya baadhi ya akina mama kutopewa elimu na mikopo, na kuahidi suala hilo litafanyiwa kazi.

Madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye baraza lao la kawaida wakijadili Ajenda mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya manispaa hiyo.

Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.
Powered by Blogger.