AKINA MAMA WALALAMIKA KUFANYIWA UKATILI WA KIUCHUMI NA WAUME ZAO KIPINDI CHA MAVUNO



Akina mama wanaoishi katika Kata za Nyida, Itwangi na Nsalala halmashauri ya Shinyanga vijijini mkoani hapa, wamelalamika kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kiuchumi kutoka kwa waume zao, kwa kuuza mazao kwa nguvu bila ya kuwa shirikisha na kisha pesa kuzitumia hovyo na kuwafanya kuendelea kuwa maskini.

Walisema idadi kuwa ya akina mama katika maeneo hayo ya vijijini ndio hua wanakesha mashambani wakilima kuliko waume zao, lakini linapofika suala la kuuza mazao wanaume ndio huchukua fedha zote kwa madai ndio kichwa cha faimilia, na kisha fedha hizo kuzitumia katika masuala ya Anasa.

Baadhi ya akina mama hao Elzabeth Simon na Merry Christopher walibainisha hayo hivi karibuni kwa nyakati tofauti kwenye Mdaharo wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsi ndani ya jamii, ulioandaliwa na Shirika la Kivulini linalo tetea haki za wanawake na watoto mkoani Shinyanga kwa ufadhiri wa Shirika la OXFAM.

“Kipindi hiki cha mavuno kwenye familia zetu kumekuwa na ukatiri wa kiuchumi ambapo wanaume wameanza tabia ya kuuza mazao na kupesa kutoonekana, wana kwenda Centa kuzifanyia Anasa, kunywa pombe na kununua Madada poa ambao hutoka mjini kwenye kipindi hiki cha mavuno, na ukihoji pesa zikowapi una ambulia kipigo,”walisema.

Nao wanaume waliokuwa kwenye mdaharo huo akiwamo James Masunga, walikiri kuwepo na tabia hiyo kwa baadhi ya wenzao kwa madai kuwa hiyo ni dhana ambayo ilijengeka toka zamani, na kuomba wadau wa maendeleo, mashirika na Serikali kuendelea kujikita zaidi kutoa elimu ya matumizi ya fedha kwa wananchi.

Naye mwenyekiti wa Kijiji cha Welezo Kata ya Nyida Janet Mabula, alikiri kuwepo na ukatili huo wa kiuchumi ndani ya jamii, na kubainisha kwa sasa amekuwa akipokea kesi nyingi za vipigo kwa akina mama, ambao wamekuwa wakigomea waumezao kuuza mazao kiholela bila ya kushauriana na familia.

Kwa upande Ofisa maendeleo ya Jamii halmashauri ya Shinyanga vijijini Deusi Mhoja ambaye alikuwa mwenyekiti wa mdaharo huo, alisema Serikali imekuwa ikitoa elimu kila mara kwa wananchi namna ya matumizi ya fedha pamoja na kutunza chakula kwa kutokiuza chote, na kubainisha kuwa elimu hiyo wataendelea kuitoa zaidi.


Akina mama ambao ni wana mabadiliko kutoka Kata za Nyida, Nsalala na Itwangi Shinyanga vijijini, wakiwa kwenye mdaharo wa kupinga vitendo vya ukatiri wa kijinsia ndani ya jamii.

Monica Simoni akizungumza kwenye mdaharo huo na kukalalamika vitendo ambavyo hufanyiwa akina mama na waume zao kwenye kipindi cha mavuno, ambapo wamekuwa wakiwanyanyasa kiuchumi kwa kuuza mazao kwa nguvu na kutoshirikisha familia, na kisha pesa kuzitumia kwenye masuala ya Anasa na kuwafanya kuendelea kuwa maskini.

James Masunga akizungumza kwenye mhadaro huo amekiri ni kweli akina mama wamekuwa wakinyanyasika kutoka kwa waume zao kiuchumi kwenye kipindi cha mavuno, na kuiomba Serikali na Mashirika yaendelee pia kutoa elimu zaidi kwa wananchi hasa wanaume vijijini namna ya matumizi ya pesa ili waweze kupata maendeleo na kilimo chao kionekane kuwa na Tija.

Mwenyekiti wa kijiji cha Welezo Kata ya Nyida Janet Mabula akizungumza kwenye mdaharo huo amesema hivi sasa ameshaanza kupokea kesi nyingi za akina mama kupewa vipigo na waume zao kwa madai ya kumzui kuuza mazao kiholela bila ya kushirikisha familia.

Kwa upande Ofisa maendeleo ya Jamii halmashauri ya Shinyanga vijijini Deusi Mhoja ambaye alikuwa mwenyekiti wa mdaharo huo, alisema Serikali imekuwa ikitoa elimu kila mara kwa wananchi namna ya matumizi ya fedha pamoja na kutunza chakula kwa kutokiuza chote, na kubainisha kuwa elimu hiyo wataendelea kuitoa zaidi.

Na Marco Maduhu, ambaye pia ni mwandishi wa Gazeti la Nipashe Shinyanga.








Powered by Blogger.