WATU WENYE UALBINO WAMEIPONGEZA JAMII YA SHINYANGA KUTOWANYANYAPAA
Chama cha watu wenye ulbino Manispaa ya Shinyanga (TAS) wameipongeza jamii kwa kuzingatia elimu kwa vitendo ambayo hutolewa na viongozi wa Serikali na Dini, juu ya kuondoa unyanyapaa dhidi yao, na kuwafanya waishi kwa amani na upendo.
Hayo yamebainishwa leo April 10, 2018 na katibu wa chama hicho Lazaro Anael, kwenye kikao cha viongozi wa Kata ya Masekelo manispaa ya Shinyanga, wakati akifuatilia mrejesho wa mafunzo waliopewa viongozi hao ngazi ya Kata, namna ya kutoa elimu ndani ya jamii ya kuacha kunyanya paa watu hao Albino.
Anael amesema katika mradi wao wa ujumuishwaji watu wenye ualbino ndani ya jamii (ALICN) kwa ufadhili wa Lilian Faundation kutoka Nezeland, ambao utadumu miaka miwili (2017-19) umeonekana kuanza kuzaa matunda, ambapo jamii imeanza kuwaona Albino ni watu wa kawaida na kushirikina nao kwenye shughuli mbalimbali zikiwamo za kiuchumi.
“Mradi huu wa ujumuishwaji watu wenye Ualbino ndani ya jamii tunautekeleza katika Kata 17 za manispaa ya Shinyanga, ambapo mpaka sasa Kata tano zimeshatolewa elimu ya kutonyanyapaa Albino ambazo ni Ndala, Oldshinyanga, Mwamalili, Kolandoto na Ibadakuli, na mrejesho wake unaonekana kuwa mzuri,”Amesema Anael
Naye Zungu Mboje mwenye Ualbino mkazi wa Kata ya Masekelo mjini Shinyanga, anasema hata majina ya udharirishaji ambayo walikuwa wakiitwa zamani ikiwamo Zeluzelu, Mbilimelo hayapo tena, na watu ambao wanawafahamu huwaita kwa kutamka majina yao.
Kwa upande wake mtendaji wa Kata ya Masekelo Ester Daudi, ametoa wito kwa jamii kuendelea kuwa na tabia ya kuzingatia elimu mbalimbali kwa vitendo ambazo hutolewa kwao, ikiwamo hiyo ya kutowanyanyapaa watu wenye Ualbino ili wapate kuishi kwa Amani na kufanyashughuli zao za kiuchumi.
TAZAMA HABARI PICHA HAPA CHINI.
Katibu wa chama cha watu wenye Ualbino katika manispaa ya Shinyanga (TAS) Anael Lazaro, akizungumza kwenye kikao na viongozi wa Kata ya Masekelo manispaa ya Shinyanga juu ya kupanga mkakati ya kuendelea kutoa elimu ndani ya jamii ya kuacha kunyanyapaa Albino, kwa njia wa Sinema, mabonanza ya michezo, midaharo, pamoja na mikutano ya hadhara.
Zungu Mboje mkazi wa Kata ya Masekelo mjini Shinyanga,anapongeza elimu ambayo hutolewa kwa wananchi dhidi ya kutowanyanyapaa na kubainisha kuwa hata majina ya udhalirishaji ambayo walikuwa wakiitwa zamani ikiwamo Zeluzelu, Mbilimelo hayapo tena, na watu ambao wanawafahamu huwaita kwa kutamka majina yao.
Mtendaji wa Kata ya Masekelo Ester Daudi, akizungumza kwenye kikoa hicho ametoa wito kwa jamii kuendelea kuwa na tabia ya kuzingatia elimu mbalimbali kwa vitendo ambazo hutolewa, ikiwamo hiyo ya kutowanyanyapaa watu wenye Ualbino ili wapate kuishi kwa Amani na kufanyashughuli zao za kiuchumi.
Ofisa maendeleo ya jamii Kata hiyo ya masekelo manispaa ya Shinyanga Aisha Msofe, akizungumza kwenye kikao hicho amesema unyanyapaa dhidi ya watu hao Albino haupo tena ndani ya jamii, ambapo wamekuwa wakishirikiana nao kwenye shughuli mbalimbali za kijamii tofauti na zamani.
Mtaalamu wa Afya wa Kata hiyo ya Masekelo Zabron Mazoya anasema matukio ya kuwatenga Albino ndani ya jamii hayapo tena, ambapo wamekuwa wakishii bila ya ubaguzi na wamekuwa wakishilikiana nao katika shughuli mbalimbali, na kuwaona kama watu wa kawaida.
Huseni Mohamed Kheli akiwakilisha viongozi wa madhehebu mbalimbali ya kidini kwenye Kata hiyo ya Masekelo, ameahidi vingozi hao wa kidini wataendelea kutoa elimu ya kupinga unyanyapaa kwenye madhabahu kwa waumini wao dhidi ya watu hao Albino.
Mtaalamu wa afya Kata ya Masekelo Zabroni Mzoya (mkono wa kushoto), akiwa na Zungu Mboje mwenye Ualbino kwenye kikao hicho cha viongozi wa Kata ya Masekelo, juu ya kupanga mikakati ya kuendelea kutoa elimu ndani ya jamii ya kupinga unyanyapaa dhidi ya watu wenye Ualbino.
Mtendaji wa mtaa wa Bondeni Kata hiyo ya Masekelo Osca Mshana (mkono wa Kushoto) akiwa na Ofisa maendeleo ya jamii Kata hiyo Aisha Msofe kwenye kikao cha TAS manispaa ya Shinyanga.
Wajumbe wakiendelea na majadiliano kwenye kikao, na namna ya kupanga mikakati ya kutoa elimu kwa jamii juu ya kutonyanyapaa watu wenye Ualbino, na kushirikiana nao katika shughuli za kijamii pamoja na kutowaita majina mabaya.
Wajumbe wakiendelea na kikao.
Katibu wa chama cha watu wenye Ualbino Manispaa ya Shinyanga (TAS) Lazaro Anael, akielezea wajumbe madhumuni ya kikao hicho ambacho kimefanyika katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Masekelo Mjini Shinyanga.
Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.