DC MATIRO ATENGUA MUONGOZO UTOAJI MIKOPO MARA MBILI KWA MWAKA
Mkuu wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro, ametengua muongozo wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wa utoaji wa mikopo kwa akina mama mara mbili kwa mwaka, na kuagiza iwe mara Nne, ili vikundi vingi viweze kunufaika na mikopo hiyo ambayo itawainua kiuchumi.
Matiro ametengua muongozo huo leo April 27, 2018 wakati akizungumza na vikundi mbalimbali vya akina mama wa manispaa ya Shinyanga waliokatika vikundi vya ujasiriamali, kwa lengo la kutoa elimu kwao namna ya kutimiza masharti ya kupata mikopo kwa uharaka, na kuondoa vikwazo ambavyo vimekuwa vikikwamisha kupata mikopo hiyo kwa uharaka.
Alisema Serikali imedhamilia kuwainua kiuchumi akina mama, ambapo wameshahamasika kujiunga kwenye vikundi, na kuamua kuvunja muongozo wa halmashauri hiyo wa kutoa mikopo kwa akina mama asilimia Tano mara mbili kwa mwaka, na iwe mara Nne ili vikundi vyao vyote viweze kunufaika na fedha hizo.
“Nautengua muongozo wa halmashauri kutoa mkopo kwa akina mama mara mbili kwa mwaka, kuanzia sasa iwe mara Nne, na agizo hili nyie maofisa maendeleo mka mweleze mkurugenzi wenu, tuna taka akina mama wainuke kiuchumi na kuunga juhudi za Rais John Magufuli ya Tanzania ya viwanda,”alisema Matiro.
“Naomba akina mama muache malalamiko kuwa maisha magumu, huku mkiwa mmekaa majumbani, na wakati kuna fursa nyingi ambazo zitaweza kuwa inua kiuchumi na kuanzisha viwanda vidogo, na sasa hivi fedha ambazo mtapewa za mikopo za halmashauri hazina Riba, fedha ambayo utakopa ndiyo hiyo hiyo ambayo utairejesha, “acheni kulialia”,”aliongeza Matiro.
Awali kabla ya kutolewa agizo hilo, akina mama hao walihoji mikopo hiyo ya halmashauri hua ina tolewa mara ngapi, ambapo Ofisa maendeleo ya jamii manispaa hiyo Ruchagula Chalres, alisema kutokana na muongozo uliopo hutolewa mara mbili kwa mwaka, muongozo ambao mkuu huyo wa wilaya aliutengua.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii halmashauri hiyo ya manispaa ya Shinyanga Mwanamsiu Dosi, alisema katika mwaka wa fedha (2017-18) fedha za maendeleo walitenga shilingi Milioni 248, na mpaka sasa wameshatoa Shilingi Milioni 125 katika vikundi 20, Akina mama vikundi 11 shilingi 60,000,000, Vijana vikundi 9, Shilingi 65,000,000,.
TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro, akizungumza na baadhi ya akina mama wa manispaa ya Shinyanga ambao wameshajiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali, namna ya kujua kuandika maombi ya kuomba mikopo na kutimiza masharti ya maombi hayo, pamoja na kuandika katiba zao kwa usahihi, na hatimaye kupata mikopo kwa uharaka ya halmashauri ambayo itawakwamua kiuchumi.
Katibu wa umoja wa wanawake CCM (UWT) wilaya ya Shinyanga mjini Roda Madaha, akizungumza na akina mama hao kabla ya kumkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambaye ndiye mwenye kikao hicho cha semina ya mafunzo ya mikopo, aliwataka akina mama hao kutobweteka bali wachangamkie fursa za kupata mikopo ya halmashauri ambayo itawainua kiuchumi.
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake CCM (UWT) wilaya ya Shinyanga Mjini Shumbuo Katambi, akizungumza kwenye Simina hiyo ya siku moja, aliwataka akina mama hao kuzingatia elimu ambayo watapewa na wataalamu maofisa maendeleo ya jamii, namna ya kuunda vikundi vya ujasiriamali, kuomba maombi ya mikopo, kuandika katiba ya kikundi na kutimiza masharti yote, ili wapate kupata mikopo hiyo na kujikwamua kiuchumi.
Ofisa maendeleo ya jamii halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Ruchagula Charles, akitoa mafunzo namna ya kuandika katiba ya kikundi na kutimiza mashart yake ili waweze kupata mikopo kwa uharaka bila usumbufu.
Ofisa maendeleo ya jamii halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Magret Lyanga, akitoa elimu nanma ya kuanzisha vikundi, ambapo vinatakiwa kuanzia watu watano, kisajiliwe, kiwe na katiba yao, kiwe na shughuli ya kuzalisha mali, wajuane na wawe wanakaa sehemu mmoja.
Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Mwanamsiu Dosi, akizungumza kwenye simina hiyo alisema pesa zipo na kuwataka akina mama ambao watapata mikopo ya halmashauri hiyo, wawe wanairejesha kwa wakati, ilikutoa fursa na wengine waweze kupata mikopo hiyo ambayo itawainua kiuchumi, na kubainisha mpaka sasa wameshatoa fedha za mikopo shilingi Milioni 125 kwa vikundi 20. akina mama vikundi 11 Shilingi 60,000,000. vijana vikundi 9 Shilingi, 65,000,000.
Baadhi ya akina mama wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Simina ya kupatiwa mafunzo namna ya kutimiza masharti ya kupata mikopo ya halmashauri asilimia Tano, kupitia vikundi vyao iliwapate kuinuka kiuchumi.
Semina ya kujiunga kwenye vikundi na kupata mikopo ikiendelea.
Akina mama wakiendelea kusikiliza Simina hiyo.
Akina mama wakiendelea kusikiliza kwa makini Semina hiyo, ya namna ya kutimiza masharti ya kupata mikopo ya halmashauri ya manispaa ya Shinyanga.
Semina ikiendelea.
Mmoja wa akina mama Verediana Eford akizungumza kwenye Simina hiyo, alisema pale wanakuwa wakienda kuomba mikopo kwenye halmashauri hiyo hua kuna usumbufu mkubwa, ambapo kwenye kikundi chao cha pendo tangu mwaka juzi waliomba mkopo, lakini hadi leo hawajapatiwa, na hivyo kuomba urasimu wa mikopo hiyo usiwepo ikiwa ina katisha tamaa.
Akina mama wakisoma vipeperushi vya namna ya kuandika katiba ya kikundi kwa kuzingatia masharti yake, ili kuondoa usumbufu ambao wamekuwa wakiupata wa kurudishwa mara kwa mara kwenda kuifanyia marekebisho wakati wa kuomba mikopo.
Diwani wa Viti maalumu Zuhura Waziri (mwenye ushungi mweupe kichwani) naye akifuatilia Semina hiyo ya akina mama namna ya kutimiza masharti ya kupata mikopo ya halmashauri, fedha za mapato ya ndani asilimia Tano kwa wanawake, Tano kwa vijana.
Akina mama wakifuatilia mafunzo.
Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.