EWURA RCC YAENDESHA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA




Kamati ya huduma ya Maji na Nishati (EWURA RCC) Mkoani Shinyanga, imetoa mafunzo kwa viongozi wa serikali za mitaa manispaa  juu ya kuwajengea uwezo wa kufahamu haki na wajibu wa mtumiaji wa Nishati na Maji.


Mafunzo hayo yamefanyika leo kwenye ukumbi wa vijana Centa mjini Shinyanga, kwa kushirikisha viongozi hao wa Serikali za mitaa ambao ni Wenyeviti wa vitongoji, mitaa, na watendaji wa Kata ,ili kuwapatia uelewa wa kufahamu chombo cha Ewura CCC  namna kinavyofanya kazi.

Akiwasilisha Mada ya kufahamu majukumu ya Ewura CCC mjumbe wa kamati ya Ewura RCC Mkoa wa Shinyanga  Joseph Ndatala, amesema kazi yake ni kutetea na kusimamia maslahi ya watumiaji wa Nishati na Maji, kutoa elimu kwa umma, kupokea na kusambaza taarifa, pamoja na kushauriana na serikali ili kukidhi malengo yaliyopangwa kwa mtumiaji.

Amesema wameamua kutoa mafunzo hayo kwa viongozi wa Serikali za mitaa ili wakawe mabarozi wazuri kwa wananchi wao, na kuondoa kero ambazo zimekuwa zikiwakabili kwa muda mrefu hasa kwenye huduma ya maji na umeme.

“Viongozi wa Serikali za mitaa wakifahamu vizuri Ewura CCC tuna imani matatizo ndani ya jamii yatakwisha hasa kwenye mtatizo ya utumiaji wa maji na umeme, kwa kutatua kero ambazo zimekuwa zikiwakabili wananchi sababu mtakuwa na upeo mkubwa katika utendaji kazi wenu,”Amesema Ndatala. Naye Mwenyekiti wa wenyeviti wa viongozi wa Serikali za mitaa Nasorro Warioba. akitoa neno la shukrani ameipongeza Ewura RCC kwa kutoa mafunzo hayo ya uelewa, ambayo yamewafanya kujua namna ya kushughulikia matatizo ya maji na umeme ndani ya jamii


SOMA PIA HABARI PICHA HAPA CHINI


Mgeni Rasmi Pastor Mfoy ambaye ni Ofisa biashara wa mkoa wa Shinyanga akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack, akifungua mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo viongozi wa Serikali za mitaa juu ya kufahamu haki na wajibu wa mtumiaji wa Nishati na Maji, na kuwataka viongozi hao wakayatumie vizuri mafunzo hayo kuleta mfanikio ya kutatua matatizo ndani ya jamii hasa kwenye kero za matumizi ya maji na umeme.



Joseph Ndatala ambaye ni mjumbe wa kamati ya Ewura RCC Mkoa wa Shinyanga, akiwasilisha mada ya kufahamu majukumu ya Ewura CCC ambalo ni baraza la ushauri la mtumiaji wa huduma za Nishati na Maji, kuwa kazi yake ni kutetea na kusimamia maslahi ya mtumiaji wa Nishati na Maji, kutoa elimu kwa umma,kupokea na kusambaza taarifa,kushauriana na serikali ili kukidhi malengo ya serikali yaliyopangwa kwa mtumiaji, pia alitofautisha  Ewura kazi yake ni Kutoa Lesseni na kupanga bei ipo toafuti na Ewura CCC.

Maryciana Makundi ambaye ni mjumbe wa kamati ya Ewura RCC Mkoa wa Shinyanga akiwasilisha mada ya kujua majukumu ya kamati hiyo, amesema  kazi yake ni kusaidia na Ewura CCC ilikukamilisha malengo yake ya kutetea maslahi ya mtumiaji wa Nishati na Maji.

Mwenyekiti wa Kamati ya mkoa Ewura(RCC)Regional Consumer Consultative Wiliam Ndila, akieleza pia mjukumu Kamati hiyo kuwa ni kujenga uelewa juu ya haki na wajibu kwa kila mtumiaji wa Nishati na Maji, kusikiliza malalamiko yao na kuyafikisha kwa watoa huduma iliyapate kutatuliwa.

Katibu wa Kamati ya Ewura RCC Mkoa wa Shinyanga Zezema Shilungushela, akiwasilisha mada namna ya kuwasilisha malalamiko kwa watumiaji wa Nishati na Maji, kuwa mwananchi anapokuwa ana malalamika mfano kapelekewa billi kubwa ya maji, anatakiwa aambatanishe na vidhibitisho, pamoja na kuwasilisha malalamiko yake kwa barua na siyo mdomo.

Ofisa uhusiano na wateja kutoka Shirika la Ugavi na umeme Tanesco mkoa wa Shinyanga Vitoria Senge, akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo juu ya mkataba na haki za wateja wanaotumia Nishati ya umeme, kuwa kila mwananchi ana haki ya kuomba maombi ya kuuganishiwa umeme, kutoa malalamiko kwa barua na vidhibitisho endapo kama kwenye nyumba yake matumizi na bill ya umeme ni Tofauti, zikiwamo na bili za kubambikiziwa.

Ofisa mahusiano na wateja kutoka mamlaka ya maji na usafi wa mazingira (SHUWASA) Manka Gerald akiwasilisha mada ya mkataba wa huduma kwa wateja, kuwa kila mwananchi ana haki ya kuvutiwa maji nyumbani kwake, kutoa malalamiko endapo amebambikiziwa bill, pia kila mteja anatakiwa kulinda miundombinu ya mamlaka hiyo, kutokuiba maji ,kulipa bill za maji kwa wakati.

Mohamed Jumma ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa majengo mapya, akiuliza swali kwenye mafunzo hayo kwa upande wa SHUWASA, kuwa wamekuwa na utapeli kwenye huduma ya Service Charge ambapo mabomba ya maji yanapo haribika huambiwa wanunue vifaa, na wakati wanalipia hiyo Service Charge, pia alitoa malalamiko kwa Tanesco licha ya kuwaandikia barua kuwa kuna nguzo za umeme zipo eneo la barabara zinatakiwa kutolewa, lakini miaka mitano sasa hakuna utekelezaji, na wananchi wameanza kujenga nyumba kwa kufuata nguzo hizo za umeme na kujikuta wakijenga katika eneo la barabara, ambapo kuna weza kuja kutokea mgogoro mkubwa wa ardhi.

Deogratius Masalu ambaye ni Mtedaji wa Kata ya Chamaguha akiuliza swali kwenye mfunzo hayo, kwa Upande wa SHUWASA Kuwa kwenye kikao chao kipindi cha nyuma na viongozi hao wa Serikali za mitaa, walikubaliana na kuandika muhtasari kuwa toza ya Service Charge iondolewe, lakini wanashanghaa kwenye billi za maji bado tozo hiyo ipo, pia aliuliza swali kwa Upande wa Shirika la Umeme Tanesco kuwa kwanini wamekuwa wakisambaza Umeme mitaani kwenye nguzo zilizooza ambapo ndani ya muda mfupi zinaanza kuanguka.

Mery Makuba ni mwenyekiti wa mtaa wa Bugweto 'A' naye akichangia mada kwenye mafunzo hayo, amewalalamikia Tanesco kuwa wazembe, hasa pale wanapopewa taarifa juu ya nguzo kuanguka hawafiki kwa wakati, ambapo katika eneo lake kuna nguzo Tatu zilisha inama ndani ya miaka mitatu na zinafanya kazi, lakini hakuna matengenezo  licha ya kutoa taarifa tena kwa maandishi lakini hakuna utekelezaji.

Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Kata ya Ndembezi Solomoni Najulwa (Cheupe), akichangia mada kwenye majadiliano alitoa ushauri kwa Tanesco na SHUWASA, Pale wanapoitisha mikutano yao ya hadhara wanatakiwa wawe wanakwenda kutoa elimu hiyo kitaalamu zaidi ili kujibu maswali ya wananchi na kuondoa kero zilizopo hususani kwenye billi kubwa za maji na ongezeko la gharama za umeme.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mwadui Kisena Mahona, akichangia mada kwenye majadiliano, amesema shirika la Umeme Tanesco limekuwa kero kwa wateja wake ambapo kwenye mtaa ameshaomba umeme wananchi wake wavutiwe takribani miaka mitatu sasa, lakini hakuna majibu licha ya kuandika maombi hayo kwa barua, pamoja na kutovutiwa maji.

Ofisa uhusiano na wateja Shirika la Ugavi na umeme Tanesco mkoa wa ShinyangaVictoria Senge, akijibu maswali ya wenyeviti hao wa Serikali za mitaa, aliomba radhi kwa kutotekelezaji wajibu wao ipasavyo, na kuahidi malalamiko hayo yote yatafanyiwa kazi.

Charles Sweya ni fundi wa Shirika hilo la umeme Tanesco mkoa wa Shinyanga ,anatolea ufafanuzi wa kusambaza nguzo za umeme zilizooza, kuwa siyo kweli sipokuwa nguzo ambazo zinawekwa zimekuwa zikiooza kutokana na ardhi ya mji wa shinyanga kuwa na michwa mingi, pamoja na kuwa kama mbunga ,ambapo maji hutwama na hivyo kusababisha nguzo kuooza na kuanguka kila mara.

Ofisa rasilimali watu kutoka SHUWASA Kambila Mtebe, akijibu maswali ya wenyeviti hao wa Serikali za mitaa, kuwa suala la Service Charge lipo kisheria, na haihusiki kwenye utoaji huduma kwa matengezo madogo, bali hufanya kazi kwenye matengezo ya mabomba makubwa pale yanapo pasuka, na kubainisha kuwa adhimio la kikao kilichopita la kuondoa Service Charge hiyo bado linafanyiwa kazi.

Katibu mtendaji wa baraza la taifa Ewura CCC TAIFA Mhandisi Goodluck Mmari, akizungumza kwenye mafunzo hayo, ameipongeza Kamati hiyo ya Ewura RCC Mkoa wa Shinyanga, kwa kutoa mafunzo hayo kwa viongozi wa Serikali za mitaa, sababu watatoa elimu hiyo ndani ya jamii ipasavyo na kuondoa kero za matumizi ya maji na umeme, pia aliwataka viongozi hao malalamiko yao yasipo shughulikiwa na Shirika la umeme Tanesco ama SHUWASA Waende kwenye Ewura RCC na kisha kupelekwa Ewura CCC ambao nao watapeleka malalamiko hayo kwa EWURA ambao ndio wato Leseni na yatashughulikiwa kwa uharaka .

Viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya Ewura RCC.

Mafunzo yakiendelea ya uwasilishwaji wa mada mbalimbali.

Viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya Ewura RCC.

Viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya Ewura RCC.

Viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya Ewura RCC.

Viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya Ewura RCC.

Katibu mtendaji wa baraza la Taifa Ewura CCC (Consumer Consultative Council) mhandisi Goodluck Mmari (katikati) na wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa wenyeviti manispaa ya Shinyanga Nasorro Warioba, na wakwanza kulia ni Ofisa biashara wa mkoa wa Shnyanga Pastor Mfoy, wakisikiliza uwasilishwaji wa mada kwenye mafunzo hayo, yakiwamo maswali na majibu.

Viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya Ewura RCC.


Viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya Ewura RCC.

Viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya Ewura RCC.

Viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya Ewura RCC.

Viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya Ewura RCC .

Awali mwenyekiti wa Kamati ya mkoa ya watumiaji wa huduma ya Nishati na Maji (Ewura RCC) Wiliamu Ndila akisoma hutoba ya mafunzo hayo ya viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga, kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa wa pamoja juu ya huduma ya Nishati na Maji na kukielewa chombo  cha (Ewura CCC) namna kinavyofanya kazi, hasa juu ya kuwasilishwa malalamiko ya watumiaji na yanavyoweza kutatuliwa.

Naye Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa Nasorro Warioba. akitoa neno la shukrani ameipongeza Ewura RCC kwa kutoa mafunzo hayo ya uelewa, ambayo yamewafanya kujua namna ya kushughulikia matatizo ya maji na umeme ndani ya jamii.

Viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakipiga picha ya pamoja na Viongozi wa Ewura RCC na Ewura CCC mara baada ya kumaliza mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo.

Viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakipiga picha ya pamoja na Viongozi wa Ewura RCC na Ewura CCC mara baada ya kumaliza mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo.

Na Marco Maduhu. 








Powered by Blogger.