RAIS MAGUFULI KUMWAGA AJIRA KWA VIJANA 15,000 KUWA ASKARI POLISI
UZINDUZI: Rais Dk. John Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, wakifunua pazia kuashiria kufunguliwa rasmi kwa nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto. Uzinduzi huo ulifanyika Arusha jana. PICHA: IKULU
RAIS Dk. John Magufuli amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, kuwaajiri vijana 1,500 waliopitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa ajili ya kuitumikia polisi.
Vijana hao 1,500 ni tofauti na wale 2,356 wa JKT alioagiza juzi waajiriwe na vyombo vya ulinzi na usalama kutokana na kushiriki kujenga ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5, unaozunguka migodi ya Tanzanite iliyopo eneo la Simanjiro, Manyara.
Akizungumza mbele ya halaiki ya wananchi wa Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jana baada ya kuzindua nyumba 31 za polisi, Magufuli, alionya kuwa ajira alizotangaza zisiwe kwa ajili ya watoto wa wakubwa ndani ya jeshi hilo bali ziwe kwa vijana waliopitia JKT.
Pamoja na kumwagiza IGP Sirro kufuatilia na kusimamia mchakato huo wa ajira ili usiendeshwe kwa upendeleo, alisema yeye mwenyewe atafuatilia kwa karibu.
“IGP umesema changamoto mbalimbali hapa ikiwamo upungufu wa askari, natangaza hapa vijana 1,500 wakaajiriwe wawe askari wa Jeshi la Polisi. Katika ajira hizi waajiriwe wale vijana waliopata mafunzo ya JKT.
ELIYA MBONEA Na ABRAHAMU GWANDU-ARUSHA