TANESCO SHINYANGA YADAIWA KUSAMBAZA NGUZO ZA UMEME ZILIZOOZA
Shirika la ugavi
na umeme Tanesco mkoani Shinyanga, limedaiwa kusambaza nguzo za umeme zilizooza
kwenye makazi ya watu kwa ajili ya kuwavutia umeme, ambazo zimekuwa hazidumu na
kuaanza kuanguka hovyo, jambo ambalo linatishia maisha ya wananchi.
Hayo
yalibainishwa juzi na ofisa mtendaji wa Kata ya Chamaguha halmashauri ya
manispaa ya Shinyanga Deogratius Masalu, kwenye kikao cha mafunzo ya kuwajengea
uwezo viongozi wa Serikali za mitaa wa manispaa hiyo, juu ya kufahamu haki na
wajibu wamtumiaji wa Nishati na Maji kilicho andaliwa na Ewura RCC Mkoani humo.
Alisema Shirika
hilo limekuwa halifanyi kazi zake kwa ufanisi, kwa kusambaza nguzo zilizooza
mitaani ambapo mvua tu kidogo ikianza kunyesha nguzo zote zinaanza kuinama
chini na kuanguka hovyo, na wakiwapigia simu kwenda kuziinua wamekuwa
wakichelewa na hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi.
“Naomba kuuliza
swali kwa upande wa shirika la umeme Tanesco mkoani Shinyanga kwanini mnatabia
ya kusambaza nguzo za umeme kwenye makazi ya watu ambazo zimeoza, na mvua tu
kidogo ikinyesha zote zinainama chini na kuanguka, hamuoni kwamba mna hatarisha
maisha yetu,” Alihoji Masalu.
Akijibu tuhuma
hizo Ofisa uhusiano na wateja Tanesco mkoani Shinyanga Victoria Senge, alikiri
ni kweli nguzo nyingi za umeme katika manispaa ya Shinyanga zimeoza, na kuomba
radhi kuwa suala hilo linafanyiwa kazi ili kubadirishwa kwa nguzo zote zenye
matatizo.
Naye mhandisi wa
Shirika hilo la umeme Tanesco mkoani Shinyanga Charles Sweya, akiongezea majibu
hayo alikana kusambaza nguzo zilizooza, na kutolea ufafanuzi kuwa ardhi ya
manispaa ya Shinyanga ina michwa mingi na inatunza maji, na ndio maana nguzo
zikiwekwa hazichukui muda mrefu zinaanza kuanguka hovyo.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa kamati ya watumiaji wa Nishati na Maji Ewura RCC Mkoani Shinyanga
William Ndila, aliwataka viongozi hao wa Serikali za mitaa pindi wanapoona
malalamiko yao hayafanyiwi kazi watoe taarifa kwao kwa maandishi, ili wayafikishe
sehemu husika na kupatiwa ufumbuzi.
Alisema lengo
kuu la kikao hicho ni kuwapatia mafunzo viongozi hao wa Serikali za mitaa
ilikufahamu haki na wajibu wa mtumiaji wa Nishati na Maji, na kufahamu namna ya
kutatua matatizo ambayo yanawakabili wananchi kwenye matumizi ya maji na umeme,
zikiwamo bill kubwa na kusambaziwa nguzo zilizooza.
SOMA PIA HABARI PICHA HAPA CHINI
Ofisa uhusiano na wateja Tanesco mkoani Shinyanga Victoria Senge, alikiri ni kweli nguzo nyingi za umeme katika manispaa ya Shinyanga zimeoza, na kuomba radhi kuwa suala hilo linafanyiwa kazi ili kubadirishwa kwa nguzo zote zenye matatizo.
Alisema lengo
kuu la kikao hicho ni kuwapatia mafunzo viongozi hao wa Serikali za mitaa
ilikufahamu haki na wajibu wa mtumiaji wa Nishati na Maji, na kufahamu namna ya
kutatua matatizo ambayo yanawakabili wananchi kwenye matumizi ya maji na umeme,
zikiwamo bill kubwa na kusambaziwa nguzo zilizooza.
Joseph Ndatala ambaye ni mjumbe wa kamati ya Ewura RCC Mkoa wa
Shinyanga, akiwasilisha mada ya kufahamu majukumu ya Ewura CCC ambalo ni
baraza la ushauri la mtumiaji wa huduma za Nishati na Maji, kuwa kazi
yake ni kutetea na kusimamia maslahi ya mtumiaji wa Nishati na Maji,
kutoa elimu kwa umma,kupokea na kusambaza taarifa,kushauriana na
serikali ili kukidhi malengo ya serikali yaliyopangwa kwa mtumiaji, pia
alitofautisha Ewura kazi yake ni Kutoa Lesseni na kupanga bei ipo
toafuti na Ewura CCC.
Katibu wa Kamati ya Ewura RCC Mkoa wa Shinyanga Zezema Shilungushela,
akiwasilisha mada namna ya kuwasilisha malalamiko kwa watumiaji wa
Nishati na Maji, kuwa mwananchi anapokuwa ana malalamika mfano
kapelekewa billi kubwa ya maji, anatakiwa aambatanishe na vidhibitisho,
pamoja na kuwasilisha malalamiko yake kwa barua na siyo mdomo.
Maryciana Makundi ambaye ni mjumbe wa kamati ya Ewura RCC Mkoa wa
Shinyanga akiwasilisha mada ya kujua majukumu ya kamati hiyo, amesema
kazi yake ni kusaidia na Ewura CCC ilikukamilisha malengo yake ya
kutetea maslahi ya mtumiaji wa Nishati na Maji.
Ofisa uhusiano na wateja kutoka Shirika la Ugavi na umeme Tanesco mkoa
wa Shinyanga Vitoria Senge, akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo juu ya
mkataba na haki za wateja wanaotumia Nishati ya umeme, kuwa kila
mwananchi ana haki ya kuomba maombi ya kuuganishiwa umeme, kutoa
malalamiko kwa barua na vidhibitisho endapo kama kwenye nyumba yake
matumizi na bill ya umeme ni Tofauti, zikiwamo na bili za kubambikiziwa.
Ofisa mahusiano na wateja kutoka mamlaka ya maji na usafi wa mazingira
(SHUWASA) Manka Gerald akiwasilisha mada ya mkataba wa huduma kwa
wateja, kuwa kila mwananchi ana haki ya kuvutiwa maji nyumbani kwake,
kutoa malalamiko endapo amebambikiziwa bill, pia kila mteja anatakiwa
kulinda miundombinu ya mamlaka hiyo, kutokuiba maji ,kulipa bill za maji
kwa wakati.
Mohamed Jumma ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa majengo mapya, akiuliza
swali kwenye mafunzo hayo kwa upande wa SHUWASA, kuwa wamekuwa na
utapeli kwenye huduma ya Service Charge ambapo mabomba ya maji yanapo
haribika huambiwa wanunue vifaa, na wakati wanalipia hiyo Service
Charge, pia alitoa malalamiko kwa Tanesco licha ya kuwaandikia barua
kuwa kuna nguzo za umeme zipo eneo la barabara zinatakiwa kutolewa,
lakini miaka mitano sasa hakuna utekelezaji, na wananchi wameanza
kujenga nyumba kwa kufuata nguzo hizo za umeme na kujikuta wakijenga
katika eneo la barabara, ambapo kuna weza kuja kutokea mgogoro mkubwa wa
ardhi.
Mery Makuba ni mwenyekiti wa mtaa wa Bugweto 'A' naye akichangia mada
kwenye mafunzo hayo, amewalalamikia Tanesco kuwa wazembe, hasa pale
wanapopewa taarifa juu ya nguzo kuanguka hawafiki kwa wakati, ambapo
katika eneo lake kuna nguzo Tatu zilisha inama ndani ya miaka mitatu na
zinafanya kazi, lakini hakuna matengenezo licha ya kutoa taarifa tena
kwa maandishi lakini hakuna utekelezaji na kuahidiwa kuwa suala hilo litafanyiwa kazi.
Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Kata ya Ndembezi Solomoni Najulwa (Cheupe),
akichangia mada kwenye majadiliano alitoa ushauri kwa Tanesco na
SHUWASA, Pale wanapoitisha mikutano yao ya hadhara wanatakiwa wawe
wanakwenda kutoa elimu hiyo kitaalamu zaidi ili kujibu maswali ya
wananchi na kuondoa kero zilizopo hususani kwenye billi kubwa za maji na
ongezeko la gharama za umeme.
Mwenyekiti wa mtaa wa Mwadui Kisena Mahona, akichangia mada kwenye
majadiliano, amesema shirika la Umeme Tanesco limekuwa kero kwa wateja
wake ambapo kwenye mtaa ameshaomba umeme wananchi wake wavutiwe
takribani miaka mitatu sasa, lakini hakuna majibu licha ya kuandika
maombi hayo kwa barua, pamoja na kutovutiwa maji.
Ofisa rasilimali watu kutoka SHUWASA Kambila Mtebe, akijibu maswali ya
wenyeviti hao wa Serikali za mitaa, kuwa suala la Service Charge lipo
kisheria, na haihusiki kwenye utoaji huduma kwa matengezo madogo, bali
hufanya kazi kwenye matengezo ya mabomba makubwa pale yanapo pasuka, na
kubainisha kuwa adhimio la kikao kilichopita la kuondoa Service Charge
hiyo bado linafanyiwa kazi.
Katibu mtendaji wa baraza la taifa Ewura CCC TAIFA Mhandisi Goodluck
Mmari, akizungumza kwenye mafunzo hayo, ameipongeza Kamati hiyo ya Ewura
RCC Mkoa wa Shinyanga, kwa kutoa mafunzo hayo kwa viongozi wa Serikali
za mitaa, sababu watatoa elimu hiyo ndani ya jamii ipasavyo na kuondoa
kero za matumizi ya maji na umeme, pia aliwataka viongozi hao malalamiko
yao yasipo shughulikiwa na Shirika la umeme Tanesco ama SHUWASA Waende
kwenye Ewura RCC na kisha kupelekwa Ewura CCC ambao nao watapeleka
malalamiko hayo kwa EWURA ambao ndio wato Leseni na yatashughulikiwa kwa
uharaka .
Viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya Ewura RCC.
Mafunzo yakiendelea ya uwasilishwaji wa mada mbalimbali.

Katibu
mtendaji wa baraza la Taifa Ewura CCC (Consumer Consultative Council)
mhandisi Goodluck Mmari (katikati) na wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa
wenyeviti manispaa ya Shinyanga Nasorro Warioba, na wakwanza kulia ni
Ofisa biashara wa mkoa wa Shnyanga Pastor Mfoy, wakisikiliza
uwasilishwaji wa mada kwenye mafunzo hayo, yakiwamo maswali na majibu.
Viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya Ewura RCC.
Viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya Ewura RCC.
Viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya Ewura RCC.
Viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya Ewura RCC.
Viongozi wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya Ewura RCC .
Awali
mwenyekiti wa Kamati ya mkoa ya watumiaji wa huduma ya Nishati na Maji
(Ewura RCC) Wiliamu Ndila akisoma hutoba ya mafunzo hayo ya viongozi wa
Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga, kuwa lengo la mafunzo hayo ni
kuwajengea uelewa wa pamoja juu ya huduma ya Nishati na Maji na
kukielewa chombo cha (Ewura CCC) namna kinavyofanya kazi, hasa juu ya
kuwasilishwa malalamiko ya watumiaji na yanavyoweza kutatuliwa.
Naye
Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa Nasorro Warioba. akitoa
neno la shukrani ameipongeza Ewura RCC kwa kutoa mafunzo hayo ya uelewa,
ambayo yamewafanya kujua namna ya kushughulikia matatizo ya maji na
umeme ndani ya jamii.
Viongozi
wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakipiga picha ya pamoja na
Viongozi wa Ewura RCC na Ewura CCC mara baada ya kumaliza mafunzo hayo
ya kuwajengea uwezo.
Viongozi
wa Serikali za mitaa manispaa ya Shinyanga wakipiga picha ya pamoja na
Viongozi wa Ewura RCC na Ewura CCC mara baada ya kumaliza mafunzo hayo
ya kuwajengea uwezo.
Na Marco Maduhu ambaye pia ni mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.