Baadhi ya walengwa wa
mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf 111 kupitia mpango wa kunusuru Kaya Mskini
katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini, wamedai malipo ambayo
wanalipwa kupitia mfuko huo fedha zake ni kidogo, ambazo zimekuwa hazikidhi
mahitaji yao na kuwafanya kushindwa kuinuka kiuchumi.
Walisema malipo
hayo ambayo yamelenga kuwa toa kwenye umaskini ni kidogo sana, ambapo kila
mlengwa hulipwa fedha kutokana na idadi ya watoto wake alionao, na hivyo
kufanya baadhi yao kupata fedha kidogo kuanzia shilingi 10,000 , 20,000. na 35,000
Baadhi ya
walengwa hao walitoa kilio chao kwenye ziara ya viongozi wa Tasaf kutoka Makao
makuu Jijini Dar es salam wakiambatana na wafadhili wa mradi huo kutoka Benki
ya Dunia, iliyofanyika katika vijiji vitatu vya Isela, Singita na Bukene
Shinyanga vijijini, kuanzia April (18 -19) kwa lengo la kufanya Tathimini juu
ya mradi huo na kukusanya maoni.
Mmoja wa
walengwa hao Hadija Daudi kutoka Kijiji cha Bukene Shinyanga vijijini, alisema
fedha hizo ambazo zimekuwa zikitolewa na Tasaf baadhi yao zimekuwa hazi kidhi
matakwa yaliyokusudiwa, na hivyo kushindwa kuziendeleza kuzizalisha ili wapate
kuinuka kiuchumi na kubaki kuendelea kwa maskini.
“Fedha hizi
hulipwa kulingana na mtu ana idadi ya watoto wangapi na kujikuta wengine ambao
tuna watoto wachache huambuli fedha kidogo, na hivyo kushindwa kujibana kuweka
akiba, fedha ambazo nitazizalisha na kuuaga umaskini na kujikuta nikizitumia
zote kutimizia mahitaji ya watoto shule,”alisema Daudi.
Naye Hawa Mussa
alitoa mapendekezo kwa viongozi hao wa Tasaf, kuwa kama wanadhamila ya kuwatoa
walengwa wote kwenye dimbwi hilo la umaskini, angalau waweke kiwango kuwa kila
mlengwa bila kujali idadi ya watoto wake alipwe kuanzia shillingi 70,000 na
kuendelea, fedha ambayo itawatoa kwenye ufukara.
Nao watendaji wa
kijiji Katika vijiji vyote hivyo vitatu Isela,Singita na Bukene kwa nyakati
tofauti wakati wakisoma taarifa zao za maendeleo ya Tasaf kwenye vijiji hivyo,
Moja ya Changamoto kubwa ambayo waliisoma kuwa ni walengwa kulipwa malipo
kidogo, na hivyo kufanya baadhi yao kushindwa kutoka kwenye umaskini.
Kwa upande
Meneja wa Tathimini Tasaf kutoka makao makuu Fariji Mishael, alisema fedha
ambazo wanapewa walengwa hao siyo za kuwafanya wakae nazo kusubili ziwe nyingi,
bali ni kujibana na kununua angalau kuku na kuzizalisha na hatimaye kununua
Mbuzi hadi Ng’ombe, kama wanavyo fanya walengwa wengine ambao kwa sasa maisha
yao ni Mazuri.
Pia alitoa wito
kwa walengwa hao wa Tasaf, wajiunge kwenye vikundi vya ujasiriamali ambapo
wanaweza kuwa wanakopeshana fedha wao kwa wao kwa kufanya mzunguko, na hatimaye
kupata mitaji mikubwa ambayo itawafanya wawe na miradi ya uzalishajimali na
hatimaye kuinuka kiuchumi.
TAZAMA HABARI PICHA HAPA CHINI
Meneja wa Tathimini TASAF kutoka makao makuu Jijini Dar es salaam Fariji
Mishael, akizungumza na wanufaika wa mpango huo wa kunusuru Kaya
maskini juu ya kuanzisha miradi ya uzalishaji mali, ambayo itawasidia
kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini kabisa na kutokurudi kama
zamani.
Mratibu wa TASAF kutoka Benki ya dunia nchini Marekani ( Program
Cordinator) Krishina Pidatala, akizungumza na walengwa hao wa TASAF
Shinyanga vijijini, na kuwataka fedha wanazozipata wazitumie, kwa
madhumuni yaliyokusudiwa ili wapate kuondokana na umaskini.
Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Isela Kaya ya Samuye Shinyanga
vijijini, wakiwa kwenye mkutano wa wadau wa maendeleo na wafadhili wa
mradi huo, wakisikiliza Nasaha mbalimbali ambazo zitawafanya kuendelea
kujikwamua kiuchumi pindi mradi huo utakapokoma kutoa fedha tena kwao.
Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Singita Kata ya Usanda Shinyanga
vijijini, wakiwa kwenye mkutano wa wadau wa maendeleo na wafadhili wa
mradi huo.
Wanafunzi wa shule ya msingi Isela Kata ya Samuye Shinyanga vijijini nao wakiwa kwenye mkutano huo.
Grace Mwebeha ni mnufaika wa mradi huo wa TASAF katika kijiji cha Isela
Kata ya Samuye Shinyanga vijijini, akielezea faida aliyoipata tangu
aanze kupewa fedha hizo za TASAF mwaka 2015, kuwa amejenga nyumba ya
Bati, ana mbuzi watatu, anasomesha watoto shule na kuwatimizia mahitaji
yao, na pia anawapeleka Clinic na ameshajiunga na mfuko wa bima ya afya
CHF.
Mhoja Charles ni Mnufaika wa mradi huo wa TASAF katika kijiji cha Isela
Kata ya Samuye Shinyanga vijijini naye akielezea mfanikio aliyoyapata,
kuwa ana Kondoo 10, Mabati 30 na pia amejiunga na CHF.
Magdalena Shija ambaye ni mlegwa wa TASAF akiipongeza kwa kuwatoa
kwenye dimbwi la umaskini na kutoa maombi Muda uongezwe Pamoja na fedha
ziongezwe ili waendelee kujiimarisha zaidi hasa kwenye kufungua miradi
ya kiuchumi.
Wanafunzi wa shule ya msingi Isela Kata ya Samuye Shinyanga vijijini wakiwa kwenye mkutano huo wa TASAF.
Wadau wa maendeleo kupitia mpango huo wa kunusuru Kaya Maskini TASAF
wakielekea kwenye Kaya za walengwa kuangalia maendeleo waliyoyapa tangu
kupewa fedha hizo Mwaka 2015 kwa awamu 17.
Ester Maganga ambaye ni Mnufaika wa TASAF katika kijiji cha Isela Kata
ya Samuye akiwa kwenye nyumba yake ya Bati ambayo ameijenga kupitia
fedha za TASAF.
Ester Maganga ambaye ni Mnufaika wa TASAF katika kijiji cha Isela Kata
ya Samuye akionyesha nyumba yake ya Zamani ya Nyasi, ambayo alikuwa
akiishi kabla ya kuungwa kwenye mradi huo wa kunusuru Kaya maskini
ambapo kwa sasa ana fugia Nguruwe wawili.
Nguruwe
wa mnufaika wa TASAF Ester Maganga wakionekana ndani ya nyumba ya
majani ambayo amehama mara baada ya kujenga nyingine ya Mabati.
Ester Maganga akionyesha Ng'ombe wake watatu ambao amewapata kupitia fedha za TASAF.
Bestina Mhoja ambaye ni mnufaika wa TASAF akionyesha mbuzi wake Nane na
Kondoo Mmoja ambao amewapata kupitia fedha za TASAF, huku pia akiwa na
nyumba ya Bati ,pamoja na Kuku Saba.
Meneja wa Tathimini kutoka TASAF makao makuu Jijijni Dar es Salaam
Fariji Mishael (wa kwanza mkono wa Kushoto) akiwa na Mratibu wa mradi
huo wa Tasaf kutoka Benk ya Dunia Krishina Pidatala, pamoja na familia
ya Bestina Mhoja ambaye ni mnufaika wa mpango huo wa Tasaf wa kunusuru
Kaya Maskini.
Meneja wa Tathimini kutoka TASAF makao makuu Jijini Dar es Salaam
Fariji Mishael (wa kwanza mkono wa Kulia) akiwa na Mratibu wa mradi huo
wa Tasaf kutoka Benk ya Dunia Krishina Pidatala, wakijadili mawili
matatu wakati wakifuatilia maendeleo ya walengwa hao wa TASAF.
Mhoja Charles ambaye ni mnufaika wa TASAF katika kijiji cha Isela Kata
ya Samuye akionyesha Mabati 30 ambayo ameyapata kupitia fedha za TASAF
na anatarajia naye kujenga Nyumba ya Bati.
Mhoja Charles ambaye ni mnufaika wa TASAF katika kijiji cha Isela Kata
ya Samuye akionyesha Kondoo wake 10 ambao amewapata kupitia fedha hizo
za TASAF.
Kondoo wa Mhoja Charles kama unavyowaona.
Mhoja Charles ambaye ni Mnufaika wa Tasaf mkono wa Kulia akiwa na mkewake wakiswaga Kondoo ambao wamewapata kupitia TASAF.
Wadau wa maendeleo na wafadhili wa mradi huo wa TASAF Wakikusanya maoni
kwa walengwa hao, ili wapate kuuboresha zaidi mpango huo wa kunusuru
Kaya maskini na kuwainua kiuchumi.
Maoni yakiendelea kukusanywa.
Maoni yakiendelea kukusanywa kutoka kwa walengwa hao wa TASAF.
Ukusanyaji maoni ukiendelea.
Ukusanyaji maoni ukiendelea.
Maoni yakiendelea kukusanywa.
Mtendaji wa kijiji cha Isela Kata ya Samuye Shinyanga vijijini Bundini
Mungo, akisoma taarifa ya kijiji hicho amesema jumla ya walengwa 72 ndio
wananufaika na mradi huo sawa wakazi 432, jinsia ya Kike wakiwa
218,Kiume 214 na mpaka sasa jumla ya fedha Shilingi Milioni 46,524,000
zimeshatolewa kwa walengwa hao katika awamu 17 tangu mwaka 2015 na kubainisha changamoto ni walengwa kulipwa malipo kidogo
Mtendaji wa Kijiji cha Bukene Kata ya Bukene Tarafa ya Itwangi
Shinyanga vijijini Charles Mayunga, akitoa taarifa ya TASAF Kwenye
kijiji hicho kuwa jumla ya Kaya 80 ndio zipo kwenye mradi huo, jinsia ya
kiume wakiwa 221,Kike 208 na kubainisha kuwa jumla ya Shilingi Milioni
49,492,000 zimeshatolewa kwa walengwa hao tangu mwaka huo 2015, na kubainisha moja ya changamoto kubwa kwa baadhi ya walengwa hao ni kulipwa malipo kidogo.
Josiah
Colonel ni mtendaji wa Kijiji cha Singita Kata ya Usanda Shinyanga
vijijini, akisoma taarifa ya TASAF kijijini humo, amesema jumla ya
walengwa 106 ndio wananufaika na Mpango huo, Jinsia ya Kike wakiwa 45 na
Kiume wakiwa 61 ambapo jumla ya Shilingi Milioni 100,504,000
zimeshatolewa kwa walengwa hao, na kubainisha changamoto inayowakabili baadhi ya walengwa hao ni Malipo kidogo.
Mratibu
wa TASAF halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini Happnes Shayo,
anasema jumla ya Kaya 8787 zimenufaika na Mradi huo, na kubainisha kuwa
jumla ya Shilingi Bilioni 5,519,652,000 zimeshatolewa kwa walenga hao
hadi mwezi April mwaka huu.
Kikundi cha Ngoma cha Ugoyangi kutoka Kijiji cha Usule Kata ya Bukene
Shinyanga vijijini wakitoa Burudani kwenye mkutano huo wa TASAF wa
kufanya Tathimini ya mradi huo kwa walengwa, na namna wanavyonufaika nao
na kuwatoa kwenye Dimbwi la Umaskini.
Burudani zikiendelea kwa kuonyesha utaalamu wa kucheza na Nyoka.
Kikundi cha Ngoma cha Jembe kutoka kijiji hicho cha Bukene Shinyanga vijijini kikijiandaa kutoa burudani.
Kikundi cha Jembe kikitoa burudani.
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Shinyanga Vijijini Happnes Shayo akifurahia jambo.
Burudani zikiendelea.
Kikundi cha Ngoma ya Ugoyangi wakiendelea kutoa burudani katika kijiji
cha Bukene leo, wakati wa ufangaji mkutano wa Tathimini na uchukuaji
maoni nini kiboreshwe kwenye mradi huo wa TASAF kipindi kijacho.
Burudani zikiendelea.
Mwandishi wa Habari Gazeti la Dailynews Suleiman Shaghata mkono wa
kulia akibadilishana mawazo na Mratibu wa TASAF Kutoka Benk ya Dunia (
Program Coordinator) Krishina Pidatala.
Mratibu wa TASAF Kutoka Benk ya Dunia ( Program Coordinator) Krishina
Pidatala akipokea Zawadi kutoka kwa walengwa wa TASAF ,Sanamu ya Rais
John Pombe Magufuli.
Zawadi.
Pokea Zawadi.
Burudani zikifunga mkutano huo wa TASAF katika kijiji cha Bukene Shinyanga vijijini.
Na Marco Maduhu ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga